NA MARYAM HASSAN
WAKATI dunia ikiendelea kupaza sauti juu ya ushiriki na ushirikishwaji kikamilifu wa wanawake katika nafasi mbali za uongozi, Zanzibar haipo nyuma katika haraakati hizo.
Kupitia Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) na wadadu wengine wamekuwa wakiendelea na harakati za kupigania wanawake ili kutimiza ndoto za wanawake wengi ambazo zinakatishwa na wenye dhamira binafisi zikiwepo kuwadumaza wanawake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Zanzibar ikiwa sehemu inayounda Jamhuri hiyo katika ibara ya 13(1) inatilia mkazo usawa wa watu wote mbele ya sheria na kwamba wana haki, bila ya ubaguzi wowote ya kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
Kupata Taarifa na Matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 pamoja na Zanzibar
Kwa msingi huo wa katiba ya Tanzania chini ya kifungu hicho, ni wazi kuwa nchi inatambua haki ya kila mtu kuwa kiongozi, hivyo hakuna budi wanawake wengi zaidi kupewa nafasi za uongozi ili kutekeleza haki hii muhimu ya kikatiba.
Msingi huu wa katiba unatiliwa mkazo na wadau mbali mbali ikiwemo TAMWA-ZNZ, kupitia utekelezaji mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi .
Chini ya mradi huo TAMWA- ZNZ, imefanikiwa kuwafikia wananchi wapatao 8,793 kati yao wanawake wakiwa 5,276 na wanaume 3,217 katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Licha ya kuwa jitihada kubwa zimefanyika lakini nguvu kazi zaidi inahitajika ili kufikia malengo ambayo ni kuleta usawa katika nafasi mbali mbali za uongozi kwa wanaume na wanawake sambamba na ushiriki wa wanawake katika demokrasia.
Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni wakati akitangaza matokeo ya idadi ya sensa ya watu na makaazi, Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alisema Zanzibar kama sehemu ya Jamuhuri ya Muungano, ina watu wapatao 1,889,773 kati yao wanaume ni 915,492 sawa na asilimia 48.4 na wanawake ni 974,281 sawa na asilimia 51.6.
Pamoja na matokeo hayo ya sensa kuonesha wingi wa idadi ya wanawake hapa nchini kuliko wanaume, bado hali halisi ya ushiriki wa wanawake katika uongozi haijaridhisha.
Wakati hayo yakijiri kwa upande wa takwimu za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2022 Zanzibar ilikua na idadi ya wapiga kura wapatao 566,352.
Kati ya hao wanawake ni 294,237 na wanaume ni 272,115 pamoja na takwimu hizo kuonesha wanawake ndio wapiga kura wengi zaidi katika uchaguzi huo, bado nafasi za ushiriki wanawake katika nafasi za uongozi haziendani na uhalisia wa wingi wao jambo ambalo, linawafanya wadau kujiuliza kilikoni? Vikwazo viko wapi hati wanawake kutupwa nje kwenye nafasi za uongozi?
Makala hii inafafanua namna katiba za vyama vya siasa zinavyotoa fursa za nafasi za uongozi ili kufikia 50 kwa 50, ambapo katiba nyingi hutoa vipengele vinavyohakikisha uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.
KAULI ZA WANASIASA
Katibu wa ngome ya wanawake ngazi ya Taifa katika Chama cha ACT Wazalendo, Fatma Abdulhabib Ferej, anaeleza katiba ya chama hicho inaeleza wazi usawa baina ya wanawake na wanaume.
Katika katiba hiyo alifahamisha kuwa imeonesha namna gani imejipambanua kutoa nafasi hizo kupitia ngazi ya tawi, kata, majimbo, mikoa na kitaifa kwa pande zote mbili za Tanzania na Zanzibar.
Fatma anaeleza kuwa katiba hiyo imeeleza kuwa hakutakuwa na viongozi katika majimbo, tawi kuongozwa na wanaume peke yao, bali zipo nafasi zimewekwa ili kutoa kipaumbele kwa wanawake.
“Katiba ya chama chetu ukurasa wa 21 kifungu cha 39(h), kinaeleza kuwa; kutakuwa na wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa kamati ya uongozi ACT jimbo ambao watachaguliwa na mkutano mkuu kati ya hao wanawake wawili na wanaume wawili”, alisema.
Alisema lengo la katiba ya chama kuekwa kifungu hicho ni kuondosha ukiritimba wa mfumo dume kutawala kwenye nafasi za uongozi, jambo ambalo linawanyima wanawake kusikika sauti zao.
Anaeleza kwamba ndani ya katiba hiyo ukurasa wa 36 kifungu cha 63 (e) kinaeleza kuwa wawakilishi wawili wanachama wa chama hicho nje ya nchi ibainishe kuwa angalau mmoja awe mwanamke na awe raia wa Tanzania.
“Kifungu hicho hicho (h)kinaeleza kuwa wawakilishi10 wa madiwani waliochaguliwa na jumuiya zao kati yao watano Zanzibar na watano Tanzania bara ba ambao angalau theluthi moja wakiwa wanawake kwa kadri iwezekanavyo”, aliongeza.
Kwa upande wa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis anaeleza kuwa katika katiba Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema zipo nafasi maalum ambazo zinawahusu makundi maalum hususan wanawake.
“Ndani ya katiba ya CCM tumeeleza wazi kuwa nafasi maalum hizi ni za wanawake kupitia makundi yao ya vijana, wazazi, nahii UWT” alisema.
Alisema mfumo wa kupata viongozi hutolewa upendeleo wa jinsia na kutoa mfano wa kwenye jimbo katika kura za maoni ambapo wanaume waliongoza katika nafasi za juu kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tatu huku mwanamke akiwa nafasi ya nne, kupitia vikao vya kamati humchukua mwanamke ambae alishika nafasi hiyo na kumueka katika tatu bora ili kupelekw katika vikao vya uteuzi hata kama hakupata zile alama zilizowekwa.
Mbeto alitanabahisha kuwa CCM inatekeleza katiba yake ipaswavyo licha ya kuwepo baadhi ya wanawake kuwa na hofu ya kuingia katika majimbo.
Katika mikakati ya chama kinaendelea kuhamasisha wanawake kuogembea nafasi za uongozi kwa sababu nafasi hizo zimewekwa na zinapewa kipaumbele.
MKURUGENZI TAMWA-ZNZ
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ, Dkt. Mzuri Issa anasema wamekua wakifanya harakati hizo kwa muda mrefu na kwa kiasi fulani wameanza kufahamika kwenye jamii.
Alisema wakati wanaanza harakati za kuwapigania wanawake jamii iliwashangaa sana na kuwaona kama watu wa ajabu wasiojua watendalo lakini leo hii watu wameanza kuelewa ukweli na kuwaunga mkono ingawa kwa asilimia ndogo sana.
Hata hivyo alisema jitihada za pamoja kwa wananchi wote na Asasi za kiraia zinazhitajika kumkomboa, mwanamke katika makucha ambayo yamewafanya kuwa watu wa kuongozwa na sio wakuongoza, jambo ambalo anaamini kuwa ni kutowafanya wanawake wengi kushindwa kupiga hatua za kimaendeleo.
Akifafanua zaidi alisema pamoja na jitahada mbali mbali za maendeleo zinazoendelea kufanyika hazitaweza kufanukiwa kwa asilimia mia iwapo ushiriki wa wanawake hautaongezeka na kuwa mkubwa zaidi ikiwezekana kutia kwa falsafa nzima ya hamsini kwa hamsini.