Tundu Lissu rudi Shule

Tundu Lissu rudi Shule

sikupenda kuchangia mada hii kwa kuwa inaonekana na ya kihiyo wa sheria au kama ulivosema mwanafunzi wa sheria wa semister ya kwanza ya law certificate.

Mwanasheria eti hajui kuwa sheria ya vyama vya siasa chini ya msajili imekubali kusajiliwa katiba ya chadema ambayo mwenye mada anaisema ni void ab initio. Sasa kama sheria ya vyama vya siasa imeruhusu huo mwanya wa katiba kutungwa, kwa iyo Sheria ya vyama vya siasa ya1992 ni void? Je nani anaamuru kuwa sheria iyo ni void? Ni subject of it or the court of Law? na kama ni court - inasubiri nini?

mwanasheria hajui kuwa zipo sheria za vikundi au hata nchi zinazokataa kwenda mahakamani, ipo sheria ya magazeti, sheria za TFF, cdm, nk nk.( Ouster of jurisdiction) japo bound by (courts inherent powers) Hizi hazimnyimi mtu haki yake bali zinamtaka kwanza kufuata utaratibu waliojiwekea kabla ya kuiona chombo cha haki/mahakama,au hata kuheshimu maamuzi ayo ya vyombo au taasisi husika....PIA: Ningemshauri tu akifika semester ya kwanza ya digrii ya sheria asikimbie Law of Contract, kwa kuwa aya yaliyotokea yana contractual features/yaani kujiunga kwa kwenye chama ni kukubaliana na msharti ya chama, Sheria ya mikataba inatoa mwanya wa watu kukubaliana kutokwenda mahakamani endapo mkataba umekwama, ukisaini umekubali, ukikataa kwa hiari umekataa!


Mwanasheria anadai Lissu arudi darasani sijui kusoma tafsiri ya mahakama kumkatalia ombi lake, hajui kuwa ukienda mahakamani kuomba zuio/injuction , zuio likikataliwa ina maana makubaliano yenu ya awali kabla ya zuio yanaedelea as if no injuction was sought. Kwa maana hiyo, kama chama walishaazimia kumfukuza mwanachama, wanamfukuza then yeye akikimbia kuomba zuio likafeli, then maamuzi ya chama yanabaki pale pale, zuio likikubaliwa basi maamuzi ya chama hupoteza nguvu!! Zuio limefeli maamuzi ya chama yamekubaliwa....actually failure of injuction should cement that the court reaffirms the already taken steps/awards.
Mleta mada hapa unalaumu mwakilishi wa chama kwa kukumbushi maamuzi ya kamati kuu kabla ya zuio la mfukuzwa, au unalaumu mahakama kwa kukataa kutoa amri ya zuio la ayo maamuzi? Sipendi unipe jibu.

Mwanasheria anahoji mamlaka ya mwakilishi wa chama, anataka yatolewe na superior authority? ...Ukifika hatua ya mbele utafundishwa Administrative Law, ....iyo itakufundisha vitu kama Delegation authority, ...huwezi kuwapangia chama nani atoe tamko, wao na kwa wakati wao na kwa utaratibu wao uliokubaliwa na vikao vyao halali na kupitishwa na wengi wanajua nani akisemee chama. Pia atafundishwa kuwa ukishakuwa mwanasheria mkuu wa taasisi au jumuiya flani unapewa mamlaka za kisheria kutokana na kazi yako, aidha expressly au impliedly...pia ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa idara ya sheria katika taasisi ndiye anayeelekeza maamuzi yoooote ya kisheria ndani ya iyo taasisi, hawezi kumwachia mwenyekiti au mtunza hazina kutoa maelekezo ya kisheria katika suala husika, endapo utaratibu uliowekwa hauruhusu mkurugenzi kuja directly basi utakuwa umeeelekeza mkurugenzi uyo aripoti na kushauri kwa nani, je utaratibu na organization chart ya chadema ikoje??...pia sio lazima maelezo ya mkurugenzi au wakili kwenye tafsiri za kisheria yasubiri aliyemtuma/ anaweza kusema ila atakutana na mwajiri wake kwenye 'kwa nini unisemee'? nayo sio kwenye ishu za kisheria ....mfano wakili akitoka kwenye maamuzi na vyombo vya habari vikataka kumuhoji mambo ya kisheria, ni kihiyo pekee anaweza kusema ngoja nikamwombe mteja ruhusa- kwa mambo ambayo ni tafsiri za kisheria wala si siri za mteja [ni kwa asiyejielewa pekee]


Anamshauri aliyekataliwa zuio kwenda kuappeal kuomba tafsiri ya kisheria ...ni mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza anaweza kushauri ivo. Eti mtu aombe injuction/ mahakama ikatae,...kwa kukataa mahakama inakuwa imebariki maamuzi ya awali, sasa aliyenyimwa zuio akaappeal kuomba tafsiri ya sheria. Mbele ya mahakama lililetwa ombi la zuio, zuio limefeli then ubebe content nje ya document ya ombi then ukaappeal???
Je unaappeal kukataa kukataliwa zuio au unaappeal kuhusu mahamuzi ya chama na apo kumbuka hakuna maamuzi ya chama yaliyoshtakiwa bali alienda mahakamani kukataa kutolewa maamuzi na chama, je akaappeal kukataa zuio au maamuzi ya chama? Kama ni agaist maamuzi ya chama then anapasw kuappeal kwenye ngazi ya juu kwenye chama,...kama anaappeal against kukataliwa zuio basi atakuwa anaappeal kukataa kukosa zuio. Itakuwa ni Court V. Mlalamikaji , Content iwe : KUHUSU KUNYIMWA ZUIO
Je hicho kitu kipo kwenye sheria ??


Mtetezi anakataza doing an evil to justify other evil ila bado analeta kesi ya Ngeleja kwenye content ya zuio la mlalamikaji akihusisha lisu, the the emphasis of a wrong reverts to right?? Kama unalalamika kuhusu Lissu inakuwaje ulalamikie lissu compared to Ngeleja, treat different cases differently!!



kama haya yanajulikana kwa sisi watu wa kawaida, je mleta mada, mwanasheria nguli huyajui aya???Ni fedhea wala siwezi kubishana na mleta mada.[/QUOTE

Hapo umemsomesha huyo mwanafunzi wa sheria. Mkumbushe pia kuwa sheria ya uchaguzi inazuia mgombea wa urais aliyeshindwa kwenda mahakamani kuhoji matokeo. Hii haivunji katiba?
 
Aisee wewe ni msomi wa sheria mzuri hata kwa maandishi tu inatosha Ku justify,Tindu Lissu ametumwa aje aiue chadema narudia tena pili ni mgonjwa upstairs
 
Hiyo ndiyo katiba ya CHADEMA na ndiyo imeshasajiliwa kwa msajili wa vyama vya siasa nchini...una lingine?
Kama huna lingine vizuri, haya nenda kasome katiba/sheria ya FIFA

Katiba ya CDM Leo hii ya kuifananisha na FIFA?
 
lissu mroho wa madaraka anaka yeye awe naibu katibu mkuu
 
Umaarufu wa zitto mwanzo ulitokana na kupinga ufisadi na umaarufu wake umeshuka kwa yeye kujifungamanisha na ufisadi.
 
Mpe moyo ila kumbuka katiba hiyo naye alishiriki kuitunga so kama sheria ujuavyo ni msumeno na safari hii imekula kwake
 
Kwan hii katiba ya CCM 1977 sio nayo inayozuia watu kupinga matokeo ya uraisi mahakamani? Sio hii inayomuweka Rais juu ya wote kuwa hawezi shitakiwa?

Enyi misukule je hilo la katiba ya CCM si kubwa zaidi ya ilo la katoba ya CDM?
 
Mimi hata sijaelewa unachokitetea. Cdm walishamalizsns na Zitto, akate rufaa asikate awe mbunge asiwe mbunge haifanyi tofauti. Elewa jambo dogo tu Chadema wanasema zzk sio mwanachama wao.
 
Katiba ya CDM haikatazi mwanachama kukishitaki mahakamani chama chake pale anapoona hakitendi haki au kimemkosea. Ukweli ni kuwa endapo mlalamikaji dhidi ya chama akishindwa shauri alilofungua, basi anapoteza uwanachama au kwa lugha nyingine akishinda kesi anaendelea na uwanachama wake kama kawaida. Mleta uzi unaelekea kuwa unampenda sana ZZK, tatizo la kupenda sana HUPOFUSHA. Haya uliyoandika yenye mtizamo wa upande mmoja ni matunda ya kupenda sana, angalia kote kote na uilinde taaluma yako kama kweli wewe ni Mwanasheria uongoze kundi la kurudi shule na nyuma yako awepo Msajili wa vyama vya siasa na vijana wake ndipo waje akina TL nyuma yenu.
 
Zito kama ni msafi, kwanini asiende ccm?

mwambie mzinzi slaa aludishe kadi ya ccm.zito siyo malaya wa siasa kama lema na msigwa mabele na slaa.hajawai miliki kadi ya chama kungine cha siasa zaidi ya cdm.
 
Hakuna mwanasheria mahiri kama Tundu Lisu,wewe sheria zako za kusomea chuo cha kata usizilite hapa utapata aibu.
 
sijawahi kuona chadema wakikurupuka ninauhakika wapo sahihi!!:embarassed2:
 
Duhh, Hivi ni kweli hapa Jamii Forums ni Home of Great Thinkers? Ingawa sijafanya utafiti, nashawishika kuhisi ni only 10-20% ndio wanaoweza kuwa great thinkers, Walio wengi uwezo wao unanipa mashaka makubwa... Ni uwanja wa matusi, Eneo la kampeni na sehemu ambayo watu wanarespond dhidi ya mtu/mchangiaji na siyo hoja... Kuna wakati mtu akishatupia hoja yake, analazimika kujitetea kabisa, eti 'naomba jamani watu tuchangie hiyo hoja, msinishambulie tafadhali', I see... Tubadilike Watanzania..
Kungekuwa na vigezo vya kujiunga na JF siyo kila mtu, Wengine wengi wangebaki kuwa Wasomaji tu, si kuchangia..
Hilo ni pendekezo langu kama kweli tuna malengo ya mabadiliko.. Kuna tofauti kubwa sana kati ya jamii forums na twitter..
Issue kubwa, Watu tunataka kujua nani hasa kapost pia, ID ziwe za ukweli, Sasa watu wanajiita Er.th.oc.te, Qu.n.ne, Tuj.te.em.e n.k. unaficha nini???
 
#team zzk mnasumbuka bure tuu..jamaa leo anaenda zake ATC alikowatanguliza kina mkumbo....
 
Wewe nadhani ni mwanasheria duni kupindukia.

Hivi hujawahi kuona hata baadhi ya mikataba ambayo huwa inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na kutokuelewana kati ya waliofunga mkataba, kwanza watakutana ndani ya vyombo vyao, na hivyo vyombo vyote vikishindwa ndipo watakwenda court of Law. Wewe ni mwanasheria gani usiyelijua hata hili?

Nilivyoelewa ni kuwa katiba ya CHADEMA imeeleza migogoro itatatuliwa vipi, rufaa itakatwa vipi ndani ya vyombo vya chama. Sasa endapo vyombo vyote vya chama, vya mwanzo na rufaa, vimetoa maamuzi yake na bado huridhiki, huzuiliwi kwenda mahakamani lakini kama mahakama itatoa ruling against you, utafukuzwa uanachama. Mimi nadhani huu uamuzi ni sahihi kabisa kwa chama cha siasa ili kuzuia watu wanaolala na kuamka kwenda mahakamani kuzuia maamuzi ya vikao halali vya chama kutendeka.

Lakini pia kuna taasisi ambazo zina miongozo inayotamka wazi kuwa kama hukukubaliana na uamuzi wa ngazi fulani, unaenda ngazi ipi mpaka ya mwisho, na kwa namna gani, na uamuzi wa ngazi ya mwisho hauhojiwi mahakamani. Na miongozo kama hiyo huwa ipo katika mambo ambayo maumuzi yanayotolewa huwa hayakiuki sheria za nchi na wala hakuna hitaji la kisheria la moja kwa moja. Sasa Zito kwa ujinga wake, alienda mahakamani kuzuia taratibu cha ndani ya chama zisifanyike yaani chama kisifuate katiba. Hutaki chama kifuate katiba wakati sheria ya vyama vya siasa inatamka ni lazima vyama vya siasa viendeshe mambo yake kwa kufuata katiba, wewe unayepinga vyama visifuate katiba, una akili?

Wewe naona ni mwanasheria wa sampuli za akina Ngeleja. Pole sana.

Katiba ya Chama chochote cha Siasa au kinginecho au sheria yoyote inayomzuia mtu yeyote kwenda Mahakamani kudai haki yake kwa kuona kama imekiukwa au inaelekea kukiukwa, katiba au Sheria hiyo ni batili tangu mwanzo wake (Null and void ab initio).

Ieleweke kuwa sheria yoyote inayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au katiba ya Chama chochote kiwe cha Siasa au kijamii au kikundi chochote cha watu haipaswi kuwa juu ya/ au kukiuka matakwa yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara husika ya Katiba ya CHADEMA ni kandamizi na imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mara kwa mara. Hata hivyo nawashangaa sana wananchi katika suala hili maana Mahakama haijatoa uamuzi juu ya uanachama wa Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA bali imetupilia mbali kesi yake kwa kuunga mkono pingamizi la awali (P.O) la mawakili wa CHADEMA kwamba kulikuwa na makosa ya kisheria kufungua kesi hiyo kwenye Mahakama kuu ya Tanzania tena kwenye masjala kuu ya Mahakama kuu ya Tanzania (Main Registry of the High Court of Tanzania) badala ya Masjala ya Wilaya ya Mahakama hiyo (District Registry of the High Court of Tanzania)

Na kwamba kesi hiyo ingefunguliwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mimi sipendi kuzungumzia uamuzi wa Mahakama kwenye forum hii maana maadili ya kazi zangu na taaluma yangu hayaniruhusu ila ninachotaka kufanya ni kumkosoa kaka yangu, msomi mwenzangu Tundu Lissu kwamba si kweli kwamba tangu Zitto alipofungua kesi yake mahakamani dhidi ya CHADEMA basi alikuwa si mwanachama tena wa CHADEMA kutokana na ibara ya katiba ya CHADEMA inavyosema, maana kama ingekuwa hivyo basi Zitto asingehudhulia Bungeni tangu tarehe 2/1/2014 lakini mbona ameendelea kuwa Mbunge hadi leo na hata siku zijazo mpaka utaratibu wa kisheria utakapofuatwa?

yeye Tundu ni nani hadi kutamka kwamba Zitto si mbunge tena wa Kigoma Kaskazini kama alivyotamka jana mbele ya waandishi wa habari? why souldn't he leave this matter to the proper authorities?

Hata kama Zitto akikoma kuwa Mbunge ni kwa mujibu wa katiba na Sheria za nchi na si kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA hasa kwa Ibara hiyo inayozuia mwanachama wa CHADEMA kwenda Mahakamani maana Ibara hiyo ni batlli na kinyume cha Katiba ya nchi.

Zitto bado ana fursa kubwa ya kwenda mahakama ya Rufaa kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi huo wa mahakama kuu na ni haki yake kuendelea na ubunge wake wakati akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambacho ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi juu ya haki za watu hapa Tanzania.

kwa msomi wa sheria na wakili mkongwe kama Tundu Lissu kukurupuka kwa hisia za kisiasa na kuropoka juu ya hatima ya Zitto ndani ya CHADEMA mimi naona kama ni tukano kwa taaluma hii ya kifalme (It is an abuse to this noble profession).

Taaluma hii sasa imeingiliwa na wanasiasa uchwara ambao wanaweza kusimama na kutamka lolote ili mradi tu wakidhi hoja zao za kisiasa badala ya kwenda kwenye uhalisia wa kisheria. Ndiyo maana hata Ngereja ambaye kitaaluma ni mwanasheria alipohojiwa na baraza la tume ya maadili ya viongozi katika kutoa utetezi wake anajitetea kuwa eti siyo yeye tu aliyepokea hela za escrow bali pia hata Zitto kabwe naye alipokea kutoka sehemu kadha wa kadha.

Uliona wapi mwanasheria wa kweli anatoa utetezi wa aina hiyo? Can somebody justfy wrongs because the same have been commited/done by somebody else? Unaua mtu kwa sababu fulani naye kaua? Hao ndo wanasheria dizaini ya Tundu Lissu, wanajua lakini wanajifanya hawajui ili kujustify position na kiu zao za kisiasa.

Mwisho Zitto nakupa nguvu uamue mambo haya kwa utashi wako mwenyewe. Ikiwa unaona unahitaji kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi wa mahakama kuu kutoka katika mahakama ya rufaa tanzania sisi tupo tayari kukusaidia hata bure kabisa tukiungana na Wakili Msomi Alberto Msando ili tafsri hiyo isiwe kwa manufaa yako tu bali kwa kizazi chote cha Tanzania.

Ni katika Mahakama ya rufaa tunaweza kupata maelekezo juu ya katiba mbovu za vyama kama CHADEMA zinazofifisha haki za watu/ wanachama wake kukishitaki chama wakati hilo ni takwa na haki ya kikatiba. Kuwa mwanamapinduzi kunahitaji moyo na muda.

Usikate tamaa, kama ni chama chao waachie kidizaini lakini twende Mahakama ya Rufaa tupate tafsri sahihi, na je Mahakama kuu kuendelea na kesi yako bila kutoa notisi kwako au kwa wakili wako kama tarehe ya kusikiliza ilibadilishwa kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ilikuwa sahihi(kama ni kweli)?

Hayo ndo mambo ya muhimu watanzania wangependa kujua na si longolongo za kisiasa kama za Tundu Lissu na wenzake wenye mtazamo kama huo.

Aluta Continua Comrade Zitto Zuberi Kabwe. Demokrasia ya kweli lazima izingatie sheria na Katiba za Nchi zilizo nzuri zisizokiuka haki za watu. Si sheria zote ni Sheria!
 
Back
Top Bottom