Tupeane uzoefu siku ya kwanza kuja bongo

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,091
8,547
jamani tupeane uzoefu siku yako ya kwanza kuja dar ws salaam aka bongo ilikuwaje?
na je kwanin vijana wengi wanaoishi dar hawana maendeleo kiasi cha kushindwa na wageni wanaotoka mikoani kwa maisha mazuri?
 
Baada ya kumaliza darasa la saba mwaka1990, nikaondoka na mwenyeji wangu kwenda Dar. Tulisafiri kwa treni lililokuwa linaanzia safari yake Moshi. Sisi tulipakilia Korogwe. Sikumbuki tuliingia Dar saa ngapi. ila ni kabla ya alasiri. Tukio ambalo sijalisahau ni wakati navuka barabara ya stesheni. nilikoswakoswa na gari. Mwenyeji wangu alijisahau kunishika mkono. Basi baada ya hapo ikawa kila tukitaka kuvuka barabara ananishika mkono hadi tukafika nyumba. Kuna mabasi fulani walikuwa wanaita ikalusi ni kama haya ya mwendo kasi. Nilishangaa magari marefu vile.
Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom