Tundu Lissu: Rais Magufuli ana shida gani na misiba mikubwa?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Naomba na hili la maafa nilizungumzie kidogo kabla halijazikwa na maajabu mengine ya nchi yetu.

Nadhani Mheshimiwa Rais wetu ana tatizo kubwa na misiba ya kitaifa ambalo wanaofahamu zaidi wanabidi watueleze.

1. Walipokufa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Arusha mwezi Mei 2017, Rais Magufuli hakuhudhuria mazishi yale, ijapokuwa alikuwepo nchini. Serikali ikawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

2. Walipokufa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi mwezi September 2016, Rais Magufuli, aliyekuwa asafiri kwenda Zambia, aliahirisha safari hiyo lakini hakuonekana kwenye mazishi ya wahanga hao. Serikali ikawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

3. Walipouawa askari polisi 7 kule Kibiti Ijumaa Kuu ya 2017, Rais Magufuli alikuwepo nchini. Hata hivyo, hakuhudhuria mazishi ya askari polisi hao, badala yake aliyeonekana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba.

4. Mara wakauawa wanajeshi wetu wa kikosi cha kulinda amani nchi DR Congo mwezi December 2017. Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hakuonekana Uwanja wa Taifa kwenye mazishi ya wanajeshi wetu. Aliyekwenda kwa niaba ya Serikali ni Waziri Mkuu Majaliwa.

5. Sasa wamekufa zaidi ya watu 200 kwenye Janga la MV Nyerere. Rais wetu badala ya kwenda kwenye mazishi, amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa ili yeye apate wasaa wa kunywa chai Ikulu na mapolisi wa usalama barabarani!!!

Rais wetu una shida gani na misiba hii ya kitaifa???
 
Msituchanganye

Kwa hiyo waliokuwa wanaenda misibani waliagizwa na waganga. Sasa tuna wasiokwenda, nao wameagizwa na waganga!

Kwangu mimi perspective ingekuwa ni suala la rais kufuata presidential tradition aliyoikuta. Nayo ni:
Wakati wa maafa ya MV Bukoba - Rais Mkapa mwenyewe bila kuwakilishwa alienda Bukoba uwanja wa mashujaa kuwapa pole wananchi
Wakati wa maafa ya meli MV Islander na Skagit - Rais Kikwete alienda maombolezo na kuwapa pole waliofikwa na maafa hayo
Wakati wa maafa ya mabomu ya Mbagala, Rais Kikwete alishiriki kila hatua ya maombolezo

Rais huapa kufuata katiba, sharia, kanuni na MAPOKEO (TRADITION) mbalimbali za urais.
Pia Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu na MFARIJI MKUU (Chief Comforter). Wajibu huu huwa haukasimishwi. Ndo maana rais hawezi kumtuma Makamu au Waziri Mkuu kuwapa Kamisheni maaskari wanaomaliza mafunzo. Rais asiwakilishwe kuwafariji watanzania.
-
 
Kuna kajibwa kamoja cha jirani yetu anabweka hatari lakini muoga balaa. Kuna watu wana kauli mbaya majukwaani lakini wanaogopa kufa hatareee, sasa uoga wao hukimbia mpaka kufika kwenye misiba😄😄.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Msituchanganye

Kwa hiyo waliokuwa wanaenda misibani waliagizwa na waganga. Sasa tuna wasiokwenda, nao wameagizwa na waganga!

Kwangu mimi perspective ingekuwa ni suala la rais kufuata presidential tradition aliyoikuta. Nayo ni:
Wakati wa maafa ya MV Bukoba - Rais Mkapa mwenyewe bila kuwakilishwa alienda Bukoba uwanja wa mashujaa kuwapa pole wananchi
Wakati wa maafa ya meli MV Islander na Skagit - Rais Kikwete alienda maombolezo na kuwapa pole waliofikwa na maafa hayo
Wakati wa maafa ya mabomu ya Mbagala, Rais Kikwete alishiriki kila hatua ya maombolezo

Rais huapa kufuata katiba, sharia, kanuni na MAPOKEO (TRADITION) mbalimbali za urais.
Pia Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu na MFARIJI MKUU (Chief Comforter). Wajibu huu huwa haukasimishwi. Ndo maana rais hawezi kumtuma Makamu au Waziri Mkuu kuwapa Kamisheni maaskari wanaomaliza mafunzo. Rais asiwakilishwe kuwafariji watanzania.
-
Msome vizuri Tundu Lissu utamwelewa
 
..wananchi 180+ wamekufa halafu Raisi hajitokezi eneo la maafa?!

..kwa tukio hili la MV Nyerere naamini Raisi, Makamu wa Raisi, na Waziri Mkuu, wote walipaswa kushiriki ktk kuwaaga marehemu wetu.

Umeshaambiwa, mzee baba alikuwa anakunywa chai mjengoni na trafiki. Mengine mtajiju!!! Ila rambirambi atazipangia shughuli mbadala za kitaifa. Huyu bwana fedha wa taifa ni mahiri sana.
 
WAFALME HUWA HAWARUHUSIWI KWENDA KWENYE MISIBA, hiyo ni sheria ya zamani, mbona CHAMA CHAKO HAKIJNA MTU ALIYE KUJA KUKUONA? Una matatizo gani? Awamu hazifanani walahi!
Kaa kimya kula painkillers get high ndio mchezo mzima walahi tundulissimsaliti!
 
..wananchi 180+ wamekufa halafu Raisi hajitokezi eneo la maafa?!

..kwa tukio hili la MV Nyerere naamini Raisi, Makamu wa Raisi, na Waziri Mkuu, wote walipaswa kushiriki ktk kuwaaga marehemu wetu.
Mkuu acha kusema +++ ni wananchi 227 mpaka sasa. Hao ni wengi mno pengine Rais wetu angeonyesha ushiriki usingeshangaa hata Kenyatta angesema naenda Mwanza kuhudhuria mazishi ya RAIA wengi was East Africa huko Tanzania.
Ajabu ni kuwa huyu mtu wakati ule ambao hakuwa na mandate ya kusafiri nje mpaka aombe ruhusa aliwahi kusafiri kwenda Kenya mazishi ya mtoto was Raila. Jee msiba wa mtoto was Raila ni mzito kuliko RAIA wako 220 na zaidi ? Hili anapaswa kujitokeza kujibu
 
Back
Top Bottom