Tupeane connection za mashamba/viwanja vya gharama nafuu

Brother Jof

Senior Member
Nov 5, 2018
105
134
Hello wanajukwaa,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Naomba tupeane connection za maeneo ambayo kuna viwanja au mashamba makubwa kwa bei nafuu kwaajili ya uwekezaji au ujenzi.

Mimi binafsi niko Dar, natamani sana kupata eneo au shamba lenye rutuba nzuri angalau ekari 10 pembezoni mwa jiji au katika mkoa wa Pwani kwa gharama ya wastani wa milioni moja (1,000,000Tsh) ili nikajichimbie huko nilime na kufuga. Maeneo ninayopendelea ni kama Kisarawe, Chanika (ndanindani huko), Bagamoyo, Wilaya ya Kibaya, Mkuranga n.k.

Asanteni
 
Million 1 heka kumi? Labda tufunge na kuomba sana,tena tuombe maombi ya kichawi wamiliki wapate shida kubwa, wawe na uhitaji mkubwa sana wa hela kisha maninja tutokee na milioni moja moja zetu tuwakomalie watukatie heka kumi kumi.

Bongo nyoso aiseee....
CC:-
Mfalme Fadhageti
Mkuu nishawah kusikia sehem hii ndio maana nikaja hapa nipate wadau wenye connection
 
Miono iko wilaya ya chalinze,bei laki mbili mpaka laki,usafiri toka mbezi mwisho au tegeta nyuki moja kwa moja
Labda miono ndani ndani hukooo lakini pale karibu Sasa kwa hiyo bei itamlazimu afunge na kuomba na kuwapiga upofu na dhiki wamiliki wauze Bei aitakayo.

Kule mbele ya miono maeneo ya Mandamazingara kwenyewe kumeshapanda vile barabara ya east Afrika yapita hapo.
 
Labda miono ndani ndani hukooo lakini pale karibu Sasa kwa hiyo bei itamlazimu afunge na kuomba na kuwapiga upofu na dhiki wamiliki wauze Bei aitakayo.

Kule mbele ya miono maeneo ya Mandamazingara kwenyewe kumeshapanda vile barabara ya east Afrika yapita ndani ndani kama unaenda tanga

Miono heka kumi kwa milioni moja?
Upande upi wa miono?
 
Back
Top Bottom