Tupeane uzoefu,stress za maandalizi ya ndoa.

Tupeane uzoefu,stress za maandalizi ya ndoa.

Mahari 30000 na msaafu,30000 kofia kanzu na sendles,10000 tax,iliyobakia chakula cha usiku nyumbani kwangu
Hahaaa mkuu hebu nifafanulie hii Tsh 100000/=,uliimeneji vp ikakufankishia jambo hili?,[emoji23][emoji23][emoji23]
Unaweza ukacheka mpaka basi aise

Sent from Nokia 7 Plus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tuli budget laki tano enzi hizo ilitosha usiku wa ngoma kwetu na subuhi saloon baada ya hapo kanisani na reception. Tuliweka akiba ya laki sita kwa honey moon Mombasa.

Madada walinistukiza na kitchen party

Familia ilifanya send off

Na baada ya kanisani familia ya mume ilifanya reception.
 
Niliapa binti atakebeba mimba yangu ataitwa mke wangu officially, mara pap binti wa kimasai kaidaka,na kwa process za hiyo kabila nilijua nimeukwaa mkenge,ila kwa sarakasi nilizozifanya,hata wao hawakuamini,laki 650,0000/=zangu zilitosha kabisa kumaliza kila kitu,mahari,faini na yale mapombe yao,nikarudi zangu kanda ya ziwa kuendelea na harakati za maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Kuna Siri gani siku ya honeymoon.
Nasikia watu huwa wanakamiana usiku huo balaaaa, hebu tupe uzoefu wako kwa sisi ambao hatujaoa
Sisi tuli budget laki tano enzi hizo ilitosha usiku wa ngoma kwetu na subuhi saloon baada ya hapo kanisani na reception. Tuliweka akiba ya laki sita kwa honey moon Mombasa.

Madada walinistukiza na kitchen party

Familia ilifanya send off

Na baada ya kanisani familia ya mume ilifanya reception.
 
Hivi Kuna Siri gani siku ya honeymoon.
Nasikia watu huwa wanakamiana usiku huo balaaaa, hebu tupe uzoefu wako kwa sisi ambao hatujaoa
There is a special feeling to know that in God’s eye two of you are united.
 
There is a special feeling to know that in God’s eye two of you are united.
Hahahaha Kuna zaidi ya hiki bhna.
Yaani siku hiyo ikifika kwangu nasema walai nitapiga mazoezi mwezi mzima ya maandalizi
 
Hahahaha Kuna zaidi ya hiki bhna.
Yaani siku hiyo ikifika kwangu nasema walai nitapiga mazoezi mwezi mzima ya maandalizi
Mnakuwa mmechoka harusi inachosha hasa pale pa kusimama na kupokea zawadi
 
Nitawapa mifano miwili:
1. Mimi nimeoa mwaka 2010 na bajeti ya sherehe peke yake ilikua milioni 12 hivi. (Hiyo ni nje ya pete, suti yangu na mshenga, gauni la bibi harusi, sare za maids 8, nguo za wazazi pande zote, gharama za honeymoon, send off pia nilichangia, na hapo sijahesabu gharama za kabla ya harusi kuanzia kuvikana pete, wazazi kwenda kujitambulisha, wazazi wake kuja kwetu (lazima sherehe) n.k n.k

Ili kuweza kufanikisha harusi hiyo, ilinibidi nihangaike sana ikiwa ni pamoja na kukwangua akaunti yangu benki, kuzungusha kadi za michango kila mahali hadi kwa watu nisiowajua kivile, yaani ilikua tabu kweli kweli. Mimi na ndugu zangu pia ilibidi tuzunguke huku na kule kuomba omba michango, kulia lia, na kujidhalilisha ili tu harusi hiyo ifanikiwe!

2. Rafiki yangu mmoja alioa mwaka mmoja baada yangu. Mimi binafsi alinitaarifu kuhusu harusi siku mbili kabla. Hakufanya vikao, hakutembeza kadi, hakukuwa na sherehe za kuvikana pete, send off wala nini. Siku ya harusi alitualika kanisani ambapo pia walikuepo wazazi wa pande zote, ndugu na jamaa wa karibu wasiozidi 20. Ndoa ilifungwa saa 10 na baada ya hapo alitualika chakula cha jioni kwenye hoteli moja nzuri tu. Hakukuwa na MC, tarumbeta, Mziki, mapambo, matenti, flat screen, wala vikorokoro vingine tulivyovizoea. Watu tulikula, tukanywa na tukafurahi na kupiga picha chache na maharusi. Saa nne kamili kila mtu yupo kwake. Kwa mahesabu ya haraka ile shughuli haikugharimu zaidi ya 2m na rafiki yangu hakuhangaika kabisa.

Leo ni miaka karibu 10 imepita, wote tunaishi kwa furaha na amani. Lakini ninapolitazama tukio lile naona kabisa kwamba kama ningekua najua ninachokijua sasa, ningefanya kama alivyofanya rafiki yangu.
 
Back
Top Bottom