Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Ratiba ya kampeni visiwani Zanzibar - Sept 7, 2020

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,198
Live : Shughuli nzima ya Kampeni ya Tundu Lissu leo Zanzibar


Source : swahili villa

Mapokezi ya Tundu Lissu alipowasili airport Zanzibar

Updates:
LISSU AKIZUNGUMZIA KUMUUNGA MKONO MAALIM SEIF UCHAGUZI WA ZANZIBAR
Tundu Lissu : Uchaguzi huu ni muhimu kwa taifa la Zanzibar lazima maamuzi magumu yafanyike hapa Zanzibar na kule Tanganyika

7 Sep 2020
Mgombea Urais wa Chadema, Tundu Lissu amesema Chama hicho kitamuunga mkono Maalim Seif kwa nafasi ya Urais Zanzibar kwa kuwa ndio mgombea pekee mwenye nguvu. Lissu ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya kibanda Maiti mjini Unguja. Hata hivyo Lissu amesema kwa upande wa Tanzania Bara wanachama wa cha ACT Wazalendo kumuunga mkono Mgombea wa Chadema ambae ni yeye
Source: mwananchi digital

SIKU YA JUMATATU SEPTEMBA 07, 2020

Asalaam alyekum Waheshimiwa Viongozi, Wagombea wa Ubunge, Uwakilishi, Udiwani, Wanachama, Wadau na Wapenzi wa Chadema na Upinzani kwa ujumla.




Source : Swahili Villa
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu akiambatana na mgombea mwenza wake Mheshimiwa Salum Mwalim watakuwa na mkutano wa ufunguzi wa kampeni Zanzibar, siku ya Jumatatu Septemba 07, 2020 kuanzia Saa nane Mchana katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja, Zanzibar.

Mheshimiwa Lissu ataongozana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema Mheshimiwa John John Mnyika na viongozi wengine mbalimbali wa chama CHADEMA.

Mapokezi yatafanyika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar Abeid Amani Karume international Airport kuanzia Saa nne za Asubuhi.

Msafara utatoka Uwanja wa ndege na kupita katika maeneo yafuatayo Kiembesamaki, Magomeni kwa Mchina, Mwanakwerekwe, Magomeni, Kwa Boko, Mwembenjugu, Kwa Alimsha, Karikakoo, Bizired, BOT Mkunazini, Mlandege, Michenzani na kuelekea Kisiwandui zilipo Ofisi za chama za CHADEMA.

Kisha na kufatiwa na Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Viwanja vya Kibandamaiti kuanzia Saa nane za mchana.

Pamoja na salaam za chama

Kado Salmini Mwalimu
Kny Naibu Katibu Mkuu
Chadema, Zanzibar

Source: Swahili Villa
 
Karibu sana visiwani mzee Lissu.

Endelea vile vile kutumia kauli laini zenye kuchoma usije kuteleza kidogo wakatafuta sababu ya kukuweka kizuizini.

Mungu yuko nawe ndio maana lisasi 16 hazikuwa kikwazo cha wewe kutengana na ulimwengu wa mwili.

Hata kama ikitokea hujashinda nina imani kubwa kuwa utabadilisha mengi katika Nchi hii na umekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika tanzania.

Kama imetumika nguvu yamwisho yenye matokeo ya kifo chako na haukunyamaza basi hakuna kingine cha kuhofia na kukuogopesha ambacho kinaweza kukunyamazisha usiongee ambayo unataka watanzania tusikie.

Uzuri ni kuwa huongei propaganda unaongea vitu vipo kwa hiyo huna kazi kubwa saana ya kuwaaminisha watanzania kasoro za kile unachokikosoa wakati kasoro hizo zimekuwa waaadhwih kwa watanzania wemyewe.

Hongera sana kwa unasiri wako mzee Lissu
 
Duuuh, kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani, huku Chato, Kahama, Bukene, Kaliua,Uvinza, Kigoma, Tukuyu, nk, halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura.
 
Kesho sera za Uhuru , Haki na Maendeleo ya Watu zinavuka bahari na kutua upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama kawaida kura za mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupewa kwa wingi yule asiyetokea CCM tangu mfumo wa vyama vingi kuasisiwa mwaka 1992 nchini Tanzania.

Itoshe kusema kuwa Zanzibar ni ngome ya kuaminika kwa mgombea yeyote anayesimama dhidi ya CCM na hivyo mkutano wa kampeni za Urais wa Jamhuri ya Muungano visiwani Zanzibar ni zoezi muhimu kuwathibitishia waZanzibari kuwa tunayaenzi maamuzi yao ya kuwa upande wa chama mbadala.
 
Duuuh,kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani,huku chato,Kahama,bukene,Kaliua,Uvinza,Kigoma,Tukuyu,nk,halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura
Mbona ratiba bado zinaendelea acha lawamaa za ajabu kuna siku 50 za kampeni maeneo yote atafika
 
Duuuh,kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani,huku chato,Kahama,bukene,Kaliua,Uvinza,Kigoma,Tukuyu,nk,halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura
Usiwe mjinga! Fuatilia maelezo kwa kina ili uelewe. Chadema wanachofanya sasa hivi ulikuwa uzinduzi wa kampeni katika kanda zake 10.
Ndio maana uongozi wote umeambatana pamoja. Kinachofuatia ni kutawanyika kila wilaya na vijiji kadhaa kufikiwa
 
Duuuh,kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani,huku chato, Kahama, bukene, Kaliua, Uvinza, Kigoma, Tukuyu, nk, halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura
Angalia Zoba hili
Kwani kwenda Zanzibar ndio Mwisho wa Kampeni?
 
Duuuh,kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani,huku chato,Kahama,bukene,Kaliua,Uvinza,Kigoma,Tukuyu,nk,halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura
Tulia wewe watu wanafanya Kampeni kwa strategy kinachofanyika ni uzinduzi tu kisha tunarudi Dar kupiga pasi wilaya kwa wilaya kata kwa kata mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyumba kisha utaona Moto cha muhimu tunza card yako yakupigia Kura tukutane 28/10.
 
Duuuh,kwahiyo huku bara Kesha maliza!wengine hatujamuona jamani,huku chato,Kahama,bukene,Kaliua,Uvinza,Kigoma,Tukuyu,nk,halafu tukishindwa tutasema tumeibiwa kura
CHADEMA imeanza na uzinduzi wa kanda kwanza then wanarudi kuanza sasa
 
Anaenda kunadi sera za alivyopigwa risasi.Mandela angekuwa kama Lissu hotuba zake zote zingehusu magereza
Wewe umesoma vitabu vya Mandela? Na umesikia hotuba zake?? Bila magereza basi hizo siyo hotuba zake. Hili la kumpiga risasi Lisu lazima liwatese sana. Na lazima aseme
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom