Tungeamua Kutumia akili hata Kidogo...

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Hawa Ma PhD holders/ Ma Prof wangebakizwa Vyuoni. Wangelipwa vizuri huko na wangetumika kama wataalamu. Wangeweza kuandika mapendekezo mbalimbali ya kitaalamu na Serikali ikawa na utaratibu wa kuyatumia na yanapofanikiwa wanapewa malipo mazuri.

Wangeendelea kufundisha vijana na kuwalea wengine kitaaluma. Wangeanzisha clubs, taasisi na NGOs za kitaalamu kusaidia Wananchi ambao kodi yao pia ilitumika kuwasomesha.

Prof ana Degrees 9 alipwe pesa nzuri Elimu yake itumike kwa manufaa ya Umma. Ni wazi huyu ni mtu mwenye akili na uwezo mzuri. Ana uelewa wa mambo mengi. Siasa za nchi yetu zita mu undermine na kuharibu uwezo wake wa kufikiri.

Angalia Kabudi Prof aliyekuwa Chuo na huyu wa sasa. Angalia Dr. Bashiru yule wa Udsm PSPA na huyu wa sasa. Mwangalie Prof. Kitila Mkumbo yule wa Education na wasasa. Utalia sana kwa uchungu.
 
Shida inaanzia kwenye wabunge mishahara mikubwa na posho nene. Na Bado prof akishakuwa mbunge anauwinda Uwaziri na baada ya miaka mitano mafao ya wabunge yanatoka kabla hata bunge halijavunjwa.
 
Siasa ni kansa ambayo ikiingia sehemu inaharibu kila kitu.Hata pablo escobar aliharibu life lake la U DON baada ya kujiingiza kwenye siasa
 
Back
Top Bottom