Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Narudi kama Mwananchi huru tarehe 27 Julai 2020, Serikali inipe Ulinzi. Kesi zangu 6 zina dhamana, sitakamatwa

Uzuri bado kuna makamanda wenye akili zao bado.
 

Attachments

Hiyo safari anatokea mbinguni.....maana story nyingi mwisho wa siku atasema anaahirisha kwa sababu cdf hajamuhakikishia usalama wake.

Lisu ni mtata mtata sana.
CDF kote huko?
Kipindi kile MUSIBA tu alimuonya awe makini asithubutu kupanda gari la CHADEMA akaahirisha safari.
 
Kama kawaida, ratiba itasogezwa mbele atasema anakuja mwezi wa 9 kampeni zikiwa zinakaribia kuanza..
 
Serikali,ama kwa kutumia, Polisi, Mahakama,ama Tume ya Uchaguzi ama wanaCCM ama wasiojulikana,

Wataanza kumbuguzi,na ninategemea watambugudhi ili asichukue fomu Wala asitulie na ikiwezekana hata kumfunga kabisa.

Haya kama yakitokea, yatakua makosa makubwa Sana ya kiufundi na yataigharimu CCM na Taifa kitaifa na kimataifa.

Wakijichanganya tu,

Watakua wanamtangaza zaidi hasa kwa watu na mataifa yaliyokua hayafuatilii habari zake,kumbukA Kuna Mabalozi wa nchi nyingi hapa.kuna wananchi hapa.

Vyombo vya habari vyote vikubwa vitaripoti matukio haya,

Watu watamuonea huruma,

Jumuiya ya Kimataifa itapiga kelele,

Vyombo vya Haki vya Kimataifa. Vitapiga kelele,

Mwisho wa siku wataamua kumwacha na kumpa Haki yake ya kugombea,
matokeo yake watakua wamempigia kampeni wao wenyewe,na mwisho wa siku watu watampigia kura za huruma kwa mamilioni,

Jumuiya ya Kimataifa itataka kuona uhesabuji wa kura na kutangazwa matokeo unakua wa Haki.

Kwa muktadha huo Ushindi kwa Lissu utakua umechangiwa na Vyombo vya Dola.

Kumeza ngumu kutema ngumu.

Wasipombugudhi maana yake watu kwa maelfu watataka kwenda kumpokea,kumsikiliza na kumshangilia,habari zake zitazambaa kwa kasi ya ajabu,

Mwisho wa siku atachukua fomu.

Tundu Lissu Ni fundi wa kuongea,kujenga hoja,kujibu hoja na anauwezo wa kuvumilia madongo,kumbukA huyu Ni mwanasheria na wakili mzoefu.

Tutasikia mengi.
 
Umesema na kuona vema ndugu yangu... na maneno yako yatimie... either way- lazima awajambishe tu- iwe ccm, vyombo vya dola na wengineo... jina la aliye muokoa katika shambulio lile ni kubwa kuliko majina yote.
 
Hii kitaalamu tunasema "ukikimbia nchale, ukisimama McHale"
 
Kwahiyo risasi 40 walikuwa wanatania. We ni fala.
 

Mkuu, hauna Link ?
 
Lissu kama unarudi rudi acha mbwembwe nyingi CD isije ikascratch. Kuna wakati ukiamua kweli na nia ya dhati unayo kukomboa watu inabidi uache uoga kabisa na ukubali kila kitu ( wanaomfahamu mwanamapinduzi Che-guevara wanaelewa hili).. Mh Lissu kiukweli watu wanasubiri ukio wako kwa hamu lakini jaribu kuwa realistic na kama kweli umeamua na una nia ya kugombea kupitia CDM..

Mpaka sasa upinzani kama kweli mnataka Urais na Ubunge mko nje ya muda mpaka sasa, kinachotakiwa ni kuanzisha mapambano kwa nguvu now now kuliko hizi sinema, CCM haiwezi kutoka kirahisi kama mnavyofikiri na inahitaji watu kujitoa kweli na kuacha kutegemea vijana mbogamboga..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…