Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hana sifa za kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.

Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.

Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.

Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.
Mhe T.Lisu ni mwanaharakati mwenye uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko popote. Anafanya hata zaidi ya uwezo wake. Watu wa aina yake hawafai kua viongozi wakubwa ( raisi ) sababu wapo tayari kufa kutetea haki iliyopotea ila hawaoni wanapokisea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That's true
 
Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.

Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.

Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.

Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.
Uko sahihi kabisa kiongozi ! angalia mahojiano yake na watanzania waishio marekani kwa u tube kikweli hana maturity ya kutofautina ,hili tatizo ndo linamtesa sana magufuli anapenda sana kusifiwa ,nikupongeze umeona tunahitaji raisi asiependa sifa na live tv na mfanyabiashara sio huyu mkulima (no hard feelings ),Ila nilichokipenda kwako wakati tunajaribu kutokosea tusikosee zaidi mimi kwa mtazamo wangu bado sampuli ya lowassa inahitajika (simaanishi lowassa) watu wenye hekima ,utulivu na busara

Huyu ni mwanaharakati bora na mbunge makini abaki hivyo.
 
Back
Top Bottom