Tundu Lissu ni mshindi

Tundu Lissu ni mshindi

Nabii Musa alikimbia Kutoka Misri kwenda nchi ya Midian, kisa na mkasa alikimbia mkono wa Farao baada ya kumuua mmisri akiwa anamtetea muisrael mwenzake. Baadaye alirudi kuwakomboa waisrael.
Kisa hiki cha Mussa nimekisoma leo asubuhi Kutoka 1: 10-25
 
Kuna mtu jana tu kashindwa. Amelala juu ya udongo.
Kifo ni kitu ambacho kila mtu lazima akipitie hata manabii wa Mungu wamekipitia ila shetani yupo hadi leo,je tutasema shetani ni mshindi? Binafsi huwa nashangaa sana pale mtu anapofurahia kifo cha mwengine wakati anajua hata yeye lazima atapitia huko na hali hajui atakufa kwa hali gani,sidhani kama kifo cha mtu mwengine ni ushindi.
 
Lissu amekamatwa na polisi mara nyingi zaidi kuliko mtanzania mwingine yeyote. Kila alipopelekwa mahakamani hajawahi kukutwa na hatia. Sio Rushwa, uzinzi, wizi, ufisadi, ujambazi hata ule wimbo wa ccm wa uchochezi hajawahi kukutwa nayo.
Leteni ushahidi badala ya hisia na umbea. Kwani Lissu ni malaika? Vinginevyo tunachoweza kufanya ni kuwapuuza.
 
Huwa nacomment post kadhaa huku jf nikiwaambia UOVU HAUSHINDI.
NIkweli uovu haushindi.
 
Umesahau na sifa ya kutetea "ushoga!"

Sasa sijui Mungu gani atakuwa na mtu anayetetea ushoga!

Nawaza kwa sauti!
 
Umeongea kwa hekima kuu ambayo kama watawala wanapitia huku kwa GT na wakayaelewa haya uliyowanenea Tanzania ingebarikiwa Sana.Mh.SSH ambaye ndiye Rais wetu wa VI akajinyenyekeze mbele za Mungu na kujishusha ili amrejeshe nyumbani Mh.Lissu na wenzake ili nao washiriki kuijenga Tanzania Mpya.

Tunahitaji kuijenga nchi yetu na hivyo tunahitaji raslimali zote ikiwemo watu,Mali asili kama ardhi,Maji,madini na vivutio vyetu tulivyopewa na Mungu vitumike kwa faida ya wote.
Mh.SSH tunakuomba utuwezeshe kuandika Katiba Mpya ya Wananchi ili Watanzania wajitawale na kujiendeleza kifursa kila moja kwa vipawa alivyopewa na Muumba kwa faida ya Taifa letu.

Tanzania Mpya haistahili kuwa nchi ya uchumi wa chini,kati chini wala kati juu Bali nchi ya uchumi mkubwa(Nchi ya dunia ya kwanza) endapo itatumia vema raslimali zake kwa hata nusu ya vilivyopo.Tusiidumaze nchi kwa tamaa za wachache katika mwavuli wa vyama vya siasa.Nchi hii ni yetu sote.
 
Mshindi Bora m Yule anayepambania maslahi ya nchi yake na Yuko tayari age Kwa sababu ya wengi,

Kwenye hao wawili, JPM ni mshindi

Ukimwona Lissu umuulize Kwa nini ni yeye tu alipigwa lisasi na si mwingine?? Au ndio wale waliokuwa vikwazo Kwa nchi??

Kwa nini kabla ya tukio kulikuwa na kuwatia hofu viongozi eti Kwa mradi Fulani mwaweza Fanya, Ila huu msifanye Kwa sababu mtashitakiwa na mara sjui Miga

Lakini hakuna cha Miga Wala nini, Je nikweli labda alikuwa miongoni mwa waliokuwa upande wa manyonyaji na mabeberu?? Mbona hatukushitakiwa na angalau nchi INA shere na mabeberu kwenye migodi!!

Kwa nini ni yeye tu?
Mtapamba sana ila naamini hakuna binadam mkamilifu na hakuna binadam asiyekubali kukosolewa
 
Ombea adui yao aishi miaka mingi, ili utakapo barikia ajionee kwa macho.amna hata kabisa afe kabla hajaona baraka zake mungu ameweka mbele yako.

Lissu sio mshindi ilibidi anaesemekana kuwa adui yake aishi miaka mingi aone mafanikio ya lissu.
Je lissu akifanikiwa kweli nani ataona sasa?


Huwa inategemea na Mungu apendavyo yeye zaidi.

Je adui ni nani? Je ni Mtesi?

Wengine hata hawaja qualify kuitwa adui huwa tunawachukulia kuwa kama adui kimakosa sababu ya kukosa Ufahamu wa kutosha kuhusu mahusiano na Neno la Mungu ndani yetu.
 
Lissu ameshinda nini hadi anakimbia nchi? Ameifanyia nini Tanzania zaidi ya kuichafua? Tuwe serious kidogo. Mwandishi wa makala hiyo ni Lissu au kuwadi wake. Sasa anafurahi Magufuli amekufa. Je itamuongezea nini. Natamani arejee nchini aone atakavyopokelewa. Inawezekana waliompiga risasi ni waliokuwa wakijipendekeza kwa Magufuli au hata maadui zake wengine ambao hawana uhusiano na serikali. Wapo wanaosema ni Bashite. Siku moja tutajua ukweli na utatuweka huru.
Uchunguzi huru ungefanyika tufahamu mbichi na mbivu.Nani alimshambulia Mh.Lissu kwa mvua ya risasi mchana kweupe?Kwa nini hakuna upelelezi uliofanyika?Utetezi wenu wa kusema Mh.Lissu ni muumini wa ushoga hautoshi na hakuna ukweli maana ni mambo ya kufikirika.Jiulize hapa nchini kuna mashoga?Lissu ndiyo anawezesha uwepo wao au ni Tabia za binadamu kwa hiari yao wameamua kuwa mashoga/mabasha?Je,serikali imefanya nini kuwaangamiza?Kumsingizia Mh.Lissu kwa masuala ya ushoga ni upungufu wa kufikiri ama upotoshaji wa hoja za msingi.
Pia tatizo hilo hata kama lipo siyo kikwazo kwa maendeleo ya Watanzania walio wengi,tatizo letu ni Sera mbovu zinazowekwa na watawala wabinafsi wanaotumia ubovu wa Katiba iliyopo kuhujumu nchi yetu.Wanaingia mikataba ya kinyonyaji na mabeberu halafu wanajitungia sheria za kuwalinda wasishtakiwe popote duniani.Unategemea tunyamaze?
 
Huyu Mwingira ni mtumishi wa Mungu??? La hawla wala quwwata illa billah!!!!
Unamuona si mtumishi kisa amemuongelea Lissu.
Ulitaka amuongelee St Meko ndio ungemuelewa👉👧wewe
 
Umesahau na sifa ya kutetea "ushoga!"

Sasa sijui Mungu gani atakuwa na mtu anayetetea ushoga!

Nawaza kwa sauti!
Watu wanashindwa kuona kuwa Lissu hayupo sawa anahitaji msaada,wao wanamsifia tu vile anavyobwatuka.
 
Umesahau na sifa ya kutetea "ushoga!"

Sasa sijui Mungu gani atakuwa na mtu anayetetea ushoga!

Nawaza kwa sauti!
Ushoga ulianzia huku...
Lesbian, gay, bisexual, and transgender (LGBT) rights in Israel are considered the most developed in the Middle East.[1]Although same-sex sexual activity was legalized in 1988, the former law against sodomy had not been enforced since a court decision in 1963. Israel became the first country in Asia to recognize unregistered cohabitation between same-sex couples, making it the first country in Asia to recognize same-sex unions in any capacity. Although same-sex marriages are not performed in the country, Israel recognizes same-sex marriages performed elsewhere
 
Sawa basi ufanyike uchunguzi tujue nani alishambulia lissu. Binafsi naamini kila mtu yuko sahihi sasa serikali iruhusu uchunguzi huru na yenyewe ishiriki tuone..serkali wakikubali dhambi hio sio yao wakikataa hilo halikwepeki nyote mnaopinga ni interest zenu
 
Back
Top Bottom