Tundu Lissu, tunafanyaje juu ya Prof. Kabudi?

Tundu Lissu, tunafanyaje juu ya Prof. Kabudi?

Professa kabudi ni changamoto mpya kwa upinzani, changamoto mpya kwenye bunge na siasa za ushindani wa hoja kwa ujumla. Sio changamoto ya kupuuzwa, ni changamoto ya kutafutia suluhu na suluhu ipo. Mh. Tundu Antipas Lissu

Mpaka sasa, Tundu Lissu ameitendea haki nafasi ya msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. Amejenga hoja zenye tija na ametoa miongozo muhimu sana katika kukijengea chama taswira ya heshima mbele ya jamii. Ila ujio wa profesa Kabudi unaleta shida kidogo....

Labda niseme, democrasia haiwezi kutambulika bila debate, yaani ushindani wa hoja. Profesa Kabudi hapaswi kuonekana anaoverwhelm upinzani. Ni kosa sana kimbinu kwa Lissu, kwasababu zozote zile kumuacha prof Kabudi atambe anavyota ndani ya bunge.

Kwenye siasa za ushindani wa hoja , mara zote debate ipo kazini. Mtu kama Kabudi anapoleta hoja unapaswa kumjibu. Kumuacha Kabudi afundishe bungeni kunaweza kuwa sawa japo ni kukubali kujitoa mapema kwenye siasa za ushindani wa hoja. Kumbuka siasa ni debate! Actually, kinachofanyika bungeni ni parliamentary debate .

Mimi najua Lissu ni mjengaji mzuri wa hoja japo naomba nimuongezee machache kwenye hii changamoto mpya ya ujio wa prof Kabudi.

1. Listen; watu wanaweza kunishangaa sana napokuomba usikilize. Na hii ni kwasababu wanajua huwaga unasikiliza. Ila kumshinda prof Kabudi kwa hoja unahitaji kumsikiliza kwa makini sana. In all his arguments, somewhere he will expose himself. Hii ni kawaida sana.
Kwa hao wana CCM wengine waliokuwa bungeni ilitosha tu kuwasikiliza kwa rasharasha na kusubiria wakati wako wa kujenga hoja.
Kwa kabudi mapungufu hayatakuwa mengi kiivyo, so you have to go for the details because everything he says, he has to be accountable for it.

2. Practice debate judo. Philosophia ya judo ni nzuri sana kama ukiitumia kwenye ushindani wa hoja. Kwenye judo kama mtu akikutupia pigo basi haumjibu hapo kwa papo. Ila unaongezea nguvu kidogo kwenye muelekeo wa nguvu zake ili kumuangusha.
Mfano; unaweza kukubaliana na hoja zake nyingi ila ukaja na hoja moja na kusema hudhani kama inaleta maana sana kisha hapo unaanza kujenga hoja zako.

Sisi wapenzi wa siasa za ushindani wa hoja tunafuatilia mtanange kati yako mheshimiwa Lissu na prof Kabudi kwa hisia kubwa sana. Tunaamini kama kawaida wapinzani tutashinda kwa hoja. Tutoe kimasomaso mheshimiwa Lissu.

BringBackBen
Kwenye midahalo bila kujali mada ilitayarishwa (prompt) au haikuandaliwa (impromptu) kuna suala la kukubaliana na hoja (crossing the floor).
Sio kila wakati lazima upinge kila mjadala hata kama una hoja dhaifu! Ni sawa na masumbwi. Mwalimu akiona mpiganaji wangu ataumizwa zaidi, hutupa taulo ulingoni. Unachojaribu kumwambia Lissu ni kwamba ajikaze kiume
Mimi nakushauri ujaribu kuwa mfuatiliaji wa Prof. Kabudi ili ikiwezekana uwe unamusaidia Lissu kujenga hoja. Inaweza ikafaa.
Jaribuni!
 
Sasa kama ni hivyo mangi mbona hata sisi tuliomsafisha Lowassa na kumpa fomu ya urais ndani ya saa 24 baada ya kumtaja fisadi kuu miaka 8 mbona tukiulizwa tunakuwa wakali kama Gwajima amenyimwa sadaka
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] nimefuatilia majibizano yako na huyo Mangi,ila hii imenichekesha sana,,nilitaka nione mwisho wake ila nimeishia hapa kucheka maana umeweka hoja ambayo sidhani kama atajibu zaidi tu ya kuwa mkali,ila kura nilimpa huyo fisadi
 
Alikopotelea polepole na kabudi anaenda huko huko hakuna mtu mwenye akili timamu aliyekwenda kutetea chama dola akabaki na akili zake za kawaida, hiyo ya juzi ni kwa sababu ya ugeni kwenye kazi atakapokuwa mwenyeji huyo utamshangaa kama vile mwakye
Haa mwakye na liunga lililokuwa linamtoka uson wakampa uwaziri sijui aliwadanganya kuwa amegundua mafuta mapya na ile sula akasema yuko kwenye utafiti wa hayo mafuta
 
Kabudi kutetea kuwa honorary degrees zinaheshimiwa sana je huko ni kujustfy kupewa kwake uwakili wa heshima baada ya kufeli mitihani ya uwakili?
 
Massanda Omtima
Kila argument ni debatable kasoro tu zile undesoutable facts. Mtu akikwambia Mkoa wa dodoma uko Tanzania hiyo ni fact, hapo hakuna debate.

Ila the rest are debatable .
Unahitaji tu kuwa umefanya research ya kutosha kwenye jambo & uwe articulate. Ukiwa na convincing power ya kumfanya third neutral party akubaliane na mtazamo wako basi tena, ndio ushindi huo
 
Naona darasa la dakika 29:18 limekuingia kisawasawa maana ulidhan lissu ataomba muongozo lakina ukashangaa nae anapiga meza,,ni hiv ukiwaza kushoto wengine wanawaza kulia so subiri ndio kwanza kabud kaanza baadae utamwamkia shikomooo
Si kweli unayosema... Kwa taarifa yako wote walikuja kwa moto kama huo ila unakuja kuzima gafla kama mabua.... Ni ngumu kutetea uongo kuwa kweli siku zote; utaanza leo na kesho ila kuanzia keshokutwa na kuendelea you'r finished.
Refer Prof. Muhongo where is he.. Ukimwita kwenye hoja anakuja kama kuku aliyenyeshewa maji
 
Naona darasa la dakika 29:18 limekuingia kisawasawa maana ulidhan lissu ataomba muongozo lakina ukashangaa nae anapiga meza,,ni hiv ukiwaza kushoto wengine wanawaza kulia so subiri ndio kwanza kabud kaanza baadae utamwamkia shikomooo
Hahahahaha mkuu darasa gani pale kakimbia hoja nzito kabisa kuhusu thesis yake!!! Alikuwa anatokwa povu kuhusu katiba mpya leo hii anaogopa hata kuiongelea??? Afu mnasema katoa darasa?? Mtego wake ni huo tu akishindwa kuyaishi maneno yake yaliyompa phD ya katiba mpya na serikali tatu basi atafeli kma mwakyembe na polepole!!!!
 
2. Practice debate judo...nimeipenda
 
Wazir yyte anaepewa dk 30 za kuongea lazima apewe glass za maji na alikunywa mara 3. Unaweza kuona ana ana majigambo lakin jiulize alijigamba nn pale
Mara nyingine ukimuona mtu anakunywa maji ambayo labda ni mengi kuliko kawaida ya unywaji mahaki ambapo kuna AC, ujue ana stomach butterflies au yuko na tension fulani na yawezekana sababu hajaizoea hadhira ile.

Itoshe tu kusema kuwa Kabudi ni mgeni sana serikalini na kwenye siasa za bungeni na akishirikisha halmashauri ya kichwa chake vizuri ataacha kuzungumza bubgeni kana kwamba yuko kwenye lecture hall. Anyway, by and by atajifunza kutofautisha.
 
Alikopotelea polepole na kabudi anaenda huko huko hakuna mtu mwenye akili timamu aliyekwenda kutetea chama dola akabaki na akili zake za kawaida, hiyo ya juzi ni kwa sababu ya ugeni kwenye kazi atakapokuwa mwenyeji huyo utamshangaa kama vile mwakye
Kwa hivyo Chadema ikija kuwa chama dola, watakao kuwa huku watakuwa hawana Akili Timamu.
 
  • Kwa kujenga hoja Tindu Lissu na upinzani kwa ujumla hawatoboi kwa Prof. Kabudi
  • Labda walete vurugu kama walizokuwa wakiwafanyia Prof. Muhongo na Tibaijuka enzi zile za bunge la awamu ya Jakaya Kiwete
Mmesahau kuwa mlisema hivyo hivyo kwa Tulia na kwa maneno yenu ya leo inaonyesha kachemsha na sasa mnalotumaini kwa huyo Kabudi. Lisu anamsoma tu Kabudi, ngoja aje. Kama kubadilisha mawaziri wa sheria vile ni kutafuta wa kushindana na Lisu basi tayari keshawashinda serikali nzima.
Mungu wetu tunayekuabudu simama upande wa wenye haki - iwe wao au wanyonge.
 
Kwa hivyo Chadema ikija kuwa chama dola, watakao kuwa huku watakuwa hawana Akili Timamu.
Chama dola ni ccm, vyama vingine vya upinzani nchini hakuna chenye mlengo wa kuwa chama dola, kwa sababu lengo lao ni kuongoza nchi kwa kushirikisha wananchi na ndio maana wapinzani wote wanazungumzia mabadiliko makubwa ya katiba ili serikali iwe shirikishi tofauti na sasa hivi ambapo chama kilichopo madarakani hakipokei maoni toka nje ya mfumo wao katika kuongoza nchi bila kujali kama maoni hayo ni mazuri kiasi gani, nimeona ni vyema nikufafanulie suala la chama dola
 
Back
Top Bottom