Uchaguzi 2020 Tundu Lissu jambo hili kuhusu wabunge wa CCM kupitisha sheria zinazotumiiza naomba kila unapoenda na kila katika mkutano wako uliongelee

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Naomba nikiri nimefurahi sana kusikia umeeleza ni namna gani wabunge wa CCM wamepitisha sheria zinazotuumiza wananchi.

Kwanini nimefurahi sana?

Sababu kubwa ni hii,baadhi ya watanzania wenzetu wanaanza kusahau tabia za wabunge wa CCM na kuwa tayari kuwachagua kisa ni matajiri,watu maarufu,wana majina makubwa,n.k ila wanasahau wabunge hawa wawapo bungeni,hata kama ni matajiri au ni maarufu kiasi gani,huwa hawana msaada kwa wananchi hasa katika kupitisha sheria zinazoletwa na serikali yao Bungeni.

Hivyo,naomba Lissu na wagombea wote wa ubunge wa CHADEMA nchi nzima,tumieni kipindi hiki kuwakumbusha wananchi wasibabaike na baadhi ya majina makubwa na maarufu kwani majina hayo kwenye part caucus ya chama ni madogo kuzidi la salary slip wa JamiiForums.

Kwa mfano,wakumbusheni wananchi kuwa watu kama kina Tarimba,Jerry Slaa,Dr.Kimei na wengineo,watu hawa wakiingia Bungeni,hawawzi kukwepa ule utaratibu wa kusemaa ndioooo.

Jengeni hoja kwa kuwakumbusha wananchi sheria zingine kama ile ya kuongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilima 8 mpaka 15,sheria ya iliyohusu kikokotoo,sheria ya vyama vya siasa,sheria ya mtandao,n.k kuwa sheria hizi ni kazi ya wabunge wa CCM kwahiyo kumrudisha Magufuli na wabunge wa CCM ni kutengeneza mazingira ya sheria nyingine kandamizi kama hizi kutungwa na kupitishwa.

Naposema limenifurahisha ni kwasabubu nilishaliongelea hapa JF kwani naona ziko dalili za baadhi ya watanzania wenzetu kusahau mwenendo wa wabunge wa CCM wawapo Bungeni na kupumbazwa na majina makubwa au umaarufu walionao.

Nawasihi sana swali hili lipeni kipaumbe katika mikutano yenu ya kampeni nchi nzima kama mnavyofanya kwa swala la wafanyakazi kutoongezewa mishahara kwa miaka mitano na swala wafanyabiasha kunyanyaswa na TRA na mengineyo.

Wapinzani wakumbusheni Watanzania madhara ya wabunge wa CCM yakiwemo kubariki (makato makubwa ya Bodi ya Mikopo, kuunganisha Mifuko, kikokotoo kipya)

Uchaguzi 2020 - Chonde chonde Watanzania,msisahau mwenendo wa wabunge wa CCM wawapo Bungeni na hatari ya kuwarudisha tena Bungeni kwa wingi
 

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
873
1,000
Naunga mkono hoja. Wabunge kupitia chama tawala ni maadui zetu! Wao watapitisha lolote wanalotakiwa kulipitisha na chama/serikali yao! Wakifika bungeni hawana habari na wananchi waliowachagua. Kazi yao kubwa inakuwa kulinda vitumbua vyao bas! Hawakutusaidia zaidi ya kupitisha sheria kandamizi! Hawa hawatakuwa na jipya zaidi ya kuendelea kugonga meza na kuitikia ndioooo.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Naunga mkono hoja. Wabunge kupitia chama tawala ni maadui zetu! Wao watapitisha lolote wanalotakiwa kulipitisha na chama/serikali yao! Wakifika bungeni hawana habari na wananchi waliowachagua. Kazi yao kubwa inakuwa kulinda vitumbua vyao bas! Hawakutusaidia zaidi ya kupitisha sheria kandamizi! Hawa hawatakuwa na jipya zaidi ya kuendelea kugonga meza na kuitikia ndioooo.
Bahati mbaya sana jambo hili ni kama halipewi uzito kwenye kampeni huku wananchi nao wakianza kusahau ukweli huu.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Naomba nikiri nimefurahi sana kusikia umeeleza ni namna gani wabunge wa CCM wamepitisha sheria zinazotuumiza wananchi.

Kwanini nimefurahi sana?
Sababu kubwa ni hii,baadhi ya watanzania wenzetu wanaanza kusahau tabia za wabunge wa CCM na kuwa tayari kuwachagua kisa ni matajiri,watu maarufu,wana majina makubwa,n.k ila wanasahau wabunge hawa wawapo bungeni,hata kama ni matajiri au ni maarufu kiasi gani,huwa hawana msaada kwa wananchi hasa katika kupitisha sheria zinazoletwa na serikali yao Bungeni..
CC: Molemo CHADEMA Chadema Diaspora
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,953
2,000
Kwa maovu ya awamu ya tano pekee, Lissu anaweza akaongea siku nzima na asiyamalize.

Mengine madiwani na wabunge wamsaidie.

Zitengenezwe clips ambazo zitasambazwa kwa watu zenye matamshi ya rais, wabunge na madiwani wa CCM walioyatoa kwa miaka mitano ya kwanza.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,976
2,000
Kwa mfano,wakumbusheni wananchi kuwa watu kama kina Tarimba,Jerry Slaa,Dr.Kimei na wengineo,watu hawa wakiingia Bungeni,hawawzi kukwepa ule utaratibu wa kusemaa ndioooo.
Wananchi hawataki kusikia Hilo
Kila siku mnafanya makosa Yale Yale,kulia Lia wakati wa kampeni badala ya sera
Huu ni uchaguzi mwepesi sana kwa ccm toka iundwe,Ni uchaguzi wa vitu au maneno matupu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom