Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maseto, Jun 28, 2012.

 1. M

  Maseto JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe. Lissu hakutenda haki. Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.

  Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima. Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo. Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima, aache ulaji alionao sasa, ni sawa na kumwambia ajiue.

  Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema:

  'If you have done everything in your power and failed why don't you resign?'

  Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.

  Lakini Pinda alisema '...Mhe. Lissu lugha hiyo si nzuri sana... mimi nakuheshimu sana....'
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa watu wanaoelewa na kukubali utawala wa demokrasia/vyama vingi, basi watakubaliana na kauli ya Lissu 100%. Alichosema na namna alivyosema Lissu ndivyo inavyotakiwa. Mh Pinda anafanya 'zilipendwa' akisaidiwa na Spika, lakini gharama za huu muziki wa zilipendwa zitalipwa na CCM.

  Kwa kiongozi yoyote ambaye anashindwa kufanya yale anayooamini na ambayo wanachi wanamtegemea kwa sababu zozote zile (iwe mfumo, ugonjwa, whatever) basi kiongozi huyo anatakiwa ajiuzulu. Kuendelea kukalia kiti ni sawa na kugeuka jiwe. Katika hali ya sasa Pinda hawezi kusema ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari halafu akaendelea na kazi zake kama Waziri mkuu. Haiwezekani. Ama unaondoa vizingiti (mfumo mbaya) au vizingiti vinakuondoa. Lakini vyote viwili haviwezi kubaki halafu tukasema tuna uongozi bora. Tuna shida sana na mentality ya zilipendwa.
   
 3. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nimeona alionekana kuwa amekasirika sana Mh.Pinda,lakini napata tatizo sana na busara zake! wakati mwingine huwa anatamka maneno kama yuko kijiweni. Leo alikuwa anashindwa tu kusema kauli aliyotoa jana haikustahili.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  For how long we should remain without solution for doctors' strikes? Nina ndugu yangu yuko serious kapelekwa hospitali jana (Kibosho hospital) hakuhudumia kuwa zima kwa kuwa madaktari wako kwenye vikao visivyoisha.
   
 5. a

  alfazulu JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 735
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI MKUUU ALITAKA AELEZWEJE? AU ALITAKA UJUMBE HUO UMFIKIE KUPITIA MTU ASIYE MHESHIMU? swala la kuheshimiana au kutoheshimiana na Lisu Linahusianaje na ukweli unaoonekana wazi kuwa ameshndwa kusuluhisha tatizo lillilopo?
   
 6. M

  MUNYAMAKWA Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teeh teeh teeh!! ulaji mtamu jamani.Nani aachie ngazi kiulaini hivi ,labda asiwe kiongozi wa Nchi hii .Kwanza Hatuna utamaduni wa Watawala(viongozi) kuwajibika pindi mapungufu yanapotokea mikononi mwao.Na yeyote atapomkumbushia mtawala au kiongozi husika juu ya jukumu hili la kuwajibika , badala yake ataona kama anafanyiwa fitina.Ninashauri viongozi wa ngazi za juu muwe mfano katika kuwajibika ili hawa wachini yenu waone suala hili kama jambo la kawaida na si la majungu au fitina kama linavyodhaniwa
   
 7. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Politics ikichanganywa na Professional kinachojitokeza ni VITUKO Visivyoisha.
   
 8. w

  warea JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu amtazame mgonjwa wako, maana yeye si mwanadamu.
   
 9. M

  MTK JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?" the statement is clear full stop.
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,475
  Trophy Points: 280
  "mh. Lissu lugha hiyo sio nzuri sana.... Mimi nakuheshimu sana..." upm mtam jamani pinda ametoa kauli toka uvunguni mwa moyo wake.!!
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jamani uongoz watu wanaufurahia tu ila ni mgumu mno,,,,,wanafurahia kushona suti za kuapishiwa ila ugumu wake unakua hapa,,,,,dr Mwinyi alipoapishwa alisema ataanza na tatizo la madaktar,ila limemshinda maskin nae anaandamwa na sakata la mabomu,na nna imani litalipuka kikao kijacho,na kuna watu watafukuzwa tena bungeni,,,,kuna wizara kadhaa zitaleta kizungumkuti
  -afya,
  -mambo ya ndani
  -ulinzi
  -viwanda na biashara,lets wait
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ukuu mtamu sana aise watu hawako tayari kuachia madaraka
  Ni bahati mbaya kauli imemtoka Lissu ila kwa kweli alistahili kuitoa
  maana mtu anaposhindwa jambo ambali alipaswa awe na suluhisho lake kinachofuata ni kuachia ngazi
  Ila kwa kuwa hatuna utamaduni huo sasa haya ndo matokeo yake kuzungumzia mambo ya heshima sijui nini
  Ukweli unauma na mtu anapokuambia ukweli wako huna la ziada zaidi ya kulikubali ila kwa PM kukubaliana na ukweli ni ngumu sana
   
 13. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

  Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
   
 14. a

  akelu kungisi Senior Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tundu Lisu was right! Sasa amekosea wapi? Lugha ya maudhi iko wapi hapo? Cha ajabu Bi Mkora kama kawaida yake amesapoti ujinga ati Lisu alipotoka kumuuliza swali lile! PM ameshindwa kutatua mgogoro sasa kwa nini asijiudhuru? Haya mambo yatawarudi CCM muda si mrefu! Huo ni ujinga!
   
 15. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mbali ya kushindwa kushughulikia tatizo la mgomo wa madaktari kuna kadhia zingine nyingi tu zinazostahili kuwajibika kwake na kujiuzulu............ameshaprove mara nyingi jinsi alivyo incompetent
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,885
  Likes Received: 83,367
  Trophy Points: 280
  Yeye na DHAIFU wameshindwa kutatua ufisadi wa EPA, Rada, Kiwira, Kupanda kwa gharama za maisha, mgomo wa madaktari n.k. kwa kifupi kazi ya kuongoza nchi imewashinda...sasa wanangoja nini kujiuzulu!?
   
 17. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Yuko kama wale vijana wake wa TISS.........very sloppy, hata kujipanga hawajui
   
 18. K

  Kailanga Senior Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alishindwa kujizuia on this, he was so immotional!
   
 19. MALUNGU

  MALUNGU JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  mfano kulia bungeni 2009, "liwalo na liwe" jana na madudu kibao ambayo anakosa maamuzi.
   
 20. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Lissu: If you have done everything in your power and failed why dont you resign?'
  Pinda: Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana umri umesogea unataka nikafie huko kijijini nini? kwa taarifa yako hata mpige mayowe sitoki wewe hujui spika yupo nyuma yangu mfano halisi si uliona vile visahihi vyenu na Zito viilishia wapi au nikuwekee uso wa mbuzi?
   
Loading...