Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Hivi karibuni waziri Bashe, ametoa kauli ya ajabu, kauli inayoashiria kukosa weledi na busara kama kiongozi.
Nasema amekosa weledi, kwa sababu mawazo yake yameishia pale alipokuwa amesimama bila ya kupima madhara yake kwasiku za mbeleni.
Kama Bashe angekuwa na hekima, kwanza angeomba taarifa kwa watoa msaada, ni virutubisho gani vimewekwa kwenye huo mchele, na ili vifanye nini kwa mlaji? Lakini pia, kama alikuwa bado na mashaka, angeweza kuchukua hata sampuli kadhaa na kuzipeleka kwenye maabara kadhaa kubwa za vyakula Duniani ili kujiridhisha.
Lakini maamuzi yake kuwa mchele huo utupwe, kudiplomasia, hiyo ni kupeleka ujumbe mzito kwa waliotoa, kuwa ni maadui zetu, wanaotaka kutuangamiza kupitia vyakula.
Nchi hii, chanjo zote za watoto tunapewa msaada. Madawa ya cancer ni msaada. Madawa ya kifua kikuu ni msaada. Madawa ya kupunguza makali ya ukimwi ni msaada. Hospitali ya Mlangazila pamoja na vifaa tiba vyake, ni msaada.
Kwa kauli na maamuzi ya Waziri Bashe, ni kuwa hivi vyote tusivitumie kwa sababu hatujui vina nini ndani yake.
Sasa, kama hao walioutoa huo msaada, walifanya hivyo kwa dhamira njema, na sisi tumewachukulia ni maadui wa Taifa letu, na wenyewe wakaona kuwa kwa vile imeonekana wao hawana dhamira njema na Tanzania, wakasema basi kuanzia sasa hawatatoa msaada wowote kwa Tanzania unaohusiana na vyakula au madawa kwa sababu vitu hivyo vyote vinaingia miilini mwetu, yeye Bashe atagharamia chanjo zote za nchi hii, labda kwa kupitia ule mradi wake wa ng'ombe kule Nzega?
Nchi hii tunapewa misaada mpaka ya kujengewa vyoo!! Ni lini tuliwahi kukataa misaada ya vitu vidogo vidogo kwa maelezo kuwa tuna uwezo wa kujitegemea?
Nchi hii mpaka kutunza mbuga zetu za wanyama, tunafanya kusaidiwa. Umeme umesambazwa vijijini, kwa 80% uligharamiwa na pesa ya MCC. Tangu wasimamishe pesa ya MCC, hiyo 20% iliyobakia inatutoa jasho!
Hivi sisi ni nini tuliweza chini ya CCM hata tukasimama mbele ya uso wa Dunia, tukatamba kufanikiwa. Tunashindwa hata kuendesha mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar. Kila siku ni hadithi. Umeme kila siku ni hadithi!!