nowsasa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 1,095
- 1,130
Umemuelezea huyu bishoo rasta..namkumbuka sana miaka ileee pale mjini kati yeye na akina ngomaley na marasta wengine wa wakati wakizengea vidosho wa kizungu huku wakiwa wamevaa batiki zao na mbwembwe nyingi...wampuuze huyu msanii.Huyu mwandishi ni Rastafarian,ana bendi yake inaitwa "The Ngoma African Band".Huyu Ras namfahamu sana,na sidhani anawakilisha hisia za Watanzania wote wanaoishi Ujerumani na Austria.
Watu wanajisahau sana,hizi sio zile nyakati za kina Moses Nnauye na Propaganda nyepesi,hizi ni nyakati za kizazi chenye kudadisi chini ya mwamvuli wa technolojia.
Ras anafanya haya yote sababu ya maslahi ya kuendelea kuishi Ujerumani na kupewa tenda za matamasha ya utamaduni wa Afrika kupitia Ubalozi,ni lazima alifanye hili,and he is not that much smart,ngoja tumtunzie heshima tu.
Ila ndugu yangu Ras hukupaswa kupachikwa kwenye aina hii ya mgongano,ungekaa kimya kama wenye busara wengine walivyokaa kimya kwenye mtifuano huu.
Nakumbuka Austria msimu wa majira ya joto kulikiwa na Tamasha la Waafrika,ikiitwa "African Festival",huyu bwana alikuwa anakuja na band yake anapiga na pale Germany.Enzi za kina Mahalu akiwa Italy na yule bitozi akiwa Ujeruman wakati wa Ben Mkapa.
Ras kinachomsukuma ni tender za matamasha ya Kiafrika na yale ya kiutamaduni ambapo ubalozi wa Ujerumani umekuwa ukimtumia sana kuimba na kuburudisha.Na nyimbo zake sio nzuri vileee,ni ile radha tu ya Kiswahili unayopenda kuisikia ukiwa mbali na nyumbani.
Miaka ya nyuma bend yake ilikuwa inatumia wanenguaji toka Tanzania,kwa hiyo alihitaji vibali kadhaa kama toka Wizara ya Utamaduni ili kwenda Ubalozi kuomba Viza,haya yote yanamsukuma kufanya anachofanya.
Ras ni mtoto wa mjini kati Dsm,ni wale marasta wala nyama kwa kificho,hawana imani hiyo kwa dhati,walifunga rasta wakati huo wa wimbi la watoto wa kizungu waliokuwa wanawavizia pale YMCA Posta kipindi cha Majira ya joto Ulaya wanapokuja kujitolea au likizo Afrika.Vijana wengi walifunga rasta sbb wasichana wakizungu waliwaamini Rastafariani na waliolewa nao wakawapeleka Ulaya.Hii ni rika la yule Mwandishi mashahuri ambaye na yeye alikuwa na rasta ila alinyoa,anajiita "Mwenyekiti".
Ngoja tumstahi Ras wetu,japo naamini alichoandika siyo kuwa ni msimamo wa Watanzania wote,na si kweli kuwa hawaruhusiwi kukutana na viongozi wa siasa,ila hairuhusiwi kujiingiza kwenye siasa za ndani ya Ujerumani.
Mwaka 2010 alimtungia kibao Kikwete cha kumpigia kampeni kurudi Madarakani,alikiita "Jakaya Kikwete 2010".Andishi hili linaonyesha kanisa Ephraim siyo mbabiloni(Babylon Man).Wababiloni huwa wanasimama na upande wanaohisiwa kuonewa mpaka pale ukweli utakapothibitisha kuwa hawajaonewa.Hii ndio imani ya marasta wote kuanzia kina Bob Marley na Lucky Dube mpaka kina Justine Kalikawe....Huyu ni mbabiloni mpya huyu
Lissu hana chembe wala sifa za Uhaini,wazungu sio wajinga kiasi hicho.Ingekuwa ni hivyo,kina Dr Slaa enzi hizo wasingekuwa wanafanya Mikutano London,Ujerumani huko mpaka Italia.Asipotoshe kana kwamba ni yeye tu kakaa Ujerumani.
Sent using Jamii Forums mobile app