Tundu Lissu: Wabunge wa kupewa siyo Wabunge wa Wananchi, tusikubali Majimbo ya kupewa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,148
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu anesema Ubunge wa kupewa kwa makubaliano fulani siyo Ubunge wa Wananchi.

Mbunge wa Wananchi ni yule aliyeshindana na kushinda kwa kura halali ambaye Waliompigia kura na Wasiompigia kura Watamuheshimu kwa sababu ya Uhalali wake, amesema TAL.

Lissu amewataka wenzake waache kucheka cheka kwa kuachiwa Majimbo kwani mbele ya Wanaccm wanaonekana hawana akili.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Naunga mkono 100% hicho alichosema Lissu, tatizo naona anasemea mahala pasipo sahihi, na hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa..

- Amejaribu kimya kimya kuwaamsha wenzie chamani lakini hawakuonesha dalili za kumuelewa, hivyo ameona kuliko aendelee kuwapigia mbuzi gitaa, bora akaongee na wananchi.

- Anatafuta umaarufu, kutaka kujiweka juu ya wenzake chamani, na kujitofautisha nao.

Kutofautiana mawazo na wenzako sio kosa, lakini kosa ni pale unapoamua kutoka nje na kuropoka hovyo [ ndio ni kuropoka hata kama kile unachosema kina mantiki, lakini hukisemei sehemu sahihi], huo sio ustaarabu, sio utaratibu, na pia unakuonesha ulivyokosa uvumilivu.

Nakumbuka Lema nae alikuwa na doubt na maridhiano, mpaka akafikia stage ya kumtaka Mbowe ajitoe huko, leo Lema yupo kimya, nini kilimtokea kama alikalishwa chini na wenzake akaeleweshwa akawaelewa I don't know.

Kwa Lissu inaonekana his situation is tense, na inawezekana hata ile safari yake ya kwenda Ubelgiji kwa ajili ya kumuona daktari ulikuwa ni mpango wa kupooza mambo, bahati mbaya amerudi na kukuta hali ya mambo bado haieleweki sasa ameamua kufunguka..

Hiki alichosema Lissu inawezekana pia kikawa na ukweli hasa nikiunganisha mambo kadhaa, kuanzia kwa Tulia kule Mbeya kutaka jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe, mpaka kwa Sugu kusema kwa kujiamini atamfuata Tulia popote atapokwenda, naona kujiamini kule kunaweza kuwa kumesababishwa na hii kauli aliyoitoa Lissu kuhusu kupewa majimbo.
 
lisu kashaona dj anayoyafanya ni haramu kwa wananchi! aache asali apiganie wananchi.
 
Katika nusu mkate aliopewa mbowe, lissu hajamegewa hata silesi moja ndo chanzo ya kelele hizi.
 
Tunataka KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Serikali ya UMOJA w kitaifa haitafanikiwa bara.

Maridhiano ni Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi baaas, uhuni wa kina Sugu kuchekelea kugaiwa majimbo ukome.

Hamna Cha Bure duniani.
 
In all fairness, aliumia kupigania alichokuwa anakipigania...nimeona Taarifa ya Mzeee Bwana Tundu kuliona Gari alilokuwamo wakati wa mashambulizi. Apewe mda labda ametoneshwa, maana hii mikiki mikiki ya kauli zake sasa Mhh 'Ahhhh'

Nikirudi kwenye Mada, nitagusa kule kule nilipoona kuna walakini- Maridhiano! Wafungue pazia basi naye achungulie, manake kama atakuwa hana usemi huko, ataendelea kujisemea semea majukwaani. Lissu ana hoja! Haya ya majimbo nayo nimeyakataa, yawe ji majimbo ya Kugawa au Majimbo ya Utawala. Tusikubali.

Huu Udikteta wao, utawakosti mpaka 2035 na wanaweza, vinginevyo kumletea wakati mgumu SSH na vurugu asiyotegemea.
 
Naunga mkono 100% alichosema Lissu, tatizo naona anasemea mahala pasipo sahihi, na hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa...
Nje ni wapi?

Watanzania Wengi ni wajinga hawaelewi kuwa hivi vyama vya Siasa ni mali ya Umma havina umiliki Binafsi

Tundu Antipas Lisu ameongea kwa Watanzania wote kwani Ubunge wa kupewa hauishii Chadema tu

CCM kwenyewe kuna waliopewa Ubunge ndio hao wanaolia na kuvua nguo bungeni

Ubunge ni Mali ya Wananchi ndio sababu kwenye Katiba mpya tunataka kifungu cha Wananchi Kumfukuza mbunge akizingua!
 
Nje ni wapi?

Watanzania Wengi ni wajinga hawaelewi kuwa hivi vyama vya Siasa ni mali ya Umma havina umiliki Binafsi..
Vyama vya siasa vina sheria na taratibu zake, vile sio vikundi vya wacheza ngoma wa mitaani, na ili ukubaliwe kuwa mwanachama wake lazima ukiri kufuata sheria na taratibu za chama husika.

Suala la chama cha siasa kuwa mali ya umma lina maana kwamba, kila mtanzania mwenye sifa anaruhusiwa kujiunga navyo, lakini sio vyama kuwa mali ya umma ndio kila kiongozi wake ajiropokee tu mambo ya ndani mitaani, huo ni uwendawazimu.
 
Vyama vya siasa vina sheria na taratibu zake, vile sio vikundi vya wacheza ngoma, na ili ukubaliwe kuwa mwanachama wake lazima ukiri kufuata sheria na taratibu za chama husika.

Suala la chama cha siasa kuwa mali ya umma lina maana kwamba, kila mtanzania mwenye sifa anaruhusiwa kujiunga navyo, lakini sio vyama kuwa mali ya umma ndio kila kiongozi wake ajiropokee tu mambo ya ndani mitaani, huo ni uwendawazimu.
Mtaani ni wapi?

Kufichaficha mambo ni Ujinga wa Chadema tu kwa sababu mnaoamini hicho chama ni mali ya Mtei& Family

CCM wanaelezana kila hatua ya Maridhiano na hata wale Covid-19 wanajua kila kinachoendelea lakini hapo Ufipa st Freeman Mbowe Peke yake ndio katunza siri

Ujinga wa Chadema wanasahau kuwa Makatibu Wakuu wao wote ni Vipenyo
 
Rais anayehonga upinzani wabunge hawezi kemea rushwa na ufisadi maana na yeye anaufanya.

Tusahau kuchukuliwa hatua waliohusika katika ripoti ya CAG maana si ajabu nae anahusika.
 
Naunga mkono 100% hicho alichosema Lissu, tatizo naona anasemea mahala pasipo sahihi, na hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa..

- Amejaribu kimya kimya kuwaamsha wenzie chamani lakini hawakuonesha dalili za kumuelewa, hivyo ameona kuliko aendelee kuwapigia mbuzi gitaa, bora akaongee na wananchi.

- Anatafuta umaarufu, kutaka kujiweka juu ya wenzake chamani, na kujitofautisha nao.

Kutofautiana mawazo na wenzako sio kosa, lakini kosa ni pale unapoamua kutoka nje na kuropoka hovyo [ ndio ni kuropoka hata kama kile unachosema kina mantiki, lakini hukisemei sehemu sahihi], huo sio ustaarabu, sio utaratibu, na pia unakuonesha ulivyokosa uvumilivu.

Nakumbuka Lema nae alikuwa na doubt na maridhiano, mpaka akafikia stage ya kumtaka Mbowe ajitoe huko, leo Lema yupo kimya, nini kilimtokea kama alikalishwa chini na wenzake akaeleweshwa akawaelewa I don't know.

Kwa Lissu inaonekana his situation is tense, na inawezekana hata ile safari yake ya kwenda Ubelgiji kwa ajili ya kumuona daktari ulikuwa ni mpango wa kupooza mambo, bahati mbaya amerudi na kukuta hali ya mambo bado haieleweki sasa ameamua kufunguka..

Hiki alichosema Lissu inawezekana pia kikawa na ukweli hasa nikiunganisha mambo kadhaa, kuanzia kwa Tulia kule Mbeya kutaka jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe, mpaka kwa Sugu kusema kwa kujiamini atamfuata Tulia popote atapokwenda, naona kujiamini kule kunaweza kuwa kumesababishwa na hii kauli aliyoitoa Lissu kuhusu kupewa majimbo.
Lisu yupo sahihi. Vinginevyo msipigie kelele ubunge waliopewa kina Halima na Wenzake
 
Mtaani ni wapi?

Kufichaficha mambo ni Ujinga wa Chadema tu kwa sababu mnaoamini hicho chama ni mali ya Mtei& Family

CCM wanaelezana kila hatua ya Maridhiano na hata wale Covid-19 wanajua kila kinachoendelea lakini hapo Ufipa st Freeman Mbowe Peke yake ndio katunza siri

Ujinga wa Chadema wanasahau kuwa Makatibu Wakuu wao wote ni Vipenyo
Wapo wengi waliowahi kuadhibiwa na vyama vyao kwa sababu ya kuropoka hovyo nje ya vikao, wewe hapa nakuona umetawaliwa na mihemko, hebu tulia kwanza.
 
Wapo wengi waliowahi kuadhibiwa na vyama vyao kwa sababu ya kuropoka hovyo nje ya vikao, wewe hapa nakuona umetawaliwa na mihemko, hebu tulia kwanza.
Hao walioadhibiwa ni wajinga tofauti na Mwanasheria nguli Tundu Antipas Lisu!
 
Lisu yupo sahihi. Vinginevyo msipigie kelele ubunge waliopewa kina Halima na Wenzake
Sijakataa mantiki ya usahihi wa hoja ya Lissu, napingana na mahali anapotolea hoja yake, tuelewane hapo.

Ubunge wa kina Mdee una matatizo mengi, lazima upigiwe kelele.
 
CCM wanaelezana kila hatua ya Maridhiano na hata wale Covid-19 wanajua kila kinachoendelea lakini hapo Ufipa st Freeman Mbowe Peke yake ndio katunza siri
Sasa kama CCM wanaelezana na hata Covid19 wanajua, iweje uendelee kuiita kuwa ni 'siri' inayotunzwa na Mbowe?
 
Back
Top Bottom