tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,788
- 4,490
Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.
Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.
Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.
Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.
Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.