Tundu Lissu, tunafanyaje juu ya Prof. Kabudi?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Professa kabudi ni changamoto mpya kwa upinzani, changamoto mpya kwenye bunge na siasa za ushindani wa hoja kwa ujumla. Sio changamoto ya kupuuzwa, ni changamoto ya kutafutia suluhu na suluhu ipo. Mh. Tundu Antipas Lissu

Mpaka sasa, Tundu Lissu ameitendea haki nafasi ya msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. Amejenga hoja zenye tija na ametoa miongozo muhimu sana katika kukijengea chama taswira ya heshima mbele ya jamii. Ila ujio wa profesa Kabudi unaleta shida kidogo....

Labda niseme, democrasia haiwezi kutambulika bila debate, yaani ushindani wa hoja. Profesa Kabudi hapaswi kuonekana anaoverwhelm upinzani. Ni kosa sana kimbinu kwa Lissu, kwasababu zozote zile kumuacha prof Kabudi atambe anavyota ndani ya bunge.

Kwenye siasa za ushindani wa hoja , mara zote debate ipo kazini. Mtu kama Kabudi anapoleta hoja unapaswa kumjibu. Kumuacha Kabudi afundishe bungeni kunaweza kuwa sawa japo ni kukubali kujitoa mapema kwenye siasa za ushindani wa hoja. Kumbuka siasa ni debate! Actually, kinachofanyika bungeni ni parliamentary debate .

Mimi najua Lissu ni mjengaji mzuri wa hoja japo naomba nimuongezee machache kwenye hii changamoto mpya ya ujio wa prof Kabudi.

1. Listen; watu wanaweza kunishangaa sana napokuomba usikilize. Na hii ni kwasababu wanajua huwaga unasikiliza. Ila kumshinda prof Kabudi kwa hoja unahitaji kumsikiliza kwa makini sana. In all his arguments, somewhere he will expose himself. Hii ni kawaida sana.
Kwa hao wana CCM wengine waliokuwa bungeni ilitosha tu kuwasikiliza kwa rasharasha na kusubiria wakati wako wa kujenga hoja.
Kwa kabudi mapungufu hayatakuwa mengi kiivyo, so you have to go for the details because everything he says, he has to be accountable for it.

2. Practice debate judo. Philosophia ya judo ni nzuri sana kama ukiitumia kwenye ushindani wa hoja. Kwenye judo kama mtu akikutupia pigo basi haumjibu hapo kwa papo. Ila unaongezea nguvu kidogo kwenye muelekeo wa nguvu zake ili kumuangusha.
Mfano; unaweza kukubaliana na hoja zake nyingi ila ukaja na hoja moja na kusema hudhani kama inaleta maana sana kisha hapo unaanza kujenga hoja zako.

Sisi wapenzi wa siasa za ushindani wa hoja tunafuatilia mtanange kati yako mheshimiwa Lissu na prof Kabudi kwa hisia kubwa sana. Tunaamini kama kawaida wapinzani tutashinda kwa hoja. Tutoe kimasomaso mheshimiwa Lissu.

BringBackBen
 
Ndio mangi, kwani wewe huwaamimini PROF BAREGU na PROF SAFARI ?
Siku wakiwa vinyonga kama hawa wanaovalishwa gamba la kijani hawataaminika! Hebu ona huyu kabudi muumini na mwandishi wa katiba ya warioba-atakapoanza kupinga kile alichoandika na kukiamini na kukipigia debe ana haki ya kuaminiwa hata hoja kutoka kuzimuni? Kama lile gumashi lililopelekwa kwenye ile wizara ya usanii lilivyopinga thesis ya lenyewe kuhusu serikali tatu?
 
Kabudi tayali yupo ndani ya Serikali hivyo perfomance yake usidhani itakuwa kama alivyokuwa nje ya Serikali.

Rejea ya Akina Ayubu Rioba naye tulimsifia sana lakini sasa tunaona.

Subiri sasa na yeye aizoee Serikali.
 
Siku wakiwa vinyonga kama hawa wanaovalishwa gamba la kijani hawataaminika! Hebu ona huyu kabudi muumini na mwandishi wa katiba ya warioba-atakapoanza kupinga kile alichoandika na kukiamini na kukipigia debe ana haki ya kuaminiwa hata hoja kutoka kuzimuni? Kama lile gumashi lililopelekwa kwenye ile wizara ya usanii lilivyopinga thesis ya lenyewe kuhusu serikali tatu?
Sasa mangi kwani ili uwe PROF lazima akubaliane na sisi kimtizamo ?
 
Naona darasa la dakika 29:18 limekuingia kisawasawa maana ulidhan lissu ataomba muongozo lakina ukashangaa nae anapiga meza,,ni hiv ukiwaza kushoto wengine wanawaza kulia so subiri ndio kwanza kabud kaanza baadae utamwamkia shikomooo
Ni kwa vile bado mgeni ndani ya serikali, mpaka kufikia vikao vya bunge vya mwezi Novemba mtajua kwamba kuna tatizo kubwa ndani ya mfumo wa serikali ya Tanzania inayoongozwa na ccm, mtakosa lugha ya kumtetea hapa
 
Sasa mangi kwani ili uwe PROF lazima akubaliane na sisi kimtizamo ?
Suala siyo kukubaliana na sisi au na wengine! suala ni msimamo (consistency). Hivi mtu umetumia miaka 6 kusomea PHD na umeandika thesis baada ya uchambuzi wa kutosha leo hii upewe tonge la kijani ukatae yote!! Hizi njaa kwenye marlboro zitatumaliza!! Huyu Kabudi ameandika ile katiba kwa vidole vyake na ametumia muda kufanya uchambuzi wa maoni yetu na maandiko mbali mbali duniani kote hivi Tonge la kijani linatosha kusaliti kazi yake mwenyewe?
 
Mtu kama Kabudi anapoleta hoja unapaswa kumjibu. Kumuacha Kabudi afundishe bungeni kunaweza kuwa sawa japo ni kukubali kujitoa mapema kwenye siasa za ushindani wa hoja.

Lissu aliongea 30 minutes bila kuwa interrupted. Zamu ya Waziri kujibu hoja za msemaji wa upinzani ni muda wa Kabudi. Lissu hawezi kumu interupt ovyo ovyo out of turn, ataonekana chizi.

Halafu Kabudi kakutisha wewe tu na wanafunzi mediocre wa sheria. Watu wazima wamemuona ni academician ambae mkusanyiko wowote mbele yake yeye anadhani ni darasa, na hana busara wala haongei sense yeyote.

Kabudi kajidai statesman wa kulinasihi bunge liache kutukanana. Eti kawaambia usitumie neno stupid bali mwambie mtu upeo wako unapungua.

Can you imagine a true statesman kama Ally Hassan Mwinyi au Joseph Sinde Warioba waseme "wabunge tafuteni mbadala wa neno stupid lenye maana hiyo hiyo stupid" !

Halafu unanambia huyu ni genius wa sheria kwenye historia ya UDSM? Genius wa sheria gani kama wanasheria wenzio wote wanajua wewe hujapasi mtihani ambao mawakili wote nchi nzima wameufanya?
 
Hivi prof. Muhongo aliishia wapi... Labda tuanzie hapa... Kabudi ni mdogo sana
 
Suala siyo kukubaliana na sisi au na wengine! suala ni msimamo (consistency). Hivi mtu umetumia miaka 6 kusomea PHD na umeandika thesis baada ya uchambuzi wa kutosha leo hii upewe tonge la kijani ukatae yote!! Hizi njaa kwenye marlboro zitatumaliza!! Huyu Kabudi ameandika ile katiba kwa vidole vyake na ametumia muda kufanya uchambuzi wa maoni yetu na maandiko mbali mbali duniani kote hivi Tonge la kijani linatosha kusaliti kazi yake mwenyewe?
Sasa kama ni hivyo mangi mbona hata sisi tuliomsafisha Lowassa na kumpa fomu ya urais ndani ya saa 24 baada ya kumtaja fisadi kuu miaka 8 mbona tukiulizwa tunakuwa wakali kama Gwajima amenyimwa sadaka
 
Naona darasa la dakika 29:18 limekuingia kisawasawa maana ulidhan lissu ataomba muongozo lakina ukashangaa nae anapiga meza,,ni hiv ukiwaza kushoto wengine wanawaza kulia so subiri ndio kwanza kabud kaanza baadae utamwamkia shikomooo
Lilikuwa darasa bali matambo ya irrelevance issues na matamko ya maneno ya kisheria, Hakika Prof Kabudi Alichemka Sana na pressure ilimpanda kiasi cha kunywa glass Saba za maji
 
Sasa kama ni hivyo mangi mbona hata sisi tuliomsafisha Lowassa na kumpa fomu ya urais ndani ya saa 24 baada ya kumtaja fisadi kuu miaka 8 mbona tukiulizwa tunakuwa wakali kama Gwajima amenyimwa sadaka
Inconsistency!! continues
 
Back
Top Bottom