Tundu Lissu rudi Shule

Tundu Lissu rudi Shule

Mtu yeyote katika chama chochote cha siasa anayekiuka katiba, adhabu yake inayomfaa ni kufukuzwa uanachama. Katiba ya CHADEMA inatamka kuwa maamuzi yoyote yale yatafanywa na vikao vya chama. Zito hataki maamuzi yafanyike katika vikao vya chama, anazuia vikao vya chama visifanyike. Hivi huyu kweli ni mwanademokrasia? Zito angekuwa mwerevu na mwenye akili iliyotulia, angefanya kila linalowezekana ndani ya vikao vya chama, apate utetezi au hata ikiwezekana kuomba msamaha kwenye vikao vya juu ili apunguziwe adhabu.

Zito kwa ukaidi na kiburi chake, licha ya watu wengi kumshauri, amejinyonga mwenyewe kisiasa. Aendelee kuwasikiliza akina Mwigulu na akina Mangula kuwa yeye bado ni mwanasiasa mahiri na kuwa hii ni hatua tu na siku moja atakuja kuibuka kisiasa lakini wenye jicho la tatu wanajua wazi kabisa, labda Zito afanyiwe overhaul la sivyo his descending move is progressively on track.
 
Mtu yeyote katika chama chochote cha siasa anayekiuka katiba, adhabu yake inayomfaa ni kufukuzwa uanachama. Katiba ya CHADEMA inatamka kuwa maamuzi yoyote yale yatafanywa na vikao vya chama. Zito hataki maamuzi yafanyike katika vikao vya chama, anazuia vikao vya chama visifanyike. Hivi huyu kweli ni mwanademokrasia? Zito angekuwa mwerevu na mwenye akili iliyotulia, angefanya kila linalowezekana ndani ya vikao vya chama, apate utetezi au hata ikiwezekana kuomba msamaha kwenye vikao vya juu ili apunguziwe adhabu.

Zito kwa ukaidi na kiburi chake, licha ya watu wengi kumshauri, amejinyonga mwenyewe kisiasa. Aendelee kuwasikiliza akina Mwigulu na akina Mangula kuwa yeye bado ni mwanasiasa mahiri na kuwa hii ni hatua tu na siku moja atakuja kuibuka kisiasa lakini wenye jicho la tatu wanajua wazi kabisa, labda Zito afanyiwe overhaul la sivyo his descending move is progressively on track.

CHADEMA wamechemsha kwa kuwa na katiba kandamizi.

Tundu Lissu amechemsha kwa kusimamia katiba kandamizi na kukurupuka kutangaza Zitto kajivua uanachama.

Zitto kachemsha kwa kujiambatanisha na chama chenye katiba kandamizi (licha ya kujiita cha Demokrasia) na kushindwa kumaliza matatizo yake ndani ya chama.

CCM imechemsha kwa kuchochea migogoro katika upinzani ambao hauhitaji hata kuchochewa ili kufarakana.

Wote baba yao mmoja.
 
wewe umeaandika taarabu tupu mwanzo mwisho kubwa jinga wewe chicken head, hujui laws na bylaws,kwani zitto lazima awe cdm? kama katiba ya chama ni kandamizi unachagua chama unachokiona nafuu au unaanzisha chama chama chako mwenyewe
IF UR IN ROME BEHAVE LIKE A ROMAN
 
Nimesoma aya moja nimegundua ni ujinga tu... Kiufupi ni kwamba katiba ya CHADEMA inatambulika mpaka kwa msajili wa vyama then who are you?

Huyu Jamaa anataka kujitangaza kuwa wakili Mkali kwa mgongo wa Tundu lisu, nafkri haijui katiba ya CHADEMA ndio maana kakurupuka na kujiandalia katiba itakayomsaidia Zito kushindwa tena, Huyu ni mbumbu kwani ameonekana kuegemea sana kwenye mtu aliyetumwa na chama kama msemaji yeye kamchukulia kama ametunga yeye. Ni sawa na ZKK kusema hii ni kwa sababu ya ESCROW wakati mwenye hoja ni Kafulila.
 
kwani ni lazima ZZK ubaki CHADEMA si uanzishe chama chako au kagombee uraisi sisiem, kama wewe unaweza unaweza kushindana na chama na unategemea kukishinda chama basi wewe ni bora kuliko chama na hapo ulipo sio mahali pako kapatafute ambako ni sawa na wewe
 
Mkuu Mselewa;

Niliposoma kichwa cha habari cha thread hii nilijua umekuja kulisaidia jukwaa kuelewa na labda kutoa ufafanuzi wa kisheria kwenye hiki ulichokiita "sakata la Zitto". Kwa bahati mbaya uzi huu haujawa exhaustive.

Kumekuwa na maoni mbalimbali juu ya hili suala ikiwa ni siku tatu sasa tangu mahakama itoe uamuzi wake. Baadhi wamekuwa wakijaribu kuuaminisha umma kuwa hili ni pigo kubwa kwa demokrasia na mageuzi nchini.

Kilicho nishangaza zaidi hata wanachama na viongozi wa CCM wameonyesha kusononeshwa na maamuzi haya wakidai eti "upinzani utayumba" na kwamba ndugu Zitto alipaswa kusamehewa.

CDM ni chama kinachoongozwa na katiba, kanuni na miongozo halali, na nina hakika documents hizi ndizo zimetumika/zitatumika katika maamuzi ya suala hili.

Nikuombe sasa utumie jicho lako la kisheria kutuongoza katika mjadala huu kwa manufaa ya jukwaa hili na Taifa.

Natanguliza shukrani.

Tatizo nikiweka jambo linaunganishwa kwenye uzi mwingine.Nimeshakata tamaa
 
Katiba ya Chama chochote cha Siasa au kinginecho au sheria yoyote inayomzuia mtu yeyote kwenda Mahakamani kudai haki yake kwa kuona kama imekiukwa au inaelekea kukiukwa, katiba au Sheria hiyo ni batili tangu mwanzo wake (Null and void ab initio).

Ieleweke kuwa sheria yoyote inayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au katiba ya Chama chochote kiwe cha Siasa au kijamii au kikundi chochote cha watu haipaswi kuwa juu ya/ au kukiuka matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara husika ya Katiba ya CHADEMA ni kandamizi na imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mara kwa mara. Hata hivyo nawashangaa sana wananchi katika suala hili maana Mahakama haijatoa uamuzi juu ya uanachama wa Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA bali imetupilia mbali kesi yake kwa kuunga mkono pingamizi la awali (P.O) la mawakili wa CHADEMA kwamba kulikuwa na makosa ya kisheria kufungua kesi hiyo kwenye Mahakama kuu ya Tanzania tena kwenye masjala kuu ya Mahakama kuu ya Tanzania (Main Registry of the High Court of Tanzania) badala ya Masjala ya Wilaya ya Mahakama hiyo (District Registry of the High Court of Tanzania)

Na kwamba kesi hiyo ingefunguliwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mimi sipendi kuzungumzia uamuzi wa Mahakama kwenye forum hii maana maadili ya kazi zangu na taaluma yangu hayaniruhusu ila ninachotaka kufanya ni kumkosoa kaka yangu, msomi mwenzangu Tundu Lissu kwamba si kweli kwamba tangu Zitto alipofungua kesi yake mahakamani dhidi ya CHADEMA basi alikuwa si mwanachama tena wa CHADEMA kutokana na ibara ya katiba ya CHADEMA inavyosema, maana kama ingekuwa hivyo basi Zitto asingehudhuria Bungeni tangu tarehe 2/1/2014 lakini mbona ameendelea kuwa Mbunge hadi leo na hata siku zijazo mpaka utaratibu wa kisheria utakapofuatwa?
Utakuwa umesoma vyuo vya kando kando mwanza huko au Iringa au Kurasini.
Lakini bandiko hili halisadifu Sheria ya UDSM na ndiyo madhara yake haya manawaponda mpaka ma senior wenu

Yeye Tundu ni nani hadi kutamka kwamba Zitto si mbunge tena wa Kigoma Kaskazini kama alivyotamka jana mbele ya waandishi wa habari? Why souldn't he leave this matter to the proper authorities?

Hata kama Zitto akikoma kuwa Mbunge ni kwa mujibu wa katiba na Sheria za nchi na si kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA hasa kwa Ibara hiyo inayozuia mwanachama wa CHADEMA kwenda Mahakamani maana Ibara hiyo ni batili na kinyume cha Katiba ya nchi.

Zitto bado ana fursa kubwa ya kwenda mahakama ya Rufaa kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi huo wa mahakama kuu na ni haki yake kuendelea na ubunge wake wakati akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambacho ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi juu ya haki za watu hapa Tanzania.

Kwa msomi wa sheria na wakili mkongwe kama Tundu Lissu kukurupuka kwa hisia za kisiasa na kuropoka juu ya hatima ya Zitto ndani ya CHADEMA mimi naona kama ni tukano kwa taaluma hii ya kifalme (It is an abuse to this noble profession).

Taaluma hii sasa imeingiliwa na wanasiasa uchwara ambao wanaweza kusimama na kutamka lolote ili mradi tu wakidhi hoja zao za kisiasa badala ya kwenda kwenye uhalisia wa kisheria. Ndiyo maana hata Ngeleja ambaye kitaaluma ni mwanasheria alipohojiwa na baraza la tume ya maadili ya viongozi katika kutoa utetezi wake anajitetea kuwa eti siyo yeye tu aliyepokea hela za escrow bali pia hata Zitto Kabwe naye alipokea kutoka sehemu kadha wa kadha.

Uliona wapi mwanasheria wa kweli anatoa utetezi wa aina hiyo? Can somebody justfy wrongs because the same have been commited/done by somebody else? Unaua mtu kwa sababu fulani naye kaua? Hao ndo wanasheria dizaini ya Tundu Lissu, wanajua lakini wanajifanya hawajui ili kujustify position na kiu zao za kisiasa.

Mwisho Zitto nakupa nguvu uamue mambo haya kwa utashi wako mwenyewe. Ikiwa unaona unahitaji kupata tafsri sahihi juu ya uamuzi wa mahakama kuu kutoka katika mahakama ya rufaa Tanzania sisi tupo tayari kukusaidia hata bure kabisa tukiungana na Wakili Msomi Alberto Msando ili tafsri hiyo isiwe kwa manufaa yako tu bali kwa kizazi chote cha Tanzania.

Ni katika Mahakama ya rufaa tunaweza kupata maelekezo juu ya katiba mbovu za vyama kama CHADEMA zinazofifisha haki za watu/ wanachama wake kukishitaki chama wakati hilo ni takwa na haki ya kikatiba. Kuwa mwanamapinduzi kunahitaji moyo na muda.

Usikate tamaa, kama ni chama chao waachie kidizaini lakini twende Mahakama ya Rufaa tupate tafsri sahihi, na je Mahakama kuu kuendelea na kesi yako bila kutoa notisi kwako au kwa wakili wako kama tarehe ya kusikiliza ilibadilishwa kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ilikuwa sahihi(kama ni kweli)?

Hayo ndo mambo ya muhimu watanzania wangependa kujua na si longolongo za kisiasa kama za Tundu Lissu na wenzake wenye mtazamo kama huo.

Aluta Continua Comrade Zitto Zuberi Kabwe. Demokrasia ya kweli lazima izingatie sheria na Katiba za Nchi zilizo nzuri zisizokiuka haki za watu. Si sheria zote ni Sheria!

Utakuwa umesoma vyuo vya kando kando mwanza huko au Iringa au Kurasini.
Lakini bandiko hili halisadifu Sheria ya UDSM na ndiyo madhara yake haya manawaponda mpaka ma senior wenu
 
Kijana umeandika mengi yasiyo na msingi wowote.Baada ya kusoma paragraph ya kwanza tu hapo juu nimeona "hujui lolote"na wala "hujui yaliyoendelea mahakamani".Ili upate uhalali wa kuchangia jambo, ni vizuri ukajipa muda wa kusoma na kujifunza juu ya kitu hicho.
Kwa taarifa yako tu ni kuwa "Jaji John utamwa alikubaliana na hoja ya chadema kuwa kesi hiyo ifutwe kwa kuwa inakiuka KATIBA YA CHAMA".Acha kuandika ujinga ndugu yangu.Soma hukumu ya mahakama kwanza.
 
chimwemwe67
Ninyi wanasheria wa Tz ni wehu sana. Njaa itaamaliza. Hata wewe kuna kamkate kako unatetea hapa. ZZK hajakanusha popote madai ya usaliti, that means tuhuma dhidi yake ni ukweli mtupu.

Kama hajaridhika akate rufaa kama ulivyomshauri

kwani kukanusha kuna maana yeyote ile kwako? hata akikanusha kama mipango ni kukutoa, kanusho lako halitakuwa na maana yeyote ile.
Jaribu kuingia ktk siasa ndio utaona utamu wake
 
Unasemaje juu ya katiba ya TFF inayokataza mambo ya soka kupelekwa mahakamani? Kila chombo, chama, asasi, etc kinakuwa na sheria zake, ukikiuka uaweza kufukuzwa uanachama. Zito alikiuka na yaliyomkuta sasa ni historia.
 
Back
Top Bottom