Tundu Lissu: Rais Magufuli ana shida gani na misiba mikubwa?

Another useless contribution. Wakati anauliza hayo, nasi tunajiuliza kama kichwa chake kiko sawa. Kelele tangu mitaani hadi Hospitali!! Huyo mke ana taabu. Rais Kikwete alidhihakiwa hakosi misibani. Na kweli alikwenda hadi misiba ya akina Kanumba na ubani wa mamilioni. Sasa tena kuna kiumbe anataka Rais aende misibani. Ni jukumu la rais au ni gesture ndo inayotakiwa?

Hivi Mwanahabari Huru, nawe unaamini Tundu Lissu ni kisima cha busara? Sielewi kwa nini kila wakati unaleta maelezo ya Tundu Lissu utadhani ni bonge la mtu reasonable. Nawe unamuona ni mtu wa kufanyia reference? Au ni mmoja wa wale vichaa wanaotumwa kutukana watu? Pole pole kishakuwa zilipendwa.
Sasa kwani kuwa kiongozi wa nchi ndio kuwa na busara? ?.. mbona hana?.. Lissu umrank na Chizi huyo kwa lipi au PHD-korosho.
 
Naomba na hili la maafa nilizungumzie kidogo kabla halijazikwa na maajabu mengine ya nchi yetu.

Nadhani Mheshimiwa Rais wetu ana tatizo kubwa na misiba ya kitaifa ambalo wanaofahamu zaidi wanabidi watueleze.

1. Walipokufa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Arusha mwezi Mei 2017, Rais Magufuli hakuhudhuria mazishi yale, ijapokuwa alikuwepo nchini. Serikali ikawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

2. Walipokufa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi mwezi September 2016, Rais Magufuli, aliyekuwa asafiri kwenda Zambia, aliahirisha safari hiyo lakini hakuonekana kwenye mazishi ya wahanga hao. Serikali ikawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

3. Walipouawa askari polisi 7 kule Kibiti Ijumaa Kuu ya 2017, Rais Magufuli alikuwepo nchini. Hata hivyo, hakuhudhuria mazishi ya askari polisi hao, badala yake aliyeonekana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba.

4. Mara wakauawa wanajeshi wetu wa kikosi cha kulinda amani nchi DR Congo mwezi December 2017. Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hakuonekana Uwanja wa Taifa kwenye mazishi ya wanajeshi wetu. Aliyekwenda kwa niaba ya Serikali ni Waziri Mkuu Majaliwa.

5. Sasa wamekufa zaidi ya watu 200 kwenye Janga la MV Nyerere. Rais wetu badala ya kwenda kwenye mazishi, amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa ili yeye apate wasaa wa kunywa chai Ikulu na mapolisi wa usalama barabarani!!!

Rais wetu una shida gani na misiba hii ya kitaifa???

Wewe jamaa ni mchawi uliwezaje kuona mazishi yaliyofanyika katika uwanja wa taifa
 
Kwa hiyo unasemaje???!!! Cheap politics...Unahoji ili iwe nini??? Wewe unayehoji ulikwenda misiba mingapi?? Rais ni taasisi, kumbukeni hivyo.....Hamna jema nyie...Akiamua kwenda mtakuja sema anajipendekeza na kutafuta umaarufu...Kutokwenda kwenye msiba haina maana hana uchungu...wewe zingatia kinachofanywa na serikali anayoiongoza....
 
Msituchanganye

Kwa hiyo waliokuwa wanaenda misibani waliagizwa na waganga. Sasa tuna wasiokwenda, nao wameagizwa na waganga!

Kwangu mimi perspective ingekuwa ni suala la rais kufuata presidential tradition aliyoikuta. Nayo ni:
Wakati wa maafa ya MV Bukoba - Rais Mkapa mwenyewe bila kuwakilishwa alienda Bukoba uwanja wa mashujaa kuwapa pole wananchi
Wakati wa maafa ya meli MV Islander na Skagit - Rais Kikwete alienda maombolezo na kuwapa pole waliofikwa na maafa hayo
Wakati wa maafa ya mabomu ya Mbagala, Rais Kikwete alishiriki kila hatua ya maombolezo

Rais huapa kufuata katiba, sharia, kanuni na MAPOKEO (TRADITION) mbalimbali za urais.
Pia Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu na MFARIJI MKUU (Chief Comforter). Wajibu huu huwa haukasimishwi. Ndo maana rais hawezi kumtuma Makamu au Waziri Mkuu kuwapa Kamisheni maaskari wanaomaliza mafunzo. Rais asiwakilishwe kuwafariji watanzania.
-
Kila RAIS anakuja na Flavor yake. Tuache kucremu.
Kuna waliohudhuria kila msiba mpaka tukawakejeli
Kuna waliotumia muda mwingi angani kuliko ardhini hadi tukawapa majina.
Sasa kaja anayetumia muda mwingi ardhini kuliko angani na asiyehudhuria kila msiba pia tunaona sio sawa. Mapokeo hapo ni yapi sasa?
 
Hatujibishani na wagonjwa

Kama rais huwa hahudhurii kwenye misiba kwa sababu za ushirikina, kwa hili Lissu aliloongea aidha itabidi aende akutane na balaa la hayo maagano, au aendelee kutokwenda kisha ajijengee taswira hasi kwa wananchi. Huwa anajinasibu kwamba hapangiwi, ila kwenye hili limekaa vibaya.
 
Kila RAIS anakuja na Flavor yake. Tuache kucremu.
Kuna waliohudhuria kila msiba mpaka tukawakejeli
Kuna waliotumia muda mwingi angani kuliko ardhini hadi tukawapa majina.
Sasa kaja anayetumia muda mwingi ardhini kuliko angani na asiyehudhuria kila msiba pia tunaona sio sawa. Mapokeo hapo ni yapi sasa?

Ukiambiwa chakula kina chumvi nyingi, kuonyesha umesikia hizo lawama ni kutokuweka kabisa? Kila jambo lifanyike kwa kiwango sio kuzidisha au kutukufanya kabisa.
 
Il
Amir Jeshi mkuu anatakiwa kuwaongoza raia kwenye matukio haya lakini ajabu Amir Jesh wetu mkuu anatuongoza kufungua madaraja, fly overs hata viwanda vya pipi lakini si misiba na maafa.
ile dhana ya The chief confortor haijamfikia
 
Something is wrong somewhere! Na watu wala hawashtuki and they dont care! Ila amin nawaambieni ingekuwa ni nchi zilizoendelea hilo tuu linatosha kumtoa madarakani.
 
Something is wrong somewhere! Na watu wala hawashtuki and they dont care! Ila amin nawaambieni ingekuwa ni nchi zilizoendelea hilo tuu linatosha kumtoa madarakani.
Kuanzia wanajeshi waliofia DRC Congo, wanafunzi wa Lucky Vincent hata wahanga wa MV Nyerere jamani where is our Chief Comforter?
 
Angeenda kwenye hiyo misiba Lissu asingekosa la kusema! Usiombe ukawa na ulimi unaowaka! By they way, Magufuli hakudhuria misiba (kwa hiyo hafai), mbadala wake ni nani (Mbowe)? Vipi naye amehudhudhuria msiba wa Ukerewe?
Suala la Rais kutoshiriki misiba mikubwa siyo suala la UKAWA, Mbowe au Lisu. Ni kitu kinachotushangaza wengi.

Lisu amepata tu ujasiri wa kunena lakini limesemwa na wengi, hata wana-CCM kindakinda.

Kwa kutohudhuria misiba yote mikubwa, hajafanya jinai wala hajakiuka katiba lakini kuna walakini katika busara ya uongozi. Sisi tunaoamini katika Ukristo, Biblia inasema,

'Mfalme awe kama jabali litoalo kivuli kwenye jangwa; na awe kama kijito kinachotiririsha maji kwenye ardhi kame'. Kiufupi Mfalme anastahili kuwa mfariji mkuu wa watu wake. Bila shaka hata kwa Waislam, naamini kutakuwa na aya zinazofanana na hizi za kwenye Biblia.

Kama kuna anayefahamu sababu zozote zile za Rais kutoshiriki kwenye majanga makubwa ya vifo, atueleze kuliko kupuuza hoja ya Lisu, maana hakuna Rais yeyote tumjuaye aliyewahi kufanya kama afanyavyo wa kwetu yatokeapo majanga makubwa.
 
Kwa hiyo unasemaje???!!! Cheap politics...Unahoji ili iwe nini??? Wewe unayehoji ulikwenda misiba mingapi?? Rais ni taasisi, kumbukeni hivyo.....Hamna jema nyie...Akiamua kwenda mtakuja sema anajipendekeza na kutafuta umaarufu...Kutokwenda kwenye msiba haina maana hana uchungu...wewe zingatia kinachofanywa na serikali anayoiongoza....
Acha kuchanganya mambo! Rais ni mtu na kwa sasa ni Magufuli! Urais wake hauna ubia na mtu ye yote kwa taarifa yako!! Ndiyo maana anatamba kuwa hapangiwi!!!
 
Acha kuchanganya mambo! Rais ni mtu na kwa sasa ni Magufuli! Urais wake hauna ubia na mtu ye yote kwa taarifa yako!! Ndiyo maana anatamba kuwa hapangiwi!!!

Kwa hiyo unasemaje Ndugu yangu???!!!
 
Back
Top Bottom