Mheshimiwa Tundu Lissu historia ya vita yako ya kutetea haki na utawala bora Tanzania imeandikwa kwa damu yako mwenyewe, na sina shaka hata kidogo wewe ni mpambanaji wa wapambanaji katika nchi yetu. Kati ya watu wachache wanaoweza kuelezea machungu ya kupigania haki na utawala bora duniani, basi wewe ni mhanga aliye hai na una kila moral authority ya kuelezea jinsi harakati hizo zilivyo ngumu na hatari!
Kwa bahari nzuri pia Mheshimiwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wako, naye ni mpambanaji mahiri na yeye pia anajua machungu ya kupambana na walio madarakani, amepitia hatari nyingi, kupoteza mali na fedha nyingi, kupigwa na kufungwa miezi mingi gerezani. Chadema tunajivunia kuwa na viongozi wanaoongoza kwa mifano ya maisha yao wakiwa tayari kumwaga damu zao kusimamia wanachokiamini. Hicho ni kipeo cha juu zaidi cha uongozi na hakuna ujasiri zaidi ya huo!
Mheshimiwa Tundu Lissu, endelea na mapambano lakini usiwe too radical najua hiyo ndio tabia yako ya ndani. Sikuambii haya ili kukutia maji, wala kukuogopesha, au kukuepusha na shari, la hasha, nakuambia haya kukukumbusha ukae kwenye mstari na wapambanaji wengine, ukiwaongoza kwa weledi na kadiri.
Don’t forget to be diplomatic and that you are more than an activist! Remember you are a politician and you should know how to play politics for the good of the people.
Tunahitaji Chadema imara yenye umoja na mshikamano! Maridhiano ya vyama vya siasa ndio msingi na mwanzo wa kurudi na kukua kwa demokrasia nchini mwetu. Taratibu yote yatakuwa sawa.
Siasa za mafanikio zina weledi wake. Usiwe mkali mno ukaogopwa hata na rafiki zako! Usiwe mtata mno ukashindwa kueleweka hata na wanachama na viongozi wenzako! Kuwa na kadiri katika misimamo yako, kaa katika mstari na wengine ukijua kuwa hisia za watu zinatofautiana, na pia upo wakati utapata nafasi ya kuongoza na utawajibika kuwasamehe hata wale waliofanya jaribio la kukatisha maisha yako!
Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa uliyopitia umeandika sio tu historia yako mwenyewe, bali historia ya Watanzania wote katika kudai haki na utawala bora. Nakutakia hekima, kadiri na uvumilivu katika harakati za ukombozi wa Taifa letu dhidi ya udhalimu, uzembe na ufisadi.