Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,260
1.Tundu Lissu
Majimbo ya uchaguzi yagawanywe kulingana na idadi ya watu, sio jiografia au matakwa na maslahi binafsi tu ya watawala kama ilivyo sasa. Mkoa wa mtwara wenye wapiga kura laki tisa una majimbo 10 ya uchaguzi sawa na mkoa wa Dar es Salaam wenye wapiga kura million tano na nusu nao una majimbo 10 tu ya uchaguzi huku Zanzibar yenye wapiga kura laki tano ina majimbo 50 ya uchaguzi!
2.Fatma Karume
Tume ya uchaguzi haina mamlaka ya kuwaondoa watu kiholela na kinyamelea kwa sababu ya kukosea tu kujaza fomu za uchaguzi au kutoweka nukta mwisho wa sentensi. Pia tume ya uchaguzi isitumike kufanya mambo ya hovyo kama watumishi wake kujificha ile kutopokea fomu za wagombea wa upinzani. Hata majaji wa mahakama huwa wanakosea kuliita na kuandika jina lake, fatuma badala ya fatma!
3.Ananilea Nkya
Viti maalumu vya ubunge havina faida yoyote kwa sababu wabunge wa viti maalumu hawawajibiki wa jimbo lolote. Kwa miaka mitano wabunge 113 wa viti maalumu wanalipwa billion 200 ambazo zinaweza kulipia bima ya afya kwa watoto wote wa nchi kwa kipindi hicho.