Tundu Lissu rudi Shule

Tundu Lissu rudi Shule

Sasa iko wazi kuwa Zitto Kabwe ametangazwa kuvuliwa uanachama wa CHADEMA. Inajulikana kuwa sakata la Zitto lilianzia kwenye ulioitwa mkakati wa mabadiliko uliowahusisha pia Prof. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Baada ya Mkakati wa Mabadiliko kuwekwa wazi/kugunduliwa,kikao cha Kamati Kuu cha CHADEMA kilifanyika kuwajadili wahusika. Waliohusishwa ni Zitto,Prof. Kitila na Mwigamba. Kikao husika kiliwavua nafasi za uongozi wahusika. Zitto alipokwa Unaibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Kuvuliwa uongozi kwa wahusika ulikuwa uamuzi wa dharura na wa haraka ili kupisha uchunguzi wa kina na kuandaliwa kwa mashtaka dhidi yao.

Mashtaka yaliandaliwa na kupelekwa kwa wahusika. Kikao kingine cha Kamati Kuu kiliitishwa. Kililenga kuwahoji,kujadili na kuamua juu ya mashtaka dhidi ya akina Zitto. Kabla ya kikao kufanyika,Zitto alikwenda Mahakama Kuu kuzuia kujadiliwa.

Wenzake hawakwenda Mahakamani. Walijadiliwa na kuvuliwa uanachama wao wa CHADEMA. Mahakamani Zitto alikuwa na maombi madogo na maombi makubwa. Madogo yalikuwa ya dharura. Ya kuizuia Kamati Kuu kumjadili. Ikumbukwe kuwa wakati Zitto anakwenda Mahakamani kikao hakikuwa kimefanyika.

Zitto alifanikiwa kupata zuio la muda kujadiliwa chamani na kimsingi hakujadiliwa kwenye Kamati Kuu iliyoitishwa na wala vikao vilivyofuata. Jaji John Utamwa pia alimuamuru Katibu Mkuu ampe Zitto mwenendo wa Kamati Kuu iliyompoka uongozi.

Mahakamani yalibaki maombi mengine ya kuendelea kuzuiwa kwa CHADEMA kumjadili Zitto hadi atakapowasilisha rufani yake Baraza Kuu. Ni maombi hayo ambayo Mawakili Wasomi wa CHADEMA waliyawasilishi pingamizi la awali.

Kisheria,pingamizi la awali huusiana hasa na mambo ya kisheria kama mamlaka ya mahakama,uwezo wa mwombaji wa kuweza kuomba,matakwa ya nyaraka na kadhalika. Linapowekwa pingamizi la awali,kesi au ombi ya msingi husimama.

Litakaposikilizwa pingamizi la awali na kukubaliwa,kesi ya msingi hutupwa. Linapokataliwa,kesi ya msingi huendelea. Ieleweke kuwa pingamizi la awali linasikilizwa na kuamuliwa rasmi kimahakama kwa kutolewa uamuzi.

Pingamizi la CHADEMA lilijikita hasa kwenye uhalali wa maombi ya Zitto kuwa Masjala kuu ya Mahakama Kuu ya Tanzania-High Court Main Registry. Ikadadavuliwa kuwa Zitto alipaswa kuwasilisha maombi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi au Masjala ya Wilaya ya Mahakama Kuu-High Court District Registry.

Pingamizi likapangiwa siku ya kusikilizwa. Siku ilipofika timu za Mawakili wasomi wa wahusika zikajitokeza mahakamani,mbele ya Jaji Utamwa,na kusikilizwa juu ya pingamizi hilo. Mawakili wakaeleza hoja na kila mmoja akasikilizwa. Mwisho mwishoni,Jaji akapanga siku ya kutoa uamuzi juu ya pingamizi hilo ili ijulikane kama maombi ya Zitto yangeendelea kusikilizwa au la.
 
Chimwemwe usipate taaabu Tundu anajua anachofanya, anajitoa akili ili kukidhi mahitaji yake asipofanya hivo wenye chama na yeye watamuonyesha mlango wa kutokea.

Zitto bora akaushe tu wananchi wanaona, hakuna haja ya kurudi court hao jamaa sio wazuri kivile. Siunaona ameondoka lakini kinaumana ndani.
 
Hata katiba za vyama vya mpira zimetamka hivyo. Hii ni kuhifadhi heshima ya chama. Hata mke au mtoto ayekimbilia mahakamani kumshitaki baba au familia badala ya ukoo, mke huyo au mtoto havumiliki hata kidogo.
 
Utapata shida sana hilo jina la wachaga lisipofutika kichwani mwako ushabiki mbaya sana ukiulizwa kwa nini hujui kazi unayo mfuate a.c.t kama imekuuma kajitundike.

samahan masawe,kwa taarfa yako mi nilikua naunga mkono sana chdm ila uchaga ndan ya chama ndo umenifanya nitoe iman kabsa,haiwezekan hakuna mchaga aliewah kuadhibiwa ilhal wanamakosa lukuki
 
Sakaya la Zitto lilianza pale alipotia nia ya kugombea uenyekiti wa chadema, na tushukuru hadi leo yuko hai. R.I.P Chacha Wangwe.
 
Kwa hiyo TFF si chombo halali kishetia kwa hapa nchini kwani nao kayiba yao hairuhusu mwanachama au mwanamichozo kuungulia kesi mahakamani???
 
Nakujibu hoja #1 hizo nyingine hazieleweki sababu mimi sio mwanasheria.
" 1. Katiba za vyama zinasajiliwa na msajili baada ya kujiridhisha kuwa zinaendana na katiba ya nchi na ndiyo chama kinapata uhai."
Sijajua kama kweli wewe ni mwanasheria, hivi katiba inapotungwa, kuandikwa mpaka kufikia kutumika inamaana ipo correct 100%? Kama ni hivyo kusingekua na marekebisho ya vifungu au katiba husika. Maana yangu hata kama watajiridhisha vipi bado huenda kukawa na makosa ndani yake.

That is lay man arguement.
Do you think that amendment of law is due to illigality of some provisions or what?.
Law are generally amended to suit the circumtance of the prevailling social,political and Economic development since the society is not stagnant!
 
samahan masawe,kwa taarfa yako mi nilikua naunga mkono sana chdm ila uchaga ndan ya chama ndo umenifanya nitoe iman kabsa,haiwezekan hakuna mchaga aliewah kuadhibiwa ilhal wanamakosa lukuki

Jenga hoja acha kupapasa na mimi sio massawe kuwa na wivu wa kifikra na maendeleo sio kuwa na wivu wa kichawi matokeo yake unayajua .
 
Kama soka tu....hukatazwi kwenda mahakamani, lakini ukienda umejifuta.
 
Sakaya la Zitto lilianza pale alipotia nia ya kugombea uenyekiti wa chadema, na tushukuru hadi leo yuko hai. R.I.P Chacha Wangwe.
Na wewe huu ndio uchambuzi wako katika jicho la kisheria?

Mkuu Petro E. Mselewa nahisi kama umeishia njiani, malizia mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mselewa;

Niliposoma kichwa cha habari cha thread hii nilijua umekuja kulisaidia jukwaa kuelewa na labda kutoa ufafanuzi wa kisheria kwenye hiki ulichokiita "sakata la Zitto". Kwa bahati mbaya uzi huu haujawa exhaustive.

Kumekuwa na maoni mbalimbali juu ya hili suala ikiwa ni siku tatu sasa tangu mahakama itoe uamuzi wake. Baadhi wamekuwa wakijaribu kuuaminisha umma kuwa hili ni pigo kubwa kwa demokrasia na mageuzi nchini.

Kilicho nishangaza zaidi hata wanachama na viongozi wa CCM wameonyesha kusononeshwa na maamuzi haya wakidai eti "upinzani utayumba" na kwamba ndugu Zitto alipaswa kusamehewa.

CDM ni chama kinachoongozwa na katiba, kanuni na miongozo halali, na nina hakika documents hizi ndizo zimetumika/zitatumika katika maamuzi ya suala hili.

Nikuombe sasa utumie jicho lako la kisheria kutuongoza katika mjadala huu kwa manufaa ya jukwaa hili na Taifa.

Natanguliza shukrani.
 
chimwemwe67 jinsi ulivyoandika tu unaonekana kuwa na jazba na kuonyesha uadui wako kwa Mh.Tundu Lisu.
Ungetulia kwanza ukawaza kuikosoa katiba ya chama chao. Lakini kusema maneno mengi namna hiyo hapo juu umeshindwa kuijenga hoja ile ya kisomi uliyokuwa unataka kuandika kwa sababu umelenga zaidi kum-attack Tundu Lisu. In short you simply sound like bodyguard wa Zitto.
 
Siku ambayo Chadema wanaota kutawala nchi nina uhakika mhimili wa MAHAKAMA hautakuwepo.Kwa kuwa katiba yao haitambui mahakama kama chombo cha kusimamia Haki.

Mkuu Mingoi,cha ajabu zaidi ukiacha hilo la katiba yao kutotambua mahakama kama chombo cha utoaji haki,ni kwa baadhi ya viongozi wake waandamizi ambao maisha yao yanategemea mahakama kwa kiwango kikubwa sana.Wanaishi vizuri kwa sababu ya mahakama,huku pembeni hawaitambui,what a shame!
 
Mods mmenikatisha tamaa ya kuendelea kuandika. Kwanini kila ninachoandika kuhusu Zitto mnaunganisha na wengine mnawaacha?

Mkuu Invisible,hii si haki
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom