Tundu Lissu nae!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu nae!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Feb 9, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.

  Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.

  Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.

  Ni ushauri tu lakini
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hii sred imezeeka naomba uchungulie sio kukurupuka na kurudia sred za leoleo. Au ndio kwanza umeamka na uzanduzandu manake labda jana umekosa usingizi ukiwaza namna spika anavyonyonga demokrasia
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Tundu Lisu ni mashuhuri hata kabla ya kuwa mbunge,jina keshajenga siku nyingi sana wala hataki hilo leo.Hiyo advice yako peleka chooni kawaambie inzi sio watu wenye akili.Huwezi kuissue summons kwa mbunge aliyeko bungeni hiki ni kituko ni kinyume cha katiba

  Fikiria kabla hujasema
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata kama ni ushauri tu, umemwona kuwa mwenzio amekurupuka lakini mbona wewe unayemlaumu na wewe umekurupuka? tuambie kanuni ambayo wewe unadhani amekiuka na vile vile tuambie kama hilo unalolisema mwenyewe umelifanyia utafiti.
   
 5. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Saini yako nimeipenda sana. Inaongelea mtu mwenye busara. Kama wewe ni mfano wa mtu mwenye busara twafaaa!! Ni msiba katika nchi yetu.

  Kama mtu mwenye busara"kama wewe" anatumia maneno ya namna hiyo hadharani, sijui!! Anyway, ni kweli ku-issue summons ni kituko, lakini kutaka bunge liahirishwe kwa kuwa mbunge kapewa summons ni kituko kikubwa katika karne hii na ninahisi bado vituko vitaendelea kuonekana kama tunatafuta umaarufu kwa nguvu
   
 6. c

  cray Senior Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo wewe unaona ni kawaida tu, yaani mbunge yuko kwenye kikao, afu anapewa sumons afu akae kimya, spika alitakiwa kuwa na busara, kwakumwambia kwasababu uko kwenye kudiscuss sensitive issue, basi naahirisha mjadala. Wana JF sisiem ni wajanja sana, walijua bila kumwondoa kwenye mood Mh. Lissu ingekua balaa, kwahiyo ni hila za kimakusudi zilifanywa na sisiem kumdhoofisha Lissu. Lakini pamoja na hilo kama mwanasheria aliebobea bado aliendelea kujaribu kupambana. katika mapambano silaha yoyote ile unaitumia hata kama ni fimbo, jiwe au tawi la mti.
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo kuku anzaaa yai au yai linazaa kuku??kati ya summons na kuomba muongozo wa spika nini kilianza??

  unaudhi
  unakera
  unaleta hasira
  nyambafuuuuuu

  hizi ndizo busara zangu zakwako zikowapi??wewe
   
 8. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hii thread haipo, labda wewe ndo umeangalia vibaya. Inawezekana ikawepo threaad inayomhusu Mhe Lissu lakini ina maudhui tofauti na haya katika thread yangu. Pitia vema
   
 9. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
   
 10. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hata mie ambaye ni kilaza nilishangaa sana. Nafikiri ana haraka au tuseme usongo sana, sijui nasubiri.
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Alichofanya ni sawa kabisa, kwani waliom-summon walifanya hivyo makusudi ili kum-disturb. We ulitegemea afanye nini?
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jamani hapa hoja hujibiwa kwa hoja, matusi na kashfa si sehemu ya kujenga hoja, kama huna la kuchangia nibora uipotezee thread kuliko kuongea ushabiki na upenzi kama wa simba na yanga.

  Kama sijakose hii ni mara ya nne sasa toka siku ya bunge la kwanza kumona lisu akiomba muongozo kwa jazba na kukurupuka na mara zote mama makinda amekuwa anambeat vibaya kwa kuonyesha hajui anachoomba.
  mfano jana amepewa samansi kimakosa wakati bunge linaendelea lakini kama msomi wa sheria angeatafakari kwanza namna ya kuhandle issue ile na si kukurupuka na kuanza kuomba eti dharura, na alipotakiwa asome kifungu alichemka kwanza akaambiwa kaa chini soma jipange tena, na hata baada ya kujipanga akasoma kifungu ambacho aliulizwa je kinafit kwa unavyoomba, akabaki ametoa macho.

  Wito bado mapema mno atulie, au achukue mifano ya wenzake zito na dr walivyofanya
   
 13. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Shida ya humu ndani ni ushabiki tuu, hawana ushauri kabisa kwa hao wanaowashabikia, huo si urafiki maana rafiki ni yule anayekushauri na kukuaripia kwa mabaya uyafanyayo.
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Umakini wa Tundu Lissu is Questionable... Niambieni tangu aanze kukurupuka kutukana nini tangible alifanya? Akina Slaa akina Zitto, Akina Kafulila wanavyo yeye kipi? Naomba msaada?
   
 15. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Lissu kuna chance kubwa akawa kituko Bungeni. Ni mpayukaji na itamcost.. Lazima ajifunze haraka, aonyeshe utulivu na atoe hoja za nguvu.. Ateme cheche bila kukurupuka.. Mtu una LLM unakuwa na hoja za watoto wa primary wanaocheza 'rede'
   
 16. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  nakibaliana na wewe kidogo lakini tunatofautiana pia,ccm walifanya kusudi na ule ni umafia,..walichotaka wao ni kumtoa kwenye mood ili asiwashambulie kwa uhuni wao na yeye alistukia hilo akaamua kuwachana live kwenye tv kwamba kastukia...you need to be alert all the time for these monsters are up to no good,..if someone gives you pepper dont give them sugar
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Son of soil, wabunge wana immunity ya kutoshiakiwa kwa mambo tuu waliyayazungumza ndani ya bunge. Nje ya bunge, nao ni kama raia wengine, sawa na mimi na wewe hivyo mahakama has the right kutoa summon kwa mbunge wakati wowote, ila aliyepewa summon, alitakiwa amsubiri nje baada ya bunge kuahirishwa ndipo kumsainisha. Kitendo cha kumletea summon asaini ndani ya bunge, ni kulidharau bunge lakini sio sababu ya kuiahirisha kwa sababu hiyo.

  Mahakama ni moja ya mihimili mitatu ya dola hivyo inafanya kazi zake independently of bunge na serikali. Hivyo wanaweza kutoa samansi kwa yoyote siku yoyote na saa yoyote isipokuwa kwa maofisa tuu wenye kinga ya kutoshitakiwa inayoahusu viongozi wakuu na wale wenye kinga za kibalozi, diplomatic immunity.

  Hata hivyo mahakama inaheshimu uwepo waikao vya bunge, hivyo wakati wa vikao vya bunge, hukubali kuziahirisha kesi zote zinazowahusu wabunge ili kuwapa fursa kuhudhuria vikao hivyo kwa heshima tuu na sio kwa mujibu wa sheria, taratibu au kanuni.
   
 18. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  wewe unazijua kanuni za bunge na katiba vizuri? unafahamu mbunge hatakiwi kupewa soumance wala kuingiliwa na muhimili wowote. naona wewe ndio umekurupuka kuandika, T.Lissu yupo sahihi ndg yangu
   
 19. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mwanzoni nilidhani labda Mhe Lissu angekuwa mbadala wa Dr pale bungeni. Lakini kwa sasa nadhani nilikosea na dhana zangu hazikuwa sawa.
   
 20. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hakuna mbadala wa mtu hapa, kila mtu ana strength zake na weaknesses zake.., hatuwezi wote tukawa sawa.., hapa ni percentage kama akitoa issue 100 akachemka 10 that is 90% success na atakuwa kafanya bora kuliwa wale viti maalumu wa CCM wote ambao wanatumia bunge kama mapumziko, na sehemu ya kwenda kuchukua posho.
   
Loading...