Tundu Lissu, Mtema ndani ya UDOM

Mmmmmm...kesho utasoma kwenye magazeti......wanasiasa wameenda UDOM kuchafua hali ya hewa.......
 
Watu wanataka kurudisha kadi kabla hata makamanda hawajaongea. Aliyekuwa mgombea ubunge CDM anaongea. Anasema wametishiwa wasije mkutanoni, lakini siasa ni kupigwa, kudharauliwa na mwisho ushindi.
 
Silent actor tupe mambo maana wengine ndio tumesimamishwa na hao magamba wakati tunadai haki yetu ya msingi.
 
Rejia Mtema anaongea: anaongea kuhusu mjadala wa bajeti. Mfumo mbovu wa kupitisha bajeti ambapo mbunge anaunga mkono as. 100 kisha anaeleza matatizo kibao jimboni. Mwanasheria mkuu amegeuka kada wa CCM. Kamanda Silinde ameingia pia.
 
Regia mtema anasema anashangaa wabunge wa ccm(ye anawaita MACCM),kabla ya kuanza kuchangia bajeti wanaanza kwanza kuunga mkono hoja kisha hufuata malalamiko ambayo tena huishia kwa kuunga mkono hoja!anasem MACCM wanahofia kurudi kwenye uchaguzi kwa kuwa weng walipita ama kwa kuchakachua au kwa mbinde.Anasema hayo ni mapungufu mengine ya katiba yetu.anasema katiba mpya iondoe huu udhaifu ili hata majority ya wabunge wakikataa kuunga mkono bajeti uchaguzi usirudiwe.
 
Mtema: Bajeti hii haiwezi kuwa na maana kusema uchumi unakua as. 7 wakati hauendani na hali halis ya maisha. Mikakati ya CCM imefeli kuwekeza kmenye nguvukazi ya wasomi. Wananchi waiunge mkono CDM kupinga ufisadi. Baraza la mwaziri la TZ linashawishiwa kwa maslahi ya watu wachache. Suala la posho: Jambo muhimu ni kubadili mfumo. Sitting allowance(appearance allowance?) ni wizi.
 
Silinde: ana uhakika mwaka 2015 kati ya majimbo 11 CDM wataibuka kidedea ktk majimbo zaidi ya 7. Maendeleo yanahitaji speed catalyst, siyo kutimiza ahadi kwa maneno.
 
Rejia amemaliza sasa anaingia silinde.anasema wakati wa mabadiliko ni sasa.Watanzania tumechoka kudanganywa.bungeni uongo unageuzwa ukweli.Tumeishi katika laana kwa miaka 50.Anasema hawakatai kwamba ccm kuna mazuri wamefanya lakini hayalingani na miaka 50.CCM wamelifanya taifa linakwenda linapotoka.mgombea anatoa ahadi kumi anatekeleza ahadi moja,kwaiyo itamchukua miaka 50 kumaliza ahadi zote za muhula wake wa kwanza!Vijana tumieni nafasi mliyonayo kufikisha ujumbe kwenye jamii ili kuleta mabadiliko kuchochea maendeleo.
 
Walishamaliza mitihani hawa wanafunzi? Umasikini+ Shule+Siasa=Kutangatanga. Waacheni vijana wasome kwanza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom