Tundu Lissu na Aboud Jumbe

Tundu Lissu na Aboud Jumbe

Hivi huyo mheshimiwa si bado yuko hai,kwa nini hapewi fursa ya kuelezea mtazamo wake hadharani?Ningejisikia faraja siku moja akihojiwa na wanahabari juu ya kilichotokea hata akapewa "life ban".

nahisi na hilo la kuzungumza pia ni kizuwizi alichopewa maana mzee yuko kimya baada kutoa kitabu chake hasikiki tena,iko siku maana bahari haiweki uchafu na hakuna refu lisilokuwa na mwisho.
 
Ngoja Utawaona Lumumba Watakavo Bwabwaja Humu Ndani, Nyerere Alikua Gaidi

Kumsingizia marehemu tabia ambayo hakua nayo haklika nakuambia ni dhambi mbele ya MUNGU ,hakika nakuambia Nyerere kama binadamu alikua ana makosa yake lakini hakufikia level ya kuitwa gaidi hata na maadui zake.Kuna nchi jina lake likitajwa watu wanapatwa na misisimko, hawaamini kama alikua ni binadamu wa kawaida.wanamwona kama ni mombozi wa kisisasa.jitafakari.
 
Siyo BAN ya kuongea tu bali histoia yake yote imefutwa na wala hayumo miongoni mwa marais wastaafu.Hiyo ndiyo ccm bana.

Chadema kweli munapenda kuropoka search katika google tu list ya marais wastaafu uone kama hatokuja!
 
Yaonekana wengine ni wadogo Sana kiumri ama huwa hamfuatilii mambo ya kisiasa nchini.

Mzee Aboud Jumbe hajawahi kuzuiwa kuongea na Wanahabari, Bali amejiweka mwenyewe nje ya siasa, muda mwingi anajikita katika mambo ya dini Kama ilivyokuwa kwa swahiba wake Bashiru Kwaw Swanzy.

Ametoa Vitabu viwili kuhusu hilo sakata lake:
1. The Partnership: 30 Turbulent Years of the Tanganyika Zanzibar Union - Kitabu ambacho mwandishi Ally Saleh 'Al-bato' (aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Warioba) amekitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Kitabu hicho kilitoka mwaka 1994.

2. Tuishi bila kubaguana kidini - Hiki pia kimetoka miaka ya 90 mwishoni, na nadhani kwa undani humu ndo amechambua kuhusu nini kilitokea mpaka akajiuzulu.

*Pia kuna mswada wa Kitabu cha Jumbe ambacho kiliandikwa na Profesa Haroub Othman, makubaliano ni kuwa kitabu husika hakikupaswa kutoka mpaka Jumbe afe. Bahati mbaya Haroub ametangulia mapema zaidi, lakini bado mswada husika Uko chini ya familia ya Profesa Haroub.

*Katika Kitabu "Race, Revolution & Strrugle for Human Rights in Zanzibar: Memoirs of Ali Sultan Issa and Maalim Seif Shariff Hamad" Maalim Seif naye amelielezea hilo sakata.

*Mwaka 2007 kada wa CCM aitwaye nchimbi aliandika mfululizo wa Makala katika Gazeti la Mwananchi akiuita "Machozi ya Jumbe" mfululilo ambao ulijibiwa na Ismail Jussa (aliyekuwa msaidizi wa Maalim Seif wakati Huo). Mkipata hivyo maswali yenu yatajibiwa.

Eid Mubarak

Mkuu wewe ndio watu wanaoitwa wema katika dini sababu unaongea lile unalolijua sio kila unaloliona!
Hongera sana mkuu sababu watu siasa imewaathiri wanatunga na kuunganisha maneno
 
Yaonekana wengine ni wadogo Sana kiumri ama huwa hamfuatilii mambo ya kisiasa nchini.

Mzee Aboud Jumbe hajawahi kuzuiwa kuongea na Wanahabari, Bali amejiweka mwenyewe nje ya siasa, muda mwingi anajikita katika mambo ya dini Kama ilivyokuwa kwa swahiba wake Bashiru Kwaw Swanzy.

Ametoa Vitabu viwili kuhusu hilo sakata lake:
1. The Partnership: 30 Turbulent Years of the Tanganyika Zanzibar Union - Kitabu ambacho mwandishi Ally Saleh 'Al-bato' (aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Warioba) amekitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Kitabu hicho kilitoka mwaka 1994.

2. Tuishi bila kubaguana kidini - Hiki pia kimetoka miaka ya 90 mwishoni, na nadhani kwa undani humu ndo amechambua kuhusu nini kilitokea mpaka akajiuzulu.

*Pia kuna mswada wa Kitabu cha Jumbe ambacho kiliandikwa na Profesa Haroub Othman, makubaliano ni kuwa kitabu husika hakikupaswa kutoka mpaka Jumbe afe. Bahati mbaya Haroub ametangulia mapema zaidi, lakini bado mswada husika Uko chini ya familia ya Profesa Haroub.

*Katika Kitabu "Race, Revolution & Strrugle for Human Rights in Zanzibar: Memoirs of Ali Sultan Issa and Maalim Seif Shariff Hamad" Maalim Seif naye amelielezea hilo sakata.

*Mwaka 2007 kada wa CCM aitwaye nchimbi aliandika mfululizo wa Makala katika Gazeti la Mwananchi akiuita "Machozi ya Jumbe" mfululilo ambao ulijibiwa na Ismail Jussa (aliyekuwa msaidizi wa Maalim Seif wakati Huo). Mkipata hivyo maswali yenu yatajibiwa.

Eid Mubarak

Sasa huwezi elezea kwa kifupi hiyo issue
 
Nimemsikia Shujaa Tundu Lissu mara kwa mara akihusisha Muungano na Kuwekwa kizuizini Aboud Jumbe.

Eti Nyerere, mwasisi wa CCM ndie aliyempiga BAN mzee Jumbe.
Mohamed Said na Yericko Nyerere na Pasco naombeni mje hapa tuungane na wadau wengine tuwekewe ukweli huu hasa kwa kizazi cha 1980's ambao wengi hawajui nini kilitokea kwa Jumbe na kwa nini Tundu Lissu ameishikia bango sana hiyo

Tafuta historia ya "Mchafuko wa Hali ya Hewa Zanzibar"
 
Last edited by a moderator:
Acha uongo wewe, juzi tu alipewa nishani ya Miaka 50 ya Muungano.

Huyu Lissu naye kapotosha mno kiasi msiojua Kama nyinyi nanyi mwapayuka.

Andika Google "Sikumsaliti JUMBE - Maalim Seif" ili ujifunze kidogo.

Wewe ndiwe hujui;kwani Jumbe amekufa? Kama bado yuko hai kwa nini hakaribishwi kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa kama Rais mstaafu?
 
Tafuta historia ya "Mchafuko wa Hali ya Hewa Zanzibar"

Katika watu ninaowaheshimu hapa jf ni pamoja na wewe Kiranga. Taarifa niliyonayo ni kuwa hiyo historia wamei-spin
 
Last edited by a moderator:
Chadema kweli munapenda kuropoka search katika google tu list ya marais wastaafu uone kama hatokuja!

Kwa hiyo rais mstaafu anakuwa ni wa kwenye makaratasi na mitandaoni lakini siyo katika vitendo? Ni katika hafla zipi au sherehe gani za kitaifa Jumbe amealikwa kuhudhuria kama rais mstaafu? mbona wengine wanaalikwa hadi waziri mkuu aliyejiuzuru kwa ufisadi?
 
Acha uongo wewe, juzi tu alipewa nishani ya Miaka 50 ya Muungano.

Huyu Lissu naye kapotosha mno kiasi msiojua Kama nyinyi nanyi mwapayuka.

Andika Google "Sikumsaliti JUMBE - Maalim Seif" ili ujifunze kidogo.

Tunataka sauti au maneno kutoka kwa Abdul Jumbe na si maneno ya Sharif Hamad.Acha kupotosha hoja!
 
rafiki yangu kiranga tumegee kidogo ili tuujue ukweli

Kwa kifupi tu, Jumbe alikuwa anauhoji muungano, akawa anatayarisha namna ya kumuingia Nyerere kuhusu Zanzibar kuwa na madaraka zaidi kwa mujibu wa matakwa ya Wazanzibari, wakati anaandaa makaratasi yake, sekretari wake akayaona na kumtaarifu Seif Sharif Hamad. Seif akamtuma Sekretari wa Jumbe kuiba makaratasi yake na kumpelekea Nyerere. Nyerere akambana Jumbe na kumlazimisha kujiuzulu.

The details and narrative varies according to different sources, but that is the main story.

Ndiyo maana mpaka leo kuna vikao vya Seif Sharif na Nyerere havijulikani walizungumza nini.

Ndiyo maana Tundu Lissu anapenda kumtumia Jumbe kama shujaa aliyediriki ku question uongozi wa Nyerere kuhusu Muungano.
 
Katika watu ninaowaheshimu hapa jf ni pamoja na wewe Kiranga. Taarifa niliyonayo ni kuwa hiyo historia wamei-spin

Historia si moja, siku hizi kuna internet hata wewe unaweza kuandika unachojua.

Ukikalia kulia lia "wame spin" bila.ya kuelezea historia halisi kwa mujibu wako unapunguza nafasi ya ukweli kwa mujibu wako kujulikana.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi tu, Jumbe alikuwa anauhoji muungano, akawa anatayarisha namna ya kumuingia Nyerere kuhusu Zanzibar kuwa na madaraka zaidi kwa mujibu wa matakwa ya Wazanzibari, wakati anaandaa makaratasi yake, sekretari wake akayaona na kumtaarifu Seif Sharif Hamad. Seif akamtuma Sekretari wa Jumbe kuiba makaratasi yake na kumpelekea Nyerere. Nyerere akambana Jumbe na kumlazimisha kujiuzulu.

The details and narrative varies according to different sources, but that is the main story.

Ndiyo maana mpaka leo kuna vikao vya Seif Sharif na Nyerere havijulikani walizungumza nini.

Ndiyo maana Tundu Lissu anapenda kumtumia Jumbe kama shujaa aliyediriki ku question uongozi wa Nyerere kuhusu Muungano.

Ahaaaa.... Seif amekana lakini mkuu Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom