Tundu Lissu: Kuna mtu ana ugonjwa mbaya wa kutaka kusifiwa muda wote hata kwa mambo ambayo sio ya kweli

Inferiority complex is a mental condition that could lead to ADS!
 
Nyani haoni kinyeo chake!!!
Mwishowe nitaamini maneno ya Barbarosa kuwa Lissu akiona kuna tukio ambalo litamfanya asahaulike anatafuta namna yoyote kuandika chochote ili asisahaulike.
Leo amejua watu tuko busy na mheshiwa "Sugu" kuwa huru kwa hiyo na yeye kaona asibaki nyuma.
Mapovu ruksa.
lengo la hili andiko lako la kishamba ni nini ? maana ni wazi kwamba Sugu amemaliza kifungo na wala hakusamehewa na shetani wala mtu yeyote .
 
KUNA MTU ANA UGONJWA WA KUBEZA JAMBO LOLOTE LINALOFANYWA NA KIONGOZI WA NCHI, UGONJWA HUO UNAITWA "UKWELI DEFFICIENCY SYNDROME". HUU UGONJWA HUSABABISHWA NA CHUKI,UZANDIKI,UBINAFSI NA UONGO ULITOPEA.MTU HUYU ANAWEZA HATA KUCHANGIA NA KUFURAHIA JAMBO LENYE KUATHIRI NDUGU ZAKE ILI MRADI JAMBO HILO LIWE NA MUELEKEO WA KULETA PICHA MBAYA KWA KIONGOZI NCHI
 
Kuna mtu ana ugonjwa mbaya wa kutaka kusifiwa muda wote hata kwa mambo ambayo sio ya kweli. Ugonjwa huu nauita 'Attention Deficiency Syndrome' au ADS. Nitoe mfano halisi wa dalili za ADS.

Leo Joe Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Kanda Emmanuel Masonga wameachiliwa huru baada ya kukaa gerezani miezi mitatu kwa chuki na hila za kisiasa tu.

Mara ghafla tunawasikia wapambe Magufuli wakisema Sugu na Masonga wameachiliwa kwa msamaha wa Rais na jina la Bwana Mtukufu Rais lihimidiwe!!!

Kama kweli wameachiliwa kwa msamaha wa Rais, kwa nini imechukua wiki mbili tangu tarehe 26 Aprili inayodaiwa kuwa ndio siku ya msamaha huo???

Kwa nini Magufuli mwenyewe hakusema ametoa msamaha huo kwa Sugu na Masonga???

Kama kuna mtu anafikiri hilo haliwezekani, akumbuke Rais Ali Hassan Mwinyi alifanya nini kwa wanajeshi waliofungwa maisha kwa kujaribu kuipindua Serikali ya Mwalimu Nyerere.

Mwinyi alitoa taarifa rasmi kwamba amewapa msamaha wahaini hao. Hiyo ilikuwa mwaka '95 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Tuendelee. Kila mfungwa, ukiachia waliofungwa kipindi kirefu kwa makosa makubwa au waliohukumiwa kifo, anastahili kupata automatic remission ya theluthi moja ya kifungo chake.

Remission hii ilikuwa inawahusu Sugu na Masonga vile vile. Je, hawakuipata??? Kama wameipata kama inavyotakiwa na sheria, hiki kinachoitwa msamaha wa Rais ni kitu gani kama sio uthibitisho wa ugonjwa wa ADS???

Lissu, Ubelgiji,
10 Mei 2018.
Lisu hawezi kuandika hivi, haya ni mawazo yako
 
lissu aache kulopoka atuambie sugu amehukumiwa juzi tu miez mitano kwa muda aliokaa miezi mitano imeisha
 
Huu ugonjwa wa kupenda kusifiwa kila kitu ndio utaimaliza Tanzania.

Yani mtu anapenda asifiwe tuuu, kila kitu kisifiwe tuuu. Juzi nimeshangaa sana, watu tunasema mfumo wetu wa elimu ni mbovu, mitaala yetu imepitwa na wakati na inabidi irejewe upya, ubora wa elimu umeshuka mtu anapinga anasema watu waende kuona panya anaegundua kifua kikuu elimu haijashuka.

Yani panya kutegua mabomu ndio kielelezo kua elimu haijashuka? Kwani ni panya wa Tanzania tu wanaojua kutegua mabomu?

Yani mtu anapenda kusifiwa kila kitu, yani anataka watu wasema uchumi unakua kwa kasi, ajira milioni 3 zimetengenezwa, makusanyo ni trillion 40 kwa mwaka, standard gauge, stiglers gorge, barabara na madaraja kila kona, ndege dreamliner 2 na bombadia 6, mfumuko wa bei hakuna, ufaulu 100%, kiwango cha elimu hakuna mfano duniani, ufisadi hakuna, amani 100%, nidham 1000%, uchapakazi 2000%, foleni dar hakuna, maji kila nyumba na kila mtaa, umeme kila nyumba, madawa hospitalini ni ya kumwaga, vitanda vya wagonjwa hadi wagonjwa wanapungua, madaktari wa kufa mtu, hospitali za rufaa kila wilaya nk nk. Watu wanataka kuona hayo.

Ukisema vingine wewe sio mzalendo wa kweli. Hatari.
 
Nyani haoni kinyeo chake!!!
Mwishowe nitaamini maneno ya Barbarosa kuwa Lissu akiona kuna tukio ambalo litamfanya asahaulike anatafuta namna yoyote kuandika chochote ili asisahaulike.
Leo amejua watu tuko busy na mheshiwa "Sugu" kuwa huru kwa hiyo na yeye kaona asibaki nyuma.
Mapovu ruksa.
Jifunze maana ya siasa,na kazi ya mwana siasa,alafu jufunze zaidi kuhusu siasa za upinzani zinafanywaje,ukiyajua hayo uje upitie upya komenti yako.
 
Kuna mtu ana ugonjwa mbaya wa kutaka kusifiwa muda wote hata kwa mambo ambayo sio ya kweli. Ugonjwa huu nauita 'Attention Deficiency Syndrome' au ADS. Nitoe mfano halisi wa dalili za ADS.

Leo Joe Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Kanda Emmanuel Masonga wameachiliwa huru baada ya kukaa gerezani miezi mitatu kwa chuki na hila za kisiasa tu.

Mara ghafla tunawasikia wapambe Magufuli wakisema Sugu na Masonga wameachiliwa kwa msamaha wa Rais na jina la Bwana Mtukufu Rais lihimidiwe!!!

Kama kweli wameachiliwa kwa msamaha wa Rais, kwa nini imechukua wiki mbili tangu tarehe 26 Aprili inayodaiwa kuwa ndio siku ya msamaha huo???

Kwa nini Magufuli mwenyewe hakusema ametoa msamaha huo kwa Sugu na Masonga???

Kama kuna mtu anafikiri hilo haliwezekani, akumbuke Rais Ali Hassan Mwinyi alifanya nini kwa wanajeshi waliofungwa maisha kwa kujaribu kuipindua Serikali ya Mwalimu Nyerere.

Mwinyi alitoa taarifa rasmi kwamba amewapa msamaha wahaini hao. Hiyo ilikuwa mwaka '95 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Tuendelee. Kila mfungwa, ukiachia waliofungwa kipindi kirefu kwa makosa makubwa au waliohukumiwa kifo, anastahili kupata automatic remission ya theluthi moja ya kifungo chake.

Remission hii ilikuwa inawahusu Sugu na Masonga vile vile. Je, hawakuipata??? Kama wameipata kama inavyotakiwa na sheria, hiki kinachoitwa msamaha wa Rais ni kitu gani kama sio uthibitisho wa ugonjwa wa ADS???

Lissu, Ubelgiji,
10 Mei 2018.
Nadhani Lissu ndiye mwenye huo ugonjwa wa ADS. Na yote ni kwa sababu ya kujifanya mjuaji au kujikita katika mazoea ambayo safari hii Magufuli amefanya kinyume chake. 26/8 Rais alisamehe wafungwa wenye sifa kwa 1/4 ya muda wao waliotakiwa kukaa gerezani. Hakuamuru watolewe mara moja!! Yaani aliyetakiwa kukaa gerezani miezi minne unapunguziwa mwezi mmoja baada ya miezi mitatu unaachiwa. Sasa Lissu alitaka Sugu anayekuwa na kifungo cha kuishia June aachiwe siku hiyo hiyo? Mwambieni punguzo la 1/4 la kifungo cha Sugu imefikia leo mambo huku yamebadilika siyo aliyozoea!!!
 
Back
Top Bottom