Hivi kuna mtu ana takwimu ya wahandisi na technians wa umeme Tanzania?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,965
Ninaanza kuwa na wasiwasi huenda tatizo tulilo nalo ni wataalam na sio umeme.

Hapo zamani Tanesco walikuwa na chuo chao pale Morogoro kwa ajili ya kuzalisha mafundi.Kwa sasa sijui iwapo vyuo vya ufundi vilivyopo vinazalisha mafundi wa kutosha.Inaonekana ni vigumu kuwachukulia hatua hawa waliopo labda pengine kwa sababu hawana mbadala.
Jambo hili limewafanya hawa waajiriwa wa Tanesco wawe na kiburi sana.

Hakuna lugha mtakayotuambia kuhusu kukata umeme bila mpangilio kila Sikh kwani lugha zote mmeshazisema.

Ilianza kwa Makamba eti mitambo na njia vinafanyiwa matengenezo makubwa.

Baada ya hapo kiangazi kikaingia tukaambiwa maji yamepungua kwenye mabwawa.
Mvua zimenyesha hadi tunaona mafuriko wao wanatwambia eti hizi mvua hazinyeshi kwenye mabwawa.
Nina uhakika kesho wanaweza kuyabomoa mabwawa ili maji yaishe waje na mradi wa matrioni kukarabati mabwawa.

Baada ya ukarabati mkubwa wa mitambo na njia za kusambaza umeme,baada ya mvua kubwa kunyesha,baada ya chanzo kipya cha umeme Rusumo kuanza uzalishaji,baada ya majaribio ya uzalishaji wa bwawa la mwalimu Nyerere,Leo mnaweza kuwa na sababu gani ya kutuambia kwa nini umeme unakatika bila mpangilio?

Kama kuna uhakika wa wataalamu walio nje ya ajira,kuna umuhimu wa kufukuza wote wasiojitambua na kuwajibika.Wanafanya hujuma maksudi kwa mama.Mama hawastukii wajinga hawa.Walimdanganya eti baada ya miezi sita tatizo litaisha,ila ninachoona miezi sita inakaribia kuisha tatizo ndio linazidi kuwa sugu.
Wako wapi mawaziri walifanikiwa kwa hawa vichwa ngumu wa Tanesco?
 
Kataa siasa ni utapeli...Hapo hamna wente uwezo wapo wanasiasa na kuleta mazoea kweny mambo ya kutumia akili nyingi
 
Haya yote ni matokeo ya kutoajiri watu kwa miaka mingi hapo nyuma. Waliopo wamechoka, mishahara ipo chini, hakuna Motisha, Bora liende. Wanazidiwa kazi. Jaribu kuangalia sekta zote anzia Elimu , Afya, Mawasiliano TTCL, zipo hoi. Ni vile tu Tanesco inagusa maisha ya Kila siku.
 
Back
Top Bottom