Tundu Lissu, tunafanyaje juu ya Prof. Kabudi?

Tundu Lissu, tunafanyaje juu ya Prof. Kabudi?

Maprofesa wa Tanzania hugeuka kuwa Mapropesa wa watawala pale tu wanapoanza kutumikishwa na watawala kisiasa,yote hii ni kwa sababu nchi inatumikia siasa,inasimamia siasa na kulinda chama tawala baadala ya maslahi ya nchi na hatima ya vizazi vijavyo.

Prof. Issa Shivji si yupo rasmi CCM siku hizi? Hata kutoa maoni siku hizi anaogopa.

Kufupisha mjadala sample awekwe Lipumba!!

Kabudi hana hata mwaka,atakula alivyovimanga kwenye katiba!!
 
Lilikuwa darasa bali matambo ya irrelevance issues na matamko ya maneno ya kisheria, Hakika Prof Kabudi Alichemka Sana na pressure ilimpanda kiasi cha kunywa glass Saba za maji
Wazir yyte anaepewa dk 30 za kuongea lazima apewe glass za maji na alikunywa mara 3. Unaweza kuona ana ana majigambo lakin jiulize alijigamba nn pale
 
Professa kabudi ni changamoto mpya kwa upinzani, changamoto mpya kwenye bunge na siasa za ushindani wa hoja kwa ujumla. Sio changamoto ya kupuuzwa, ni changamoto ya kutafutia suluhu na suluhu ipo. Mh. Tundu Antipas Lissu

Mpaka sasa, Tundu Lissu ameitendea haki nafasi ya msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. Amejenga hoja zenye tija na ametoa miongozo muhimu sana katika kukijengea chama taswira ya heshima mbele ya jamii. Ila ujio wa profesa Kabudi unaleta shida kidogo....

Labda niseme, democrasia haiwezi kutambulika bila debate, yaani ushindani wa hoja. Profesa Kabudi hapaswi kuonekana anaoverwhelm upinzani. Ni kosa sana kimbinu kwa Lissu, kwasababu zozote zile kumuacha prof Kabudi atambe anavyota ndani ya bunge.

Kwenye siasa za ushindani wa hoja , mara zote debate ipo kazini. Mtu kama Kabudi anapoleta hoja unapaswa kumjibu. Kumuacha Kabudi afundishe bungeni kunaweza kuwa sawa japo ni kukubali kujitoa mapema kwenye siasa za ushindani wa hoja. Kumbuka siasa ni debate! Actually, kinachofanyika bungeni ni parliamentary debate .

Mimi najua Lissu ni mjengaji mzuri wa hoja japo naomba nimuongezee machache kwenye hii changamoto mpya ya ujio wa prof Kabudi.

1. Listen; watu wanaweza kunishangaa sana napokuomba usikilize. Na hii ni kwasababu wanajua huwaga unasikiliza. Ila kumshinda prof Kabudi kwa hoja unahitaji kumsikiliza kwa makini sana. In all his arguments, somewhere he will expose himself. Hii ni kawaida sana.
Kwa hao wana CCM wengine waliokuwa bungeni ilitosha tu kuwasikiliza kwa rasharasha na kusubiria wakati wako wa kujenga hoja.
Kwa kabudi mapungufu hayatakuwa mengi kiivyo, so you have to go for the details because everything he says, he has to be accountable for it.

2. Practice debate judo. Philosophia ya judo ni nzuri sana kama ukiitumia kwenye ushindani wa hoja. Kwenye judo kama mtu akikutupia pigo basi haumjibu hapo kwa papo. Ila unaongezea nguvu kidogo kwenye muelekeo wa nguvu zake ili kumuangusha.
Mfano; unaweza kukubaliana na hoja zake nyingi ila ukaja na hoja moja na kusema hudhani kama inaleta maana sana kisha hapo unaanza kujenga hoja zako.

Sisi wapenzi wa siasa za ushindani wa hoja tunafuatilia mtanange kati yako mheshimiwa Lissu na prof Kabudi kwa hisia kubwa sana. Tunaamini kama kawaida wapinzani tutashinda kwa hoja. Tutoe kimasomaso mheshimiwa Lissu.

BringBackBen

Tundu Lissu anachoweza ni makelele tu, huwa sioni kama ni mjengaji mzuri wa hoja. Kwa upinzani, wabunge wanaojua kujenga hoja ni Mnyika na Zitto. Hawa wengine sioni. Msigwa yeye anajua kutoa quotes ambazo kimsingi yeye hazitumii katika maisha yake. Tunapokuja kwa issue ya Prof. Kabudi, nadhani Lissu atapwaya sana. Msingi wa makelele ya Lissu ilikuwa kuibua mambo ya kihistoria katika sheria, mfano issue ya hati za muungano n.k. Na hiyo alikuwa akiifanya kwa kusoma sana. Sasa Prof. Kabudi alikuwa mwalimu na amesoma sana mambo hayo. Kwa kifupi yapo kichwani. Sasa sidhani kama Lissu ataweza kujenga hoja ambayo Prof. Kabudi atakuwa haijui.
 
Polisi,wasomi,maafisa mipango,washauri wa viongozi ndo majipu yanayokwamisha maendeleo
 
Kabudi nguvu ya soda vijana wapo room wanapasha subiria moto wake
 
Uprofessor ni nje ya CCM, ukishaingia milango ya Lumumba unaacha elimu yako mlangoni, huko inakwenda kuungana na akili za kina Bashite, yule jamaa wa ulanga, Kibajaji na yule Dada kwenye CV tata na ndoa lukuki..........hizo ndio akili akili za Lumumba.
 
Tundu Lissu anachoweza ni makelele tu, huwa sioni kama ni mjengaji mzuri wa hoja. Kwa upinzani, wabunge wanaojua kujenga hoja ni Mnyika na Zitto. Hawa wengine sioni. Msigwa yeye anajua kutoa quotes ambazo kimsingi yeye hazitumii katika maisha yake. Tunapokuja kwa issue ya Prof. Kabudi, nadhani Lissu atapwaya sana. Msingi wa makelele ya Lissu ilikuwa kuibua mambo ya kihistoria katika sheria, mfano issue ya hati za muungano n.k. Na hiyo alikuwa akiifanya kwa kusoma sana. Sasa Prof. Kabudi alikuwa mwalimu na amesoma sana mambo hayo. Kwa kifupi yapo kichwani. Sasa sidhani kama Lissu ataweza kujenga hoja ambayo Prof. Kabudi atakuwa haijui.
  • Comment yako ni nzuri sana hasa haya maandishi
"Msingi wa makelele ya Lissu ilikuwa kuibua mambo ya kihistoria katika sheria, mfano issue ya hati za muungano n.k. Na hiyo alikuwa akiifanya kwa kusoma sana. Sasa Prof. Kabudi alikuwa mwalimu na amesoma sana mambo hayo. Kwa kifupi yapo kichwani. Sasa sidhani kama Lissu ataweza kujenga hoja ambayo Prof. Kabudi atakuwa haijui."
  • Hongera sana mkuu kwa hoja yenye mashiko
 
Naona darasa la dakika 29:18 limekuingia kisawasawa maana ulidhan lissu ataomba muongozo lakina ukashangaa nae anapiga meza,,ni hiv ukiwaza kushoto wengine wanawaza kulia so subiri ndio kwanza kabud kaanza baadae utamwamkia shikomooo
Sio tu atamwamkia bali atakwenda kwa hiari yake kuomba viatu akaoshe
 
Kitakachomwangusha Kabudi ni mipango ya ccm , atalazimika kuchukua maagizo ya chama badala ya werevu wake , na kwa vile atakuwa kabebeshwa mambo ya hovyo atashindwa kuyatetea , hapo ndio atakapomalizwa .

Lengo la ccm ni kudhalilisha hawa wasomi wa nchi hii .
 
  • Msingi wa makelele ya Lissu ilikuwa kuibua mambo ya kihistoria katika sheria, mfano issue ya hati za muungano n.k. Na hiyo alikuwa akiifanya kwa kusoma sana (Noah FELIX, 2017).
  • Kwa mara nyingine; Comment yako hiyo ni balaa, Mods hebu pandisheni comment ya huyu Noah FELIX ikawe ya kwanza baada ya thread
  • Pia hizo historia za baadhi ya nyakati ambazo Tundu Lissu amekuwa akipotosha potosha Prof. Kabudi alikuwapo, tena Prof. Kabudi alikuwa mtu mzima ukimlinganisha na Tundu Lissu
 
Siku wakiwa vinyonga kama hawa wanaovalishwa gamba la kijani hawataaminika! Hebu ona huyu kabudi muumini na mwandishi wa katiba ya warioba-atakapoanza kupinga kile alichoandika na kukiamini na kukipigia debe ana haki ya kuaminiwa hata hoja kutoka kuzimuni? Kama lile gumashi lililopelekwa kwenye ile wizara ya usanii lilivyopinga thesis ya lenyewe kuhusu serikali tatu?
Kwa kweli maprofesa wetu.wanahitaji maombi.
 
Suala siyo kukubaliana na sisi au na wengine! suala ni msimamo (consistency). Hivi mtu umetumia miaka 6 kusomea PHD na umeandika thesis baada ya uchambuzi wa kutosha leo hii upewe tonge la kijani ukatae yote!! Hizi njaa kwenye marlboro zitatumaliza!! Huyu Kabudi ameandika ile katiba kwa vidole vyake na ametumia muda kufanya uchambuzi wa maoni yetu na maandiko mbali mbali duniani kote hivi Tonge la kijani linatosha kusaliti kazi yake mwenyewe?
Atafanyaje? Akikumbuka yaliyomkuta Mvungi......
 
Naomba clip ya darasa la Prof Kabudi mjengoni, tafadhali
 
Lisu anaeleweka na Nyumbu tu. aminivusiamini kama Lisu ataongea kwa dakika10 na wewe msikilizaji unatumia dakika kadhaa kutafakari alicho ongea utajua Lisu hamnakitu, Nimajigambo na Povu jiingi ilahamna kitu.

Kabudi atambadilisha Lisu, asiongee uongo.Kitukitakacho mfanya Leo isu awe wakawaida sana. Maana amezoea uongo.
Kabudi yupo vizurisana atakua akimsahihisha kila lisu anapo ongopa.
Lisu aliniachahoi aliposema hakuna hatiya muungano. Uku mapovu yakimtoka, na kunabaadhi ya watu waliamini hivyo, Serikali ikamwacha atoe povu la kutosha. Baadae serikali ikaleta ile hati ya Muungano, Akadai eti zile saini zilizopo kwenye hati siza Mwalimu Nyerere na Karume.[emoji3][emoji3] Pale ndipo nilipo thibitisha Lisu hazimtoshi.
 
Naunga mkono hoja kwamba hoja zote za prof. Kabudi azipangue Lissu. Lissu una kazi ya kusoma maandiko mengi ya Kabudi ili umbane kwenye kona ya maneno yake.
 
Back
Top Bottom