Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,168
Ras kavuta mibangi yake kaamua kutoka kivyake.
Mkuu usiifananishe Bangi na Vitu vya Ajabu ,huyo ana Maslahi yake kaamua akae Upande wa Makuhani..
Ras kavuta mibangi yake kaamua kutoka kivyake.
Mwambie Lissu aje kubwatukia hapa bongo Kama kweli hamuogopi jela
Sent using Jamii Forums mobile app
Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani, umetoa taarifa ya kwamba hawapo tayari kujishughulisha kwa namna yoyote ya shughuli za vyama vya kisiasa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuaanda mikutano ya wanasiasa nchini humo.
Kupitia barua inayoaminika kuandikwa na kiongozi wa umoja huo, Ephraim Makanja imeeleza mbali na kuandaa mikutano, Watanzania waishio ujerumani hawaruhusiwi kufanya mapokezi ya viongozi wa kisiasa kwa kuwa wamepata taarifa kwamba wapo wanasiasa wanataka kuwageuza jukwaa la kisiasa.
Bw. Makanja ameeleza kwamba, anawaasa watanzania wanaoishi ujerumani kutotumika kwa namna moja ama nyingine katika kuandaa mikutano ya aina hiyo na kwamba umoja huo hautakubali kutumika kama jukwaa. "Hatutaki mkutano na viongozi wa vyama vya kisiasa kwani sisi sio kambi ya siasa," Imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Tamko hili la Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani limekuja kiwa ni siku chache kupita tangu Mbunge wa Singida Mashariki , Tundu Lissu alipopata nafasi ya kuzungumza Washington DC na watanzania waishio nchini Marekani.
View attachment 1022152
Lissu kuzuiliwa Ujerumani? | East Africa Television
Je, hii ni kwa viongozi wa upinzani pekee au kwa vyama vyote?
Je, ikitokea Bashiru Ally au Polepole akaenda huko, hatopokelewa?
Kwa kweli
Maana jinsi siku zinvyo kwenda ndio unafiki na uwongo wa Tundu Lissu unavyo kuwa uchi
Huyu jamaa ni lila rushwa tangu zamani na uzalendo kwake ni mwiko kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
hii ni uthibitisho kuwa anawasumbua sana
kama ulivyo comment wewe yalikubana sana kamanda?Mara nyingine inabidi mkoment tu ili kinyesi kitoke tunduni
Mliwezaje kumpa uongozi mtu duni kama huyu ?Sio kweli!
Kama ni kweli kaandika huyo Ephrahim makanja, basi kaamua kuandika akiwa chumbani kwake bila kutushirikisha sisi vijana wa kitanzania tunaoishi Ujerumani.
Tena mwambieni huyo mpumbavu aliyeandika hiyo barua kuwa, mawazo yake sio mawazo ya vijana wa kitanzania waliopo hapa Ujerumani
Mmmh! Umempa za uso! Alidhani ujerumani anaifahamu ƴeƴe peke ƴake!Huyu mwandishi ni Rastafarian,ana bendi yake inaitwa "The Ngoma African Band".Huyu Ras namfahamu sana,na sidhani anawakilisha hisia za Watanzania wote wanaoishi Ujerumani na Austria.
Watu wanajisahau sana,hizi sio zile nyakati za kina Moses Nnauye na Propaganda nyepesi,hizi ni nyakati za kizazi chenye kudadisi chini ya mwamvuli wa technolojia.
Ras anafanya haya yote sababu ya maslahi ya kuendelea kuishi Ujerumani na kupewa tenda za matamasha ya utamaduni wa Afrika kupitia Ubalozi,ni lazima alifanye hili,and he is not that much smart,ngoja tumtunzie heshima tu.
Ila ndugu yangu Ras hukupaswa kupachikwa kwenye aina hii ya mgongano,ungekaa kimya kama wenye busara wengine walivyokaa kimya kwenye mtifuano huu.
Nakumbuka Austria msimu wa majira ya joto kulikiwa na Tamasha la Waafrika,ikiitwa "African Festival",huyu bwana alikuwa anakuja na band yake anapiga na pale Germany.Enzi za kina Mahalu akiwa Italy na yule bitozi akiwa Ujeruman wakati wa Ben Mkapa.
Ras kinachomsukuma ni tender za matamasha ya Kiafrika na yale ya kiutamaduni ambapo ubalozi wa Ujerumani umekuwa ukimtumia sana kuimba na kuburudisha.Na nyimbo zake sio nzuri vileee,ni ile radha tu ya Kiswahili unayopenda kuisikia ukiwa mbali na nyumbani.
Miaka ya nyuma bend yake ilikuwa inatumia wanenguaji toka Tanzania,kwa hiyo alihitaji vibali kadhaa kama toka Wizara ya Utamaduni ili kwenda Ubalozi kuomba Viza,haya yote yanamsukuma kufanya anachofanya.
Ras ni mtoto wa mjini kati Dsm,ni wale marasta wala nyama kwa kificho,hawana imani hiyo kwa dhati,walifunga rasta wakati huo wa wimbi la watoto wa kizungu waliokuwa wanawavizia pale YMCA Posta kipindi cha Majira ya joto Ulaya wanapokuja kujitolea au likizo Afrika.Vijana wengi walifunga rasta sbb wasichana wakizungu waliwaamini Rastafariani na waliolewa nao wakawapeleka Ulaya.Hii ni rika la yule Mwandishi mashahuri ambaye na yeye alikuwa na rasta ila alinyoa,anajiita "Mwenyekiti".
Ngoja tumstahi Ras wetu,japo naamini alichoandika siyo kuwa ni msimamo wa Watanzania wote,na si kweli kuwa hawaruhusiwi kukutana na viongozi wa siasa,ila hairuhusiwi kujiingiza kwenye siasa za ndani ya Ujerumani.
Mwaka 2010 alimtungia kibao Kikwete cha kumpigia kampeni kurudi Madarakani,alikiita "Jakaya Kikwete 2010".Andishi hili linaonyesha kanisa Ephraim siyo mbabiloni(Babylon Man).Wababiloni huwa wanasimama na upande wanaohisiwa kuonewa mpaka pale ukweli utakapothibitisha kuwa hawajaonewa.Hii ndio imani ya marasta wote kuanzia kina Bob Marley na Lucky Dube mpaka kina Justine Kalikawe....Huyu ni mbabiloni mpya huyu
Lissu hana chembe wala sifa za Uhaini,wazungu sio wajinga kiasi hicho.Ingekuwa ni hivyo,kina Dr Slaa enzi hizo wasingekuwa wanafanya Mikutano London,Ujerumani huko mpaka Italia.Asipotoshe kana kwamba ni yeye tu kakaa Ujerumani.
Huyu mwandishi ni Rastafarian,ana bendi yake inaitwa "The Ngoma African Band".Huyu Ras namfahamu sana,na sidhani anawakilisha hisia za Watanzania wote wanaoishi Ujerumani na Austria.

Kama wale wa marekani wanajiita Diaspora tuHawa ndio wale wanaochanganya Kati ya Watanzania waishio Ujerumani na Genge la wajinga wa Ccm waishio Ujerumani....