Tundu Lisu Kuhusu Muungano

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
9,734
8,019
Watanganyika na zaidi wanachadema, Kwanini hamukubali uchambuzi na misimamo ya Viongozi wenu linapokuja suala la Muungano?
Tumsikilize Tundu Lisu Kidogo
===
Sauti inayofafana na Lissu inayoongea kwenye audio hii imezungumza yafuatayo.

Mgogoro wa Muungano ulipo ni kutokana na uhalali wa muungano, upande mmoja haujaridhika na muungano. Hawajaridhika kwa kuwa Tanaganyika haikupoteza mamlaka yake. Makubaliano ya muungano yalisema:
1. Katiba ya Jamhuri ya Tannganyika itakuwa ni katiba ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
2. Rais wa Tanganyika ndio atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanyika na Zanzibar
Vivyo hivyo kwa Nembo za taifa, mahakama kuu, serikali pia sehemu iliyotaja mali ya Tanganyika ilipaswa kujulikana kama ni mali ya muungano.

Wazanzibar wanaposema Tanganyika imejificha kwenye koti la Tanzania wako sahihi. Hivyo Tanganyika haijawahi kupoteza chochote zaidi ya Jina la Tanganyika, aidha tumeipata Zanzibar, ambayo tunaimulia nani awe Rais wao, wawe na mahusiano na nani, wakope wapi. Wameruhusiwa tu kuwa na Vikosi vya mapinduzi kwa kuwa Tanganyika imeviruhusu lakini mambo ya ulinzi na usalama ni ya muungano. Jeshi ni la Tanganyika, IGP na Mkuu wa Majeshi ni wa Tanganyika.

Rais hata kama akiwa Mzanzibar anakuwa ni rais wa Tanganyika. Huyu Rais Samia ni mzanzibar lakini ni rais wa Tanganyika, akienda Zanzibar anaenda kuwa Rais wa Muungano. Maana yake Tanganyika ina-extend nguvu zake Zanzibar. Attitude ya Tanganyika ni sawa na ya kikoloni tu, ndio maana watanganyika hawaoni shida. Wakoloni huwa hawaelewi malalamiko ya wakoloniwa.

Wakati wa ukoloni, wakoloni walikuwa hawaelewi kina Nyerere. Walikuwa wanaona wanalalamika tu, wakiona wanawalinda na kuwapa huduma nyingine. Akili hiyo ndio ipo kwa watanganyika ambao pia wanaona wanailisha na kuilinda Zanzibar, na kuwapelekea umeme bure, na kuona kama wanalalamika tu. Akili hii ni ya kikoloni kabisa.

Tanganyika ni mkoloni wa Zanzibar
Ukweli ni kwamba Tanganyika imekuwa mkoloni kwa Zanzibar kwa maana tumeichukua mamlaka muhimu ya Zanzibar tumeyachukua. Maamuzi yanaamuliwa Dar es Salaam au Dodoma. Mambo haya hayawezi kupelekwa mahakamani bali yanaamuliwa kisiasa na wananchi, au wakati mwingine huamuliwa vitani.
 

Attachments

  • Voice 001.m4a
    6.2 MB · Views: 8
Muungano unatakiwa uwe wa HAKI na kukubalika pande zote sio huu wa kuburuzana.
 
Back
Top Bottom