Tupeane fursa!

suluta

Senior Member
Dec 22, 2016
115
40
Habari zenu wana JF, naamin mpo salama na amani imetawala.

Wadau mimi binafsi nilitaka tu tushirikishane fursa mbali mbali zilizopo kwa sasa. Naamini kila mtu anakubali kuwa hali ni ngumu sana SEMA ugumu wa hali halisi unatofautiana.

Nimekaa nikawaza sana, kwani hakuna uwezekano wa serikali kutenga maeneo katika kila wilaya jwa ajili ya vijana ambao hawana ajira rasmi WAKAUNGANA by whichever means possible wakaanzisha miradi ya maendeleo?

Asimia kubwa ya nchi yetu ni maeneo ya wazi ambayo kwa kilimo au hata ufugaji yanafaa sana.

Kama hilo haliwezekani, sisi kama vijana tuungane kwa pamoja bila kujali ITIKADI ZETU ZA KIDINI, SIASA, AU KABILA. Tuungane pale panapowezekana tufanye mambo ya maendeleo. Kutokujuana isiwe sababu ya sisi kuendelea kuishi kwa shida na kulalamikia serikali.

NI MTAZAMO WANGU TU. samahani kama ntakuwa nimekosea.
 
Ni mawazo mazuri pia, ila msingi ni kuanza sisi kama sisi na si tuisubir serikal kututengea maeneo hilo hapo naona mchakato utakua mrefu hivyo tutachelewa
 
Hakuna mtu atakaekuonesha fursa, Ubunifu wako ndio utakaokutoa hapo ulipo na kukufanya upige hatua ya maendeleo Fursa zote watu wameshaziona na kuzifanyia kazi ila ukibuni ndani hizo hizo fursa utatoka tu
 
Fanyia kazi hii
 
Habari wana JF,

Sasa hivi nchini hapa pamekua na upepo wa ujasiriamali hasa kwa vijana, vijana wengi hasa ambao wametoka vyuoni wamekua na mawazo tofauti tofauti ya ujasiriamali ambayo yanaweza kuwa tija kwa jamii na kwao binafsi lakini ni wachache sana kati ya wote ambao wamefanikiwa kikwazo kikubwa kikiwa ni mitaji.

Utamaduni wa kuwekeza kwenye makampuni yanayochipukia haupo au ni mdogo sana nchini kwetu hapa, mtu kama WARREN BUFFET amepata utajiri kwa uwekezaji wa makampuni yenye thamani ndogo lakini akaweka enough capital ambayo baadae anapata faida kubwa sana. Nimeona watu wengi wakiwa na idea zenye thamani kubwa sana kama wakizitekeleza lakini zimeishia vichwani mwao ukosefu wa mtaji.

Mtu akiwa na wazo na akawafuata ndugu au marafiki waweze kuwekeza wengi wao huchukulia kama mtu anaomba msaada na sio wao kuichukulia kama fursa. Mfano kama mtu angewekeza kiasi kidogo cha fedha kwenye kampuni ya MAXMALIPO wakati inaanza leo hii angekua millionea na mmiliki wa kampuni kubwa nchini.

Kutokana na hilo nimefikiria yafuatayo

1. Mitaji ipo lakini watu hawajui jinsi ya kuipata

2. Kuna watu wana mawazo sawa na wanaweza kushirikiana na kutoa kitu bora zaidi

3. Kuna watu wana mitaji lakini hawajui wapi wawekeze

4. Kuna watu wana uelewe wa wapi mjasiliamali aende ili kuweza kupata mitaji

Ninashauri yafuatayo

1. Wajasiliamali waweze kujadili humu nu jinsi gani wanaweza kuyapa uhai mawazo yao

2. Watu wenye fedha za ziada waweza kuona hii ni kama fursa na wajaribu kuwasiliana nakuangalia namna ya kushirikiana.

3. Watu watoe ushauri ni jinsi gani mtu anaweza kuwekeza fedha zake na kuepuka kutapeliwa na wanaojifanya wana mawazo lakini kumbe ni matapeli tu.

4. upatikane ushauri ni jinsi gani mtu anaweza linda idea yake kutoka kwa wawekezaji uchwara ambao lengo sio kuwekeza ni kukusikiliza na kukukimbia kwenda kufanya wao.

5. Watu wenye idea tofauti tofauti tukutane hapa na wanaohitaji kuwekeza

6. Ujasiliamali sio lazima utoe idea kichwani kwako hata kuwekeza kwa wengine ni ujasiliamali pia

NAWASILISHA
 
Imefikia 70,000
Siwez pata kwa bei ya 50 kiongozi
 
Back
Top Bottom