Sisi wakazi wa kigamboni tumepokea uamuzi wa Bunge letu Tukufu kwa furaha kubwa mno. Tunajua kabisa kwamba kumbakumba hili litampitia hata huyu Waziri wetu mtata - wa ardhi kama mlivyolifuatilia sakata zima la Tegeta mihela kwenye magunia - aka Escrow.
Hapa tunajifunza kwamba:- Fanya ufanyavyo lakini malipo huwa ni hapa hapa duniani - ni ukweli ulio wazi sisi wakazi wa kigamboni tumeishi zaidi ya miaka 8 kama ndege msituni, kama digidigi - yaani bila kujua kesho yetu juu ya mradi huu uliogubikwa na usiri mkubwa wa Kigamboni New City.
a) Hatukopesheki - dhamana ya ardhi ama vibanda vyetu havitambuliki
b) Hatuwezi kuendeleza makazi yetu
c) Hatujui hatma yetu hasa kwenye huu usiri mzito wa mji mpya wa kigamboni
Sara zetu, Dua zetu zimetimia - hatimaye mama aliyekuwa kigingi kwenye mradi huu amepatikana na hatia. Hili kwetu ni faraja kubwa - Mwenyezi Mungu kapokea Sara / Dua zetu.
Ombi: Tunaomba Mamlaka ya uteuzi itupatie Waziri atakayekuja kulimaliza jambo hili kwa UWAZI na UKWELI - tumechoka kuishi kama digidigi ndani ya nchi yetu.
Kwa niaba ya wakazi wa kigamboni - Mji Mpya.
Natoa HOJA: