Tundu Lissu awasili salama Ubelgiji

Tundu Lissu awasili salama Ubelgiji

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,614
Reaction score
287,331
Mhe. Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, amefika salama nchini Ubelgiji baada ya kuondoka nchini Tanzania ambako alikuwa Mgombea Urais aliyeng'ara kutokana na maisha yake kuwa hatarini baada ya Vitisho vikubwa vya kumuua, aliondoka nchini Tanzania kwa Ulinzi wa UN huku akisindikizwa na mabalozi watatu, Balozi wa Marekani, wa Ujerumani na wa Ubelgiji.

Subpost 2 - HABARI_ Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Cha ( 336 X 640 ).jpg
Subpost 1 - HABARI_ Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Cha ( 333 X 640 ).jpg


Picha hizo ni za Zaventen Airport, Brussels Belgium alipowasili .
 
Wewe acha uongo. Ndiyo maana unaweka uzi na ku comment mwenyewe. Mnaanza kumpa sifa za uongo eti mgombea aliyeng'ara. Kupata 12% ndiyo kung'ara? Eti alisindikizwa na UN.

Uongo mtupu. Kwa taarifa yako hakuna UN wala balozi hata mmoja aliyemsindikiza. Unaowaita mabalozi ni maafisa wadogo sana.
 
Wewe acha uongo. Ndiyo maana unaweka uzi na ku comment mwenyewe. Mnaanza kumpa sifa za uongo eti mgombea aliyeng'ara. Kupata 12% ndiyo kung'ara? Eti alisindikizwa na UN. Uongo mtupu. Kwa taarifa yako hakuna UN wala balozi hata mmoja aliyemsindikiza. Unaowaita mabalozi ni maafisa wadogo sana.
 
Eti Ni Yeye... Watanzania nawaaminia sana, mtu kakaa huko kakuta barabara, vituo vya afya kibao, ma fly over,reli na wananchi wanafurahia eti anawahubiria "Tunataka maendeleo ya watu sio vitu", wananchi wakamchekiiii wakamsubiri kwenye box la kura.

Kuhakikisha hilo alivyoshindwa uraisi akataka waingie barabarani maandamano bila kikomo wananchi wakakausha, alivyo na mkosi hata Robert Amsterdam baada ya uchaguzi kamtelekeza kaacha kutoa zile barua za mikwara.

Aliyekuja kuimaliza kabisa CHADEMA ni Lissu na tukiwaambia humu, mkakazania "NI YEYE", Vipi zile nyaraka alizokuwa anaandaa Amsterdam za kupeleka ICC ziko wapi?,.. Siku zote nasema humu Lissu ana akili nyingi sana za darasani Ila Elimu ya Dunia ni ZERO kichwani mwake. Asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na ulimwengu.

Kutoka kuwa mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani hadi kuwa mkimbizi. Wabongo mnaona ukimbizi dili kutokana na maisha ya bongo, ila ulaya wakimbizi hasa wanaolishwa na serikali zao wanaonekana mafala tu, status ya Lissu huko hana tofauti na wakimbizi wa Somalia.

Kule anaonekana fala tu, story za Ni Yeye hawana habari nazo, Belgium wamejaa mafala kibao kama yeye kutoka Congo,Rwanda, Burundi nk wakisubiri ela ya kujikimu kila mwezi na ndo janja yao imefika mwisho. Huko game tough asikwambie mtu.
 
Wewe acha uongo. Ndiyo maana unaweka uzi na ku comment mwenyewe. Mnaanza kumpa sifa za uongo eti mgombea aliyeng'ara. Kupata 12% ndiyo kung'ara? Eti alisindikizwa na UN. Uongo mtupu. Kwa taarifa yako hakuna UN wala balozi hata mmoja aliyemsindikiza. Unaowaita mabalozi ni maafisa wadogo sana,. Sema amerudi kwa mabwana zake baada ya plans zake kubuma. Namhurumia atakavyofanywa
Kwani hatumjui huyu kamanda uchwara? Yaani Lissu alipokelewa na umati alipokuja Dar lakini siku ya kusepa hakuna cha Mbowe wala nani aliyemsindikiza. Kasambaratisha lichama lote la ufipa na kuwaacha makamanda kwenye mataa. Ni majonzi na huzuni hapo ufipa kwa sasa.
 
Hakuna mtu aliyemtishia Lissu maisha yake.

Baada ya kushindwa uchaguzi ilikuwa lazima atengeneze drama ili kuwalaghai wafuasi wake kuwa analazimika kuondoka nchini.

Yeye sio mpinzani wa kwanza kugombea Urais na ni mpinzani runner up aliyepata mafanikio madogo kuliko wapinzani wote tangu nchi yetu ianze kuwa na chaguzi za vyama vingi.
 
Back
Top Bottom