Wanyakyusa wamebaini fursa makanisani

Wanyakyusa wamebaini fursa makanisani

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
Kuna utani wa kitaifa kuwa huwezi kumtenganisha Mnyakyusa na tunda la parachichi.

Huu ni utani usioumiza unaokaribiana na ukweli kwa sababu parachichi ni tunda pendwa kwa watu wa jamii ya Kinyakyusa hasa watu wa Tukuyu.

Leo nataka nikuambie jambo moja ambalo tukiachana na utani wa parachichi basi tunaweza kuwazungumzia Wanyakyusa kwa undani zaidi tena kwa usahihi.

Bila shaka umepata kusikia maneno kuwa Mbeya kuna makanisa mengi hadi kufikia kanisa kuitwa kwa jina la muanzilishi mfano kwa mchungaji fulani.

Katika wingi huo wa makanisa basi wanyakyusa hawajakaa mbali nayo ndio wamayashikilia kwa kiasi kikubwa.

Linapokuja suala la dini wanyakyusa wengi wanakubalika sana kuna wakati unawaza, nguvu hii ya ushawishi ni ya kiasi gani Mungu aliiweka ndani ya mnyakyusa?

Kuna mwaka nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa nilikuwa nazunguka maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa kwa ajili ya majukumu ya kimasomo nilipita eneo fulani la makazi ambalo limejificha kando ya milima na majabali, nilifika eneo nikakuta jengo dogo la miti mithiri ya kambi nikaendelea mbele baada ya kutembea hatua kadhaa nikawakuta vijana watatu wa kiume na wa kike mmoja wakifyatua tofali za tope kwa ajili ya kuzichoma zitumike kwenye ujenzi.

Nilishangaa kusikia mazungumzo yao kwa lugha ya kinyakyusa nikawaza hawa watu wamefuata nini huku? Nikageuka nyuma nikaliona tena lile jengo nikakumbuka kuwa kabla sijafika eneo lile nilikikuta kibao cha kuashiria kuwa mbeleni kuna kanisa la Kipentekosti.

Sikutaka wagundue kuwa nimewabaini na kuelewa utambulisho wa lugha yao nikawasalimu kwa kiswahili nikaendelea na safari yangu.

Sio Iringa tu hata ukienda miji mingine nchini wanyakyusa wamesambaa kama wamisionari wa dini ya kikristo wamejenga makanisa na kukusanya waumini.

Wanyakyusa wamekuwa viongozi katika makanisa ndani na nje ya Tanzania iwe kwa kuhubiri, kuimba au kuratibu mambo mengine ya kidini tena kwa kuaminiwa na jamii husika haijalishi wapo ugenini kiasi gani.

Ingawaje suala la dini ni wito wa kiMungu wenye kuhitaji watu kujiweka wakfu ili kumtumikia Mungu kwa kiasi fulani uongozi wa dini umefungua milango ya fursa ya kiuchumi kutokana na mzunguko wa maisha ya sasa.

Wachungaji wanajengewa nyumba, wananunuliwa mashamba wengine wananunuliwa na magari kabisa.
Kuna baadhi ya Taasisi za kidini zimeimarika kiuchumi zinamiliki miradi mikubwa ya biashara hivyo inatoa fursa kwa Viongozi wa taasisi husika kuneemeka kiuchumi kutokana na posho na mishahara.

[emoji2398] Peter Mwaihola

Photo_1732204457672.jpg
 
Top 3 ya Wajasiliamali wa dini maarufu Tanzania wanaotoka/wenye asili ya Mbeya
1. Mwamposa
2. Lusekelo
3. Mwakasege
 
Mnyakyusa Ambilikiile Mwasapile (Babu wa Loliondo - Samunge) aliweka rekodi ya pekee ya kukusanya umati wa watu wengi sana kutoka kila kona ya nchi na hata nje ya nchi. Alipata wapi nguvu za mvuto wa pekee kiasi kile kwa kutumia kikombe tu?!

Wengine wote waliojaribu kuiga walikosa wafuasi.
 
Back
Top Bottom