Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,321
- 219,633
Akihutubia Umati wa wananchi huko Tabora , Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu anesema kwamba viongozi wanaoongoza Tanzania kwa sasa hawawatetei wananchi kwa vile hawakupigiwa kura.
Akizungumza kwa kujiamini huku akitoa mifano kadhaa iliyo hai mbele ya Mwenyekiti wake Mbowe na Mbele ya umati wa Wananchi wa Tabora, Lissu amedai kwamba kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na ule wa madiwani, Wabunge na wa Rais 2020, hakuna kura yoyote aliyopiga mwananchi iliyotoa kiongozi. Wote mnaowaona walipita bila kupingwa au walitangazwa tu.
Lissu amedai kwamba hata ukimuuliza Dr. Samia leo atutajie idadi ya kura za Urais ambazo yeye na Magufuli walipata 2020 hawezi kuzitaja kwa sababu hakuna mahali popote zilipoandikwa.
Amesisitiza kwamba Viongozi ambao hamkuwachagua hawawezi kuwa na uchungu na nyinyi, ndio maana hawawatetei na wanawatwanga tozo za kufa na kupona.
Toa Maoni yako.