Ni bahati mbaya kwamba inaonekana wengine uongo ni kama sehemu ya imani yao. Yeyote anayesema kuwa hakuna udini eti ameusikia kwa Kikwete tu na wengine Redio Iman, huyo ni muongo na anaweza kuongea lolote la kudanganya.
Asanteni
Nadhani kuna ushindan wa kisiasa, kuanzia serikalin, chama tawala na hata upinzani. Swala la udini limekuwa agenda mhm kwa wanasiasa. TZ HATUJAFIKIA THAT KIWANGO! Kauli za Jk ndio cheche za moto wa udini tz, hii nikwa maoni yangu mimi!
Nafsi yake inamsuta. Mwanasiasa pekee aliyehubiri UDINI wakati wa kampeni alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete. Alisaidiana na mtoto wake Miraji ambaye mama yake ni Mkristo. Mpambe mkuu wa Jakaya na Mwanae Miraji katika jitihada za kueneza udini alikuwa Shamte wa Six Mobile aliyeumbuliwa na Gazeti la Guardian. Mjinga mwingine aliyezungumzia UDINI alikuwa Zito Kabwe, aliyekuja kupata uenyekiti wa kamati ya bunge kwa msaada wa JK.Ndugu wanaJF wenzangu nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kuwa ni muda sasa tangu hubiri za Jk juu ya wanasiasa watumiao dini zianze kusikika. Mwanzo wa haya ilikua kipindi kile cha kampeni wkt wa uchaguzi mkuu, pungeni akihutubia Bunge, ktk hotuba zake za mwho wa mwezi na hata apatapo nafasi popote pale.
Jana akiwa km mgeni rasmi ktk tamasha la Pasaka amepata kusikika akisisitizia juu ya udini..safari ameenda mbali zaidi akikesa/akiwataka watanzania tukumbuke kuwa UHURU WA WATANZANIA ULILETWA NA WAKRISTO NA WAISLAM WAKISHIRIKIANA KWA PAMOJA, Kifupi mimi simwelewi na sielewi haswa anachomaanisha. Siasa na dini zisichanganywe kivipi? Yeye ni Rais, mwanasiasa na mwenyekiti wa chama tawala, ktk tamasha la pasaka yeye km mwanasiasa kafata nin? Si wadhehebu hzo. Nani mdini? Nadhan Rais anapaswa kuwa direct ktk hili, atueleze kinagaubaga juu ya hili, zaidi ya hapo nikama vile mchezo wa kuvua dagaa kwa karabai. Wenzangu mnamuelewaje mheshimiwa wetu? Nawasilisha hoja!
mkuu kauli kama hizo si nzuri na hazitatufikisha pazuri. Katika dunia hii hapajatokea kuwa na wailam pekee au wakristo pekee. Kwa hiyo kila mmoja aone mwenzake bila yakujali dini yake kabila yake anahaki zote za msingi ikiwa ni pamoja na kuongoza/ lakini pale mmoja anapomuona mwengine hafai kuwa ikulu kwa sababu tu si waimani yake basi hilo ni tatizo na linapaswa kushughulikiwa. Frankly writting, mimi siipendi ccm sio leo tu tangu enzi hizo lakini kwa kauli kama hizo za akina mtikila haziniweki mahala pazuri kiimani.
We need changes. Lets make, na tuachane na mabo ya udini. Otherwise tunakoelekea si pazuri. Angalia michango ya wengi humu, imekaa kidini tu. Imefikia mpaka nikawa nafikiria hii jf ifutwansi kwa sababu ya hatari ya kisiasa bala ya kidini, wengi humu tuna ndugu wa damu wa dini tofauti, majirani, marafiki, mabosi na hata mademu/mameni. Ndo maana najaribu kuiangalia hatari hiyo kwa jicho la tatu. Ni hayo tu.
Radio Imaan bado inaendelea kuwahimiza waislamu wasishirikiane na wakristo. Trh 21 jioni niliisikia Radio Imaan ikiwahimiza waislamu wawe tayari kwa lolote kama madai yao hayataingizwa kwenye katiba mpya.
Madai yenyewe:
1. Waislamu ndo walioleta uhuru hivyo madaraka serikalini lazima iwe 50/50.(eti wakristu waliopigania uhuru hawazidi 10 nchi nzima!)
2. Mahakama ya Kadhi lazima iwemo, na majaji wake lazima wahudumiwe na serikali kwa 100% kama majaji wa mahakama za taifa!
3. Na utumbo mwingi unao fanana na huo!
Nilishindwa kuelewa kama nchi hii imefika huko na vyombo vya dola havichukui hatua. Kama wameshindwa kuifungia Radio Imaan, basi wana-back up ya JK ili lengo lake litimie! Kwa taarifa yao "WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA!"
Udini hata JF upo.
Mkubwa Anheuser Huo udini uko vp? Fafanua!