KUNA VITU KADHAA BADO VINANITATIZA
1. Kuhusu serikali kutomtembelea Lissu hapo awali.
Sasa tufanye nyumba ya jirani mtoto wao anaumwa sana. Wazazi wa mtoto wamepiga ramli na kuambiwa kuwa bibi kizee jirani yao ndie mchawi aliemroga mtoto.
Taarifa zimezagaa kijiji kizima na yule bibi amezisikia.
Hivi mnaweza kugeuka na kumlaumu yule bibi kizee eti kwa nini hajaenda kumjulia hali mgonjwa au hajampelekea hata uji tu?
2. Kuhusu polisi wa Tanzania kumhoji Lissu akiwa Kenya.
Lissu sio mshukiwa wa shambulio lake yeye mwenyewe. Kwanini awe mbishi kuhojiwa na polisi wa kitanzania popote pale duniani?
Fikiria:
Wezi wamevunja nyumba yako, wakakufunga kamba, wakaiba kilakitu wakati unawaangalia.
Wakati upo London kwa shughuli zako binafsi polisi wa Tanzania wakakuomba waje wakuhoji ili wapate maelezo yako kuhusu wezi wako pamoja na mali zako zilizoibwa.
Hivi utakataa kukutana nao na badala yake utataka uhojiwe na MI5 au Scotland Yard wa Uingereza?
Uhalifu ufanyike Tanzania, wewe ndio shahidi (eye witness) mkuu, lakini unataka uhojiwe na polisi wa nchi ya kigeni?
Makubwa haya.