Tupatieni WAZIRI wa Ardhi mwenye UWEZO na hofu ya Mungu!!

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
19,834
2,000
Sisi wakazi wa kigamboni tumepokea uamuzi wa Bunge letu Tukufu kwa furaha kubwa mno. Tunajua kabisa kwamba kumbakumba hili litampitia hata huyu Waziri wetu mtata - wa ardhi kama mlivyolifuatilia sakata zima la Tegeta mihela kwenye magunia - aka Escrow.

Hapa tunajifunza kwamba:- Fanya ufanyavyo lakini malipo huwa ni hapa hapa duniani - ni ukweli ulio wazi sisi wakazi wa kigamboni tumeishi zaidi ya miaka 8 kama ndege msituni, kama digidigi - yaani bila kujua kesho yetu juu ya mradi huu uliogubikwa na usiri mkubwa wa Kigamboni New City.

a) Hatukopesheki - dhamana ya ardhi ama vibanda vyetu havitambuliki
b) Hatuwezi kuendeleza makazi yetu
c) Hatujui hatma yetu hasa kwenye huu usiri mzito wa mji mpya wa kigamboni

Sara zetu, Dua zetu zimetimia - hatimaye mama aliyekuwa kigingi kwenye mradi huu amepatikana na hatia. Hili kwetu ni faraja kubwa - Mwenyezi Mungu kapokea Sara / Dua zetu.

Ombi: Tunaomba Mamlaka ya uteuzi itupatie Waziri atakayekuja kulimaliza jambo hili kwa UWAZI na UKWELI - tumechoka kuishi kama digidigi ndani ya nchi yetu.

Kwa niaba ya wakazi wa kigamboni - Mji Mpya.

Natoa HOJA:
 

duanzi

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
16,446
0
Mama Anna Tibaijuka anatosha kuwa waziri wa Ardhi. Nimchapakazi, Mwadilifu, Pesa alizopewa na Rugemalira ni safi kabisa amepewa na kaka yake. Watanzania acheni wivu.
 

duanzi

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
16,446
0
Wakazi wa Kigamboni msiwe na wasi wasi mtalipwa fidia. Sasa hivi serikali haina pesa Mpaka kufikia mwaka 2020 mtaanza kulipwa fidia, punguzeni presha.
 

andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,225
Ni bora atoke sasa kabla ya dili lake la Kigamboni Development Authority na wahaya wenzake wa UTT na Orbit Securities halilipuka tena

Mama Anna Tibaijuka anatosha kuwa waziri wa Ardhi. Nimchapakazi, Mwadilifu, Pesa alizopewa na Rugemalira ni safi kabisa amepewa na kaka yake. Watanzania acheni wivu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom