Tundu Lissu: Rais Magufuli ana shida gani na misiba mikubwa?

Naomba na hili la maafa nilizungumzie kidogo kabla halijazikwa na maajabu mengine ya nchi yetu.

Nadhani Mheshimiwa Rais wetu ana tatizo kubwa na misiba ya kitaifa ambalo wanaofahamu zaidi wanabidi watueleze.

1. Walipokufa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Arusha mwezi Mei 2017, Rais Magufuli hakuhudhuria mazishi yale, ijapokuwa alikuwepo nchini. Serikali ikawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

2. Walipokufa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi mwezi September 2016, Rais Magufuli, aliyekuwa asafiri kwenda Zambia, aliahirisha safari hiyo lakini hakuonekana kwenye mazishi ya wahanga hao. Serikali ikawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

3. Walipouawa askari polisi 7 kule Kibiti Ijumaa Kuu ya 2017, Rais Magufuli alikuwepo nchini. Hata hivyo, hakuhudhuria mazishi ya askari polisi hao, badala yake aliyeonekana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba.

4. Mara wakauawa wanajeshi wetu wa kikosi cha kulinda amani nchi DR Congo mwezi December 2017. Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hakuonekana Uwanja wa Taifa kwenye mazishi ya wanajeshi wetu. Aliyekwenda kwa niaba ya Serikali ni Waziri Mkuu Majaliwa.

5. Sasa wamekufa zaidi ya watu 200 kwenye Janga la MV Nyerere. Rais wetu badala ya kwenda kwenye mazishi, amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa ili yeye apate wasaa wa kunywa chai Ikulu na mapolisi wa usalama barabarani!!!

Rais wetu una shida gani na misiba hii ya kitaifa???

Kama ni hoja kutoka kwa TAML- nafikiri amejidogosha.
Hizi ni issues ndogo kwa level yake kuongelea. Awaachie wadogo kukomaa na haya yasiyokuwa na uhakika.
Nijuavyo urais ni taasisi. Hajiendei tu. Kuna watu wenye kazi ya kushauri aende wapi?.

Well response ilichelewa, but atleast wamefanya kwa uwezo wao.
 
Kuna kitu ambacho mimi na wewe hatuelewi!!!

Muda wa kushirikiana na unaowaongoza katika maafa huna ila muda wa kupata chai na wakusanya kodi zisizo rasmi za barabarani, unao tele. Sijuo kama kuna mwenye akili atalielewa hili.

Hii ni ishara ya nini? Je, ni ukatili? Imani za kishirikina? Ni kutojali watu wako? Hakuna ajuaye. Ni sababu gani hasa? Watanzania ni lazima tujiulize sana.
Nani ajuaye kana alichokuwa anakunywa na kula pale ilikuwa ni chai huku watu walikuwa wanazikwa?? Labda tuiite chai yakitaifa...
Hivi wale ni viongozi wa matrafiki au??
 
Lisu anataka kumfanya rais awe bize kuhudhuria misiba kama vile ndiyo kazi ya Rais! Kuna mengi huwa namuunga mkono Lisu, lkn kama hii kauli ni yake, basi amepotoka, misiba sio siasa.

Vv
 
WAFALME HUWA HAWARUHUSIWI KWENDA KWENYE MISIBA, hiyo ni sheria ya zamani, mbona CHAMA CHAKO HAKIJNA MTU ALIYE KUJA KUKUONA? Una matatizo gani? Awamu hazifanani walahi!
Kaa kimya kula painkillers get high ndio mchezo mzima walahi tundulissimsaliti!
Sheria ya dhamana yao inawaruhusu kutoka nje ya dar? Sababu wanakesi wote.
 
Ubongo wa Tundu Lisu nadhani una Uvimbe, Urais ni Taasisi siyo mtu
Tatizo lako ni kukariri. Unamaanisha nini unaposema Urais ni Taasisi? Unajua maana ya hii statement na muktadha wa kinachozungumzwa hapa? Tukio kubwa lilioishtua dunia nzima, Mh rais katulizana zake ikulu kama vile ni jambo dogo? halafu juzi alipoona kelele nyingi na lawama anajitutumua eti kutoa kimilioni kimoja kwa wahanga. Rais wetu ana tatizo wallah!
 
Ukiambiwa chakula kina chumvi nyingi, kuonyesha umesikia hizo lawama ni kutokuweka kabisa? Kila jambo lifanyike kwa kiwango sio kuzidisha au kutukufanya kabisa.
Sema mnaipenda sura na swaga zake tu!
kwani misiba imeisha?
 
Ndio wazee wa matukio. Ila kwa hili la MV. NYERERE mmechemka sana. Hivi mbowe alienda huko kuzika.
Mwanasiasa anabaki kuvizia matukio kujenga hoja uchwara na kuondoa akili za watanzania wengi kwenye jambo la msingi kuomboleza vifo vya wafiwa. Hivi mnataka rais aazime vichwa vyenu ili awaze na kutenda sawasawa na mnachowaza.
Rudi hapo juu kwenye mchango wa Nguruvi3 msikie Kabudi alisemaje kuhusu RAISI WA NCHI kwa mujibu wa katiba ya nchi halafu jishangae wewe ulichoandika hapo MBOWE ni raisi wa nchi gani tena??
 
Naomba na hili la maafa nilizungumzie kidogo kabla halijazikwa na maajabu mengine ya nchi yetu.

Nadhani Mheshimiwa Rais wetu ana tatizo kubwa na misiba ya kitaifa ambalo wanaofahamu zaidi wanabidi watueleze.

1. Walipokufa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Arusha mwezi Mei 2017, Rais Magufuli hakuhudhuria mazishi yale, ijapokuwa alikuwepo nchini. Serikali ikawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

2. Walipokufa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi mwezi September 2016, Rais Magufuli, aliyekuwa asafiri kwenda Zambia, aliahirisha safari hiyo lakini hakuonekana kwenye mazishi ya wahanga hao. Serikali ikawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

3. Walipouawa askari polisi 7 kule Kibiti Ijumaa Kuu ya 2017, Rais Magufuli alikuwepo nchini. Hata hivyo, hakuhudhuria mazishi ya askari polisi hao, badala yake aliyeonekana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba.

4. Mara wakauawa wanajeshi wetu wa kikosi cha kulinda amani nchi DR Congo mwezi December 2017. Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hakuonekana Uwanja wa Taifa kwenye mazishi ya wanajeshi wetu. Aliyekwenda kwa niaba ya Serikali ni Waziri Mkuu Majaliwa.

5. Sasa wamekufa zaidi ya watu 200 kwenye Janga la MV Nyerere. Rais wetu badala ya kwenda kwenye mazishi, amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa ili yeye apate wasaa wa kunywa chai Ikulu na mapolisi wa usalama barabarani!!!

Rais wetu una shida gani na misiba hii ya kitaifa???
Yeye anaona kupigwa risasi 30 sio shida?Kweli Nyani haoni kundule.Si afadhali kwa case ya Maguli kama anadhani ni kafara inawezekana sio kafara la Magufuli per se,but rather la mtu mwingine.Kwa case yake,whatever happened to him is a personal problem.The whole scenario shows that he is spiritually bankrupt. Lissu angekuwa a real spiritual man,God would protect him 100%.
 
Mshirikina yule yule mzee sio bure. Haya ni matokeo ya kupewa mamlaka ya washirikina.
 
Msiba mwingine mmepanga ni lini ili aende!? Hamna msukuma ana swaga, ama huzijui swaga nini?
Ongezeni maombi kwa huyo mnaemuombaga ili hatimaye muweze kumuona sura yake mliyoimiss.
Kweli msukuma hana swaga yeye ni kazi tu!
 
Akienda shida asipokwenda shida..Hulka ya binadamu haridhiki hata ufanye nini.Fanya unayoweza chapa mwendo
 
Ongezeni maombi kwa huyo mnaemuombaga ili hatimaye muweze kumuona sura yake mliyoimiss.
Kweli msukuma hana swaga yeye ni kazi tu!

Sio kwamba hazitaki hizo swaga bali anapishana na beat. Yale makoti oversize na swaga wapi na wapi? Kazi tu bila maarifa ni sawa na kuanika nguo kavu.
 
Yeye anaona kupigwa risasi 30 sio shida?Kweli Nyani haoni kundule.Si afadhali kwa case ya Maguli kama anadhani ni kafara inawezekana sio kafara la Magufuli per se,but rather la mtu mwingine.Kwa case yake,whatever happened to him is a personal problem.The whole scenario shows that he is spiritually bankrupt. Lissu angekuwa a real spiritual man,God would protect him 100%.
Ndo umeandika nini sasa?:confused:
 
Back
Top Bottom