Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,410
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa Tundu Lissu ndiye atakayemrithi Dr Slaa endapo chama kitapata taarifa rasmi za kujiuzulu kwake. Chanzo hicho kinasema kuwa tayari Dr Slaa ameandika barua ya kujiuzulu na imefika kwenye mamlaka husika.

Chanzo hicho kinasema kuwa baada ya ujio wa Lowasa, hali ndani ya chama hicho ilikuwa tete hasa baada ya Tundu Lissu, John Mrema, John Mnyika na Dr Slaa kuanza mgomo wa kutoafiki maamuzi ya chama ya kumchukua Dr Slaa. Chanzo hicho kimenitokeza kuwa, chanzo cha mgomo huo ni kutokana na kukerwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei aliyetishia kuwafukuza viongozi hal endapo wangeendelea kuwa na msimamo wa kupinga ujio wa Lowasa. Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimenidokeza kuwa ilibidi Freeman Mbowe amuombe Mzee Mtei abatilishe msimamo wake wa kuwafukuza wanasiasa hao.

Kutokana na maombi hayo ya Mbowe kwa Mtei, hatimaye deal lilifanyika ambapo juzi Jumatano kilifanyika kikao cha falagha baina ya Lissu, Mbowe na Mtei. Katika kikao hicho Lissu alisema kuwa aliwafikishia ujumbe wenzake wa kuhudhuria kikao hicho isipokuwa wamekataa. aidha, Lissu alitoa maelezo yake kwa nini aliungana na Dr Slaa kupinga ujio wa Lowasa. kubwa alilolieleza ni tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowasa na kwamba watakuwa na wakati mgumu wawapo majukwaani kumnadi mwanasiasa huyo.

Hata hivyo, Mzee Mtei aliwaeleza kuwa tishio la kuwafukuza wanasiasa hao lilitolewa kwa ghadhabu na kwamba suluhu zaidi inahitajika kuliko mabavu. Pia alisema kuwa wakati uliopo mchango wao unahitajika sana na yeye yupo tayari kufuta kauli yake endapo watamhakikishia kuwa watakuwa tayari kumnadi Lowasa na kubadilisha fikra za Watanzania ili waamini kuwa tuhuma za ufisadi hazikuwa za msingi. Aidha, kutokana na Dr Slaa kuendelea na mgomo, Mzee Mtei alimuomba Lissu kujitokeza kwenye Media na kutoa maelezo kuwa yupo pamoja na Lowasa. Aidha, Lissu pia aeleze kwa nini Lowasa alijumuishwa kwenye List of Shame na aeleze kwamba ni yeye ndiye aliyeandaa orodha hiyo na kwamba alimpa tu Dr Slaa aisome. Likifanyika hilo, Mzee Mtei alisema kuwa watakuwa wamefanikiwa kuondoa List of Shame kutoka mikononi mwa Dr Slaa na kwamba kazi ya kumsafisha Lowasa itakuwa nyepesi.

Aidha, kwa vile Dr Slaa ameonekana kuendelea kukataa kumuunga mkono Lowasa, kikao hicho kilifanya maamuzi ya kumteua Tundu Lissu kujaza nafasi ya Dr Slaa. Kutokana na maamuzi hayo, ni dhahiri kwamba, Tundu Lissu ndiye atakayekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuziba nafasi ya Dr Slaa.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni kutolewa kwa taarifa rasmi ya kujiuzulu Dr Slaa ndipo taratibu za kichama zifanyike.

Mjumbe hauawi.
 
Tuambie mgogoro huu utawaokoaje CCM? Maana ni kama mbinu na hila hizi zinawapotezea muda na wala hazionekani kuwaokoa katika mshike mshike dhidi ya CCM vs UKAWA. Kwa wasomaji wa Biblia hata Yesu alisalitiwa na Yuda Iskariote karibu kabisa na Yesu kukamilisha misheni yake hapa Duniani.
 
Naona Lizabon umekuwa msemaji wa Chadema sasa. Vipi Membe anaendeleaje??
 
Nadhani ungeachana na habari za chadema ujikite zaidi kutoa habari za Magufuri
 
Sasa umeanza kusemea ukawa bado unaweweseka tu
 
Kama hii habari ni ya kweli tuambieni bwana. Msituchanganye Chadema wakati mnajua hali tete
 
haujawahi kuleta taarifa ya ukweli hapa jamvini tangu enzi za nuhu
 
Back
Top Bottom