VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Najua hamtaniamini. Najua mpo mtakaobisha vya kutosha na kutisha. Mtapaniki kuliko pikipiki ya kutumia kiki. Lakini, nawaambia jambo hili. Ni jambo geni na kubwa lakini muhimu na linalowezekana kwenye siasa za sasa. Siasa za sasa zinahitaji amshaamsha.
Haifichiki tena kuwa mambo ndani ya CCM yetu si shwari. Hali si hali. Wanaohoji hadharani kuhusu uhalali wa uteuzi wa rais Samia kuwa mgombea wa Urais wa CCM wamefika wawili: Mch. Malisa wa Kilimanjaro na Polepole wa palepale.
Sirini, maelfu ya wana-CCM wanawaunga mkono hao. Ni uoga-wa-kawaida tu wa kitanzania unaowazuia kusema hadharani. Wanaogopa 'kushughulikiwa' kichama na kadhalika. Wanaogopa kujikuta wakiishi mafichoni kuliko porini na kusikojulikana kama maficho ya Havana.
Nami ni muoga wa hadharani kutokana na 'viapo' vyangu. Lakini, nami niko kwenye msimamo kuwa mchakato wa kumteua Mwenyekiti huku yeye akiongoza uteuzi huo haukuwa halali na ulikiuka Katiba ya CCM na ya Tanzania. Uteuzi wa wagombea vyamani huanza baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Ni msimamo wa kikatiba yenye tiba.
Rais na Mwenyekiti wangu ametingwa. Hata mkutano mkuu kuhamishiwa kwa mtandao usio na mtandio hakutasaidia kitu. Mkutano utakosa hamshahamsha na ufanisi. Wajumbe wataambiwa tu bila ya wao kusema. Wataagizwa bila kuumizwa lakini watalizwa. Misimamo itabaki ile ile.
Rais na Mwenyekiti wangu amebaki na Tundu Lissu kama turufu mujarabu yenye jawabu kwa yanayoendelea. Lissu anaungwa mkono ndani na nje ya CCM. Anaungwa mkono na ndani na nje ya nchi. Wengine wanatema nyongo zao kwakuwa tu Lissu yuko mahabusu na 'kuonekana' anateseka kule.
Lissu akiachiwa huru hata tarehe 29 Julai, macho na masikio yataelekezwa kwake na hivyo kupumua na kuamua kutapata utulivu. Lissu anapokelewa; ataongea; ataendelea na chama chake na siasa zitarudi kwenye barabara yake. Lissu atarejesha siasa siasani na maneno majukwaani.
Imebaki hii ya Lissu tu kurudi uraiani na siasani ili kufanyike siasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Gauteng, Afrika ya Kusini)