Tundu Lissu nae!!

Tundu Lissu nae!!

Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.

Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.

Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.

Ni ushauri tu lakini

....na wewe sasa ni mnafiki!!! hivi hili jambo si tulishalijadili na hii thread si tulishaichangia????
au wamekutuma tena??? alafu you pretent kuwa mstaarabu wa maandishi wakati
there is no logic behind what you write!!! ACHA UNAFIKI!
 
Hata mie ambaye ni kilaza nilishangaa sana. Nafikiri ana haraka au tuseme usongo sana, sijui nasubiri.






kumbe na wewe ni kilaza kama huyo mwenzako aliyetuma hyo thread inayomhusu lisi? bas itabid mtafute forum nyingine kwa ajili ya vilaza kama nyie ndo mtume thread zenu za vlaza..... mmenisoma?
 
Kwenye BUNGE hili la leo unamshangaa Mh. Lissu ........ameamua naye ajifurahishe kwa kupunguza presha maana amechoka kila siku yuko serious wakati Bunge lote kuanzia speaker wake wanacheza makida makida.................Bravo Lissu ameamua kupunguza hasira za wabunge wengine wanaokerwa na majibu ya hovyo na kero ya Speaker
 
Watanzania tuna upeo mdogo sana wa kutafsiri mambo. Tunatafsiri mambo mengi kwa vey narrow premises.Mtu akihoji mamlaka makubwa ya kikatiba ya Rais ya kuteua watu wengi kwenye nafasi tofauti za uongozi anaambiwa anahoji mamlaka ya JK wakati urais ni taasisi ya kushikwa na mtanzania yeyote mwenye sifa kwa nyakati tofauti chini ya katiba ile ile.

Hoja ya Mheshimiwa Tindu Lissu ilikuwa kuhoji kitendo cha hadhi na mamlaka ya Bunge kuingiliwa na mtu kutoka nje ambaye ni wa mhimili mwingine wa dola. Hoja hii ina uzito wa kulifanya Bunge lihalalishwe kuahirisha kujadili hoja iliyopo na kujiadili hoja hiyo ya kulirudishia Bunge heshima yake.

Kuna wajinga wame-construe hoja hiyo very narrowly kwamba inamhusu Mheshimiwa Tindu Lissu personally wakati inaihusu taasisi nzima ya Bunge. Kwa bahati mbaya sana miongoni mwa wajinga hao ni kiongozi mwenywe mkuu wa taasisi iliyodharauliwa, yaani Spika wa Bunge! Kwa mwendo huu Watanzania tunahitaji elimu bora kwani tuko dull kichizi.

Swali la kujiuliza: kama aliyeuliza angekuwa siyo Tundu Lissu bali ni mbunge fulani wa CCM, Spika ange-react vilevile? Hoja ya kwamba taasisi ya bunge iko at stake ni ya msingi. Tatizo ni kwamba Anna yuko so busy kutekeleza agizo la kuwadhibiti wapinzani, kiasi kwamba hawezi kuona a few metres ahead. ni sawa na bosi anayeletewa mapendekezo ya kuongeza malipo ya pensheni anayakataa, bila kukumbuka kuwa miaka michache ijayo na yeye pia atakuwa analalamikia pensheni hiyohiyo. kwa staili ya Anna, atajikuta anajipinga mwenyewe. maana tatizo kama hilo likijatokea kwa mtu wa CCM, itabidi aendeleze precedency ileile. Au Anna ni single minded, a one-track mind ambayo haiwezi hata kuangalia pembeni kulia na kushoto?

Angalau hili la Pinda kusema uwongo bungeni litakuwa limemstua, kama kweli ni wa kustuka. maana hasira za mkizi... My take ni kwamba Tundu Lissu anaweza kujifunza haraka zaidi na kuji-align vyema kuliko ambavyo Anna anaweza kuadapt na kuwa naye wa viwango. maana alisema yeye ni wa kanuni, na tunaona kanuni zinampiga chenga
 
Back
Top Bottom