Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

Pinda kuachia ngazi kwa kushindwa si ajabu tena kwa kauli yake ya liwalo na liwe na likawa Ulimboka kupigwa hakika anatakiwa aondoke, mbona mwenzie Lowasa alijipima akaona boro kuachia ngazi pamoja na kwamba alikuwa anachapa kazi kuliko pinda?
 
Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe. Lissu hakutenda haki. Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.

Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima. Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo. Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima, aache ulaji alionao sasa, ni sawa na kumwambia ajiue.

Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema:

'If you have done everything in your power and failed why don't you resign?'

Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.

Lakini Pinda alisema '...Mhe. Lissu lugha hiyo si nzuri sana... mimi nakuheshimu sana....'


Wewe ndio hujamtendea haki Tindu Lisu. Muombe msamaha haraka kabla hujapata BAN
 
Back
Top Bottom