Tundu Lissu rudi Shule

Tundu Lissu rudi Shule

ninyi wanasheria wa Tz ni wehu sana. Njaa itaamaliza. Hata wewe kuna kamkate kako unatetea hapa. ZZK hajakanusha popote madai ya usaliti, that means tuhuma dhidi yake ni ukweli mtupu.
Kama hajaridhika akate rufaa kama ulivyomshauri

Tuhuma amejibu labda ulikusudia kujibu mahala unapokusudia wewe. Baadhi ya majibu ya tuhuma hizo tembelea tovuti yake, www.zittokabwe.com
 
When arguing with someone in an attempt to get at an answer or an explanation, you may come across a person who makes logical fallacies. Such discussions may prove futile. You might try asking for evidence and independent confirmation or provide other hypotheses that give a better or simpler explanation. If this fails, try to pinpoint the problem of your arguer's position. You might spot the problem of logic that prevents further exploration and attempt to inform your arguer about his fallacy.

.............Confirmation biased people (similar to observational selection): This refers to a form of selective thinking that focuses on evidence that supports what believers already believe while ignoring evidence that refutes their beliefs. Confirmation bias plays a stronger role when people base their beliefs upon tradition and prejudice.

Ungeandika kiswahili tungechangia vizuri.
 
jidanganye nan asiejua kuna wachaga wana id zaid ya 4 humu

Utapata shida sana hilo jina la wachaga lisipofutika kichwani mwako ushabiki mbaya sana ukiulizwa kwa nini hujui kazi unayo mfuate a.c.t kama imekuuma kajitundike.
 
Nimejaribu walau kusoma post yako nimeona kuwa wewe bado mchanga sana kisheria.
1. Katiba za vyama zinasajiliwa na msajili baada ya kujiridhisha kuwa zinaendana na katiba ya nchi na ndiyo chama kinapata uhai.
2. Mwenye mamlaka ya kusema kuwa katiba imevunjwa ni mahakama na sio wewe kama ulivyojipa mamlaka hayo
3.Katika kesi ya Anisminic Ltd v Foreign Compensation Commission where House of Lord held that a statutory exclusion clause does not deprive the courts from their jurisdiction in judicial review unless it expressly states
4. Ouster clauses katika sheria za kawaida haviinyimi mahakama usingizi wake.
5. Nyongeza ni kuwa Interlocutory orders are not Appealable.

Nakujibu hoja #1 hizo nyingine hazieleweki sababu mimi sio mwanasheria.
" 1. Katiba za vyama zinasajiliwa na msajili baada ya kujiridhisha kuwa zinaendana na katiba ya nchi na ndiyo chama kinapata uhai."
Sijajua kama kweli wewe ni mwanasheria, hivi katiba inapotungwa, kuandikwa mpaka kufikia kutumika inamaana ipo correct 100%? Kama ni hivyo kusingekua na marekebisho ya vifungu au katiba husika. Maana yangu hata kama watajiridhisha vipi bado huenda kukawa na makosa ndani yake.
 
Kule kwetu china hayo makanisa na misikiti. Tunazisajili kama kumbi za mikutano sio nyumba za ibada
 
kama unaona unadhulumiwa kwenye chama si uondoke kuliko kugangania, zitto si aondoke kwanini anagangania kubaki chadema,dhambi ya usaliti haisamehewi zitto kama yuda iskarioti.
 
Tundu Lisu ni mbabaishaji tu hata Mwakyembe alimwambia arudi shule ni mropokaji tu hana elimu thabiti.
 
Katiba ya TFF na ya FFA bac zisingekua na kifungu hicho(wambula) ..pia Msajiri asinge isange isajiri katiba hiyo
 
Ahsante mwanasheria kwa kutuletea ufafanuzi wa jambo hili... chimwechimwe
 
Last edited by a moderator:
Mi sio mwanasheria lakini nimesoma post yako naona imejaa povu nyingi sana, kwanza nakataa kwamba wewe ni mwanasheria labda ndio upo semester ya kwanza mwaka wa kwanza unasomea sheria. Na wala hukumuelewa Tundu Lisu hoja yake. labda uludi tena ukasome vizuri nini hasa kimefanya zito afukzwe.



sikupenda kuchangia mada hii kwa kuwa inaonekana na ya kihiyo wa sheria au kama ulivosema mwanafunzi wa sheria wa semister ya kwanza ya law certificate.

Mwanasheria eti hajui kuwa sheria ya vyama vya siasa chini ya msajili imekubali kusajiliwa katiba ya chadema ambayo mwenye mada anaisema ni void ab initio. Sasa kama sheria ya vyama vya siasa imeruhusu huo mwanya wa katiba kutungwa, kwa iyo Sheria ya vyama vya siasa ya1992 ni void? Je nani anaamuru kuwa sheria iyo ni void? Ni subject of it or the court of Law? na kama ni court - inasubiri nini?

mwanasheria hajui kuwa zipo sheria za vikundi au hata nchi zinazokataa kwenda mahakamani, ipo sheria ya magazeti, sheria za TFF, cdm, nk nk.( Ouster of jurisdiction) japo bound by (courts inherent powers) Hizi hazimnyimi mtu haki yake bali zinamtaka kwanza kufuata utaratibu waliojiwekea kabla ya kuiona chombo cha haki/mahakama,au hata kuheshimu maamuzi ayo ya vyombo au taasisi husika....PIA: Ningemshauri tu akifika semester ya kwanza ya digrii ya sheria asikimbie Law of Contract, kwa kuwa aya yaliyotokea yana contractual features/yaani kujiunga kwa kwenye chama ni kukubaliana na msharti ya chama, Sheria ya mikataba inatoa mwanya wa watu kukubaliana kutokwenda mahakamani endapo mkataba umekwama, ukisaini umekubali, ukikataa kwa hiari umekataa!


Mwanasheria anadai Lissu arudi darasani sijui kusoma tafsiri ya mahakama kumkatalia ombi lake, hajui kuwa ukienda mahakamani kuomba zuio/injuction , zuio likikataliwa ina maana makubaliano yenu ya awali kabla ya zuio yanaedelea as if no injuction was sought. Kwa maana hiyo, kama chama walishaazimia kumfukuza mwanachama, wanamfukuza then yeye akikimbia kuomba zuio likafeli, then maamuzi ya chama yanabaki pale pale, zuio likikubaliwa basi maamuzi ya chama hupoteza nguvu!! Zuio limefeli maamuzi ya chama yamekubaliwa....actually failure of injuction should cement that the court reaffirms the already taken steps/awards.
Mleta mada hapa unalaumu mwakilishi wa chama kwa kukumbushi maamuzi ya kamati kuu kabla ya zuio la mfukuzwa, au unalaumu mahakama kwa kukataa kutoa amri ya zuio la ayo maamuzi? Sipendi unipe jibu.

Mwanasheria anahoji mamlaka ya mwakilishi wa chama, anataka yatolewe na superior authority? ...Ukifika hatua ya mbele utafundishwa Administrative Law, ....iyo itakufundisha vitu kama Delegation authority, ...huwezi kuwapangia chama nani atoe tamko, wao na kwa wakati wao na kwa utaratibu wao uliokubaliwa na vikao vyao halali na kupitishwa na wengi wanajua nani akisemee chama. Pia atafundishwa kuwa ukishakuwa mwanasheria mkuu wa taasisi au jumuiya flani unapewa mamlaka za kisheria kutokana na kazi yako, aidha expressly au impliedly...pia ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa idara ya sheria katika taasisi ndiye anayeelekeza maamuzi yoooote ya kisheria ndani ya iyo taasisi, hawezi kumwachia mwenyekiti au mtunza hazina kutoa maelekezo ya kisheria katika suala husika, endapo utaratibu uliowekwa hauruhusu mkurugenzi kuja directly basi utakuwa umeeelekeza mkurugenzi uyo aripoti na kushauri kwa nani, je utaratibu na organization chart ya chadema ikoje??...pia sio lazima maelezo ya mkurugenzi au wakili kwenye tafsiri za kisheria yasubiri aliyemtuma/ anaweza kusema ila atakutana na mwajiri wake kwenye 'kwa nini unisemee'? nayo sio kwenye ishu za kisheria ....mfano wakili akitoka kwenye maamuzi na vyombo vya habari vikataka kumuhoji mambo ya kisheria, ni kihiyo pekee anaweza kusema ngoja nikamwombe mteja ruhusa- kwa mambo ambayo ni tafsiri za kisheria wala si siri za mteja [ni kwa asiyejielewa pekee]


Anamshauri aliyekataliwa zuio kwenda kuappeal kuomba tafsiri ya kisheria ...ni mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza anaweza kushauri ivo. Eti mtu aombe injuction/ mahakama ikatae,...kwa kukataa mahakama inakuwa imebariki maamuzi ya awali, sasa aliyenyimwa zuio akaappeal kuomba tafsiri ya sheria. Mbele ya mahakama lililetwa ombi la zuio, zuio limefeli then ubebe content nje ya document ya ombi then ukaappeal???
Je unaappeal kukataa kukataliwa zuio au unaappeal kuhusu mahamuzi ya chama na apo kumbuka hakuna maamuzi ya chama yaliyoshtakiwa bali alienda mahakamani kukataa kutolewa maamuzi na chama, je akaappeal kukataa zuio au maamuzi ya chama? Kama ni agaist maamuzi ya chama then anapasw kuappeal kwenye ngazi ya juu kwenye chama,...kama anaappeal against kukataliwa zuio basi atakuwa anaappeal kukataa kukosa zuio. Itakuwa ni Court V. Mlalamikaji , Content iwe : KUHUSU KUNYIMWA ZUIO
Je hicho kitu kipo kwenye sheria ??


Mtetezi anakataza doing an evil to justify other evil ila bado analeta kesi ya Ngeleja kwenye content ya zuio la mlalamikaji akihusisha lisu, the the emphasis of a wrong reverts to right?? Kama unalalamika kuhusu Lissu inakuwaje ulalamikie lissu compared to Ngeleja, treat different cases differently!!



kama haya yanajulikana kwa sisi watu wa kawaida, je mleta mada, mwanasheria nguli huyajui aya???Ni fedhea wala siwezi kubishana na mleta mada.
 
Sheria hii ndio kandamizi sababu mtu anaweza kuonewa na akaogopa kwenda mahakamani akihofia kushindwa kesi japo ana haki na kufutwa uanachama. Hamuoni kipengele hiki kinamnyima mtu haki yaki katiba?
Wanasheria tusaidieni.

Unavyo jiunga na chama au tasisi yeyote lazima inakatiba yake na sheria zake hata katika familia tuna sheria zetu na uki kiuka tuna kutenga Kama huna hoja tulia Dawa ikuingie
 
waulize wachaga kosa la zzk ni lip haswa,kwenda mahakaman au kutaka chama kikaguliwe au kuutaka uenyekit

Yawezekana katiba yao inakataza kukaguliwa, na pia inaelekeza mwenyekiti lazma awe mchaga
 
Tuhuma amejibu labda ulikusudia kujibu mahala unapokusudia wewe. Baadhi ya majibu ya tuhuma hizo tembelea tovuti yake, www.zittokabwe.com


tUHUMA HUJIBIWA KWENYE MAMLAKA HUSIKA SIO MTANDAONI...SUCH ANONIMOUS WRITINGS ARE NOT RELIABLE, MARA NGAPI WASANII WANAKANA TOVUTI ZAO?
 
Katiba ya Chama chochote cha Siasa au kinginecho au sheria yoyote inayomzuia mtu yeyote kwenda Mahakamani kudai haki yake kwa kuona kama imekiukwa au inaelekea kukiukwa, katiba au Sheria hiyo ni batili tangu mwanzo wake (Null and void ab initio).

Ieleweke kuwa sheria yoyote inayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au katiba ya Chama chochote kiwe cha Siasa au kijamii au kikundi chochote cha watu haipaswi kuwa juu ya/ au kukiuka matakwa yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara husika ya Katiba ya CHADEMA ni kandamizi na imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mara kwa mara. Hata hivyo nawashangaa sana wananchi katika suala hili maana Mahakama haijatoa uamuzi juu ya uanachama wa Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA bali imetupilia mbali kesi yake kwa kuunga mkono pingamizi la awali (P.O) la mawakili wa CHADEMA kwamba kulikuwa na makosa ya kisheria kufungua kesi hiyo kwenye Mahakama kuu ya Tanzania tena kwenye masjala kuu ya Mahakama kuu ya Tanzania (Main Registry of the High Court of Tanzania) badala ya Masjala ya Wilaya ya Mahakama hiyo (District Registry of the High Court of Tanzania)

Na kwamba kesi hiyo ingefunguliwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mimi sipendi kuzungumzia uamuzi wa Mahakama kwenye forum hii maana maadili ya kazi zangu na taaluma yangu hayaniruhusu ila ninachotaka kufanya ni kumkosoa kaka yangu, msomi mwenzangu Tundu Lissu kwamba si kweli kwamba tangu Zitto alipofungua kesi yake mahakamani dhidi ya CHADEMA basi alikuwa si mwanachama tena wa CHADEMA kutokana na ibara ya katiba ya CHADEMA inavyosema, maana kama ingekuwa hivyo basi Zitto asingehudhulia Bungeni tangu tarehe 2/1/2014 lakini mbona ameendelea kuwa Mbunge hadi leo na hata siku zijazo mpaka utaratibu wa kisheria utakapofuatwa?

yeye Tundu ni nani hadi kutamka kwamba Zitto si mbunge tena wa Kigoma Kaskazini kama alivyotamka jana mbele ya waandishi wa habari? why souldn't he leave this matter to the proper authorities?

Hata kama Zitto akikoma kuwa Mbunge ni kwa mujibu wa katiba na Sheria za nchi na si kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA hasa kwa Ibara hiyo inayozuia mwanachama wa CHADEMA kwenda Mahakamani maana Ibara hiyo ni batlli na kinyume cha Katiba ya nchi.

Zitto bado ana fursa kubwa ya kwenda mahakama ya Rufaa kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi huo wa mahakama kuu na ni haki yake kuendelea na ubunge wake wakati akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambacho ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi juu ya haki za watu hapa Tanzania.

kwa msomi wa sheria na wakili mkongwe kama Tundu Lissu kukurupuka kwa hisia za kisiasa na kuropoka juu ya hatima ya Zitto ndani ya CHADEMA mimi naona kama ni tukano kwa taaluma hii ya kifalme (It is an abuse to this noble profession).

Taaluma hii sasa imeingiliwa na wanasiasa uchwara ambao wanaweza kusimama na kutamka lolote ili mradi tu wakidhi hoja zao za kisiasa badala ya kwenda kwenye uhalisia wa kisheria. Ndiyo maana hata Ngereja ambaye kitaaluma ni mwanasheria alipohojiwa na baraza la tume ya maadili ya viongozi katika kutoa utetezi wake anajitetea kuwa eti siyo yeye tu aliyepokea hela za escrow bali pia hata Zitto kabwe naye alipokea kutoka sehemu kadha wa kadha.

Uliona wapi mwanasheria wa kweli anatoa utetezi wa aina hiyo? Can somebody justfy wrongs because the same have been commited/done by somebody else? Unaua mtu kwa sababu fulani naye kaua? Hao ndo wanasheria dizaini ya Tundu Lissu, wanajua lakini wanajifanya hawajui ili kujustify position na kiu zao za kisiasa.

Mwisho Zitto nakupa nguvu uamue mambo haya kwa utashi wako mwenyewe. Ikiwa unaona unahitaji kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi wa mahakama kuu kutoka katika mahakama ya rufaa tanzania sisi tupo tayari kukusaidia hata bure kabisa tukiungana na Wakili Msomi Alberto Msando ili tafsri hiyo isiwe kwa manufaa yako tu bali kwa kizazi chote cha Tanzania.

Ni katika Mahakama ya rufaa tunaweza kupata maelekezo juu ya katiba mbovu za vyama kama CHADEMA zinazofifisha haki za watu/ wanachama wake kukishitaki chama wakati hilo ni takwa na haki ya kikatiba. Kuwa mwanamapinduzi kunahitaji moyo na muda.

Usikate tamaa, kama ni chama chao waachie kidizaini lakini twende Mahakama ya Rufaa tupate tafsri sahihi, na je Mahakama kuu kuendelea na kesi yako bila kutoa notisi kwako au kwa wakili wako kama tarehe ya kusikiliza ilibadilishwa kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ilikuwa sahihi(kama ni kweli)?

Hayo ndo mambo ya muhimu watanzania wangependa kujua na si longolongo za kisiasa kama za Tundu Lissu na wenzake wenye mtazamo kama huo.

Aluta Continua Comrade Zitto Zuberi Kabwe. Demokrasia ya kweli lazima izingatie sheria na Katiba za Nchi zilizo nzuri zisizokiuka haki za watu. Si sheria zote ni Sheria!
Mimi sio mwanasheria na sina taaluma ya sheria ina ninataka kujua kutoka kwako mleta uzi huu. Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa daima imekuwa inaongozwa na Watanzania wenye taaluma ya sheria tena kwenye kiwango cha JAJI. Katiba zote za vyama vya siasa zinapelekwa kwa Msajili wa vyama vya siasa, anasoma na kuiridhia ndipo inapopewa baraka za kutumika. Je, vipengere kandamizi na vinavyokinzana na sheria mama ya nchi yaani Katiba ya JMT vilipataje baraka za Msajili na kuruhusu Katiba ya CDM itumike? Vinginevyo wanaotakiwa kurudi shule ni wengi tukianzia na Osisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
 
Mtoa mada japo anajiita mwanasheria, haijui sheria. Chama kina taratibu zake ndani ya chama ya kushughulikia matatizo. Yeyote mwenye shida afuate ngazi hizo mpaka mwisho. Zito hajazifuata. Akakimbilia mahakamani. Kwanini asikumbane na fagio la chama? Kumbuka kuwa uhai wa taasisi yeyote unapaswa kulindwa na sheria na kanuni. Zito kama naibu katibu mkuu wa chama alizijua hizo. Kama hakuziafiki angejiondoa chamani na kuukataa uongozi mapema. Kupinga sasa kunamuaibisha kwamba alikuwa kiongozi mbumbumbu. Kwa mantiki hii, hata vyama vya kimataifa mwenye wanasheria wa kimataifa kama FIFA vina katiba vyenye kipengele kama katiba ya CHADEMA. Mtoa mada aache kufikiri ndani ya box. Dunia ipo mbele zaidi ya upeo wake wa kufikiri. He should think outside the box. Katiba ya nchi haijavunjwa maana haki yake haijasikilizwa wala kuwakilishwa na mtuhumiwa kwenye ngazi nyingine za juu ndani ya chama.
 
Usaliti ni dhambi kubwa na kwa maana hiyo zitto hafit kuwa mwana harakati wa chadema laba aende kwa eacrow wenzie. Hakuna dhambi kubwa kama ya usaliti.


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom