Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

Hili linatakiwa lifanywe na Zitto atakapohitimisha hoja yake. Aweke motion ya kutokuwa na imani na serikali kisha wabunge wa CDM wasibweteke wasimame kuunga mkono tuone kama magamba wataunga mkono? na wananchi waone nani kweli anawatetea.

Naamini Zitto is one of good members wa hapa jamvini, otherwise, kwa wale wenye contacts zake kama e-mail mobile number etc wamjulishe haraka kuhusu hii idea inawezekana jamaa akawa very busy na isiione hii comment hadi siku ambayo atakuwa anafunga mjadala! Please please wadau this is very importnat kujua nani ni mnafiki na nani mkweli!
 
jamani tupeni nukuu za tundu lisu alizosema,bado hatuja wapata vizuri wengine tuko mbali nna bunge
 
Kama kweli wabunge wana uchungu na wanawakilisha wananchi basi wanapaswa kumuunga mkono Tundu Lisu. The guy has a valid point na kweli anaitetea nchi yake kama mbunge na mwanasheria wa kweli!
 
alicho nena MP Lissu ni cha msingi ila kwa kuwa watz ni wabishi na hatujui nini tufanye na kwa wakati upi.
 

Isingekuwa kuwa njama za CCM kumweka Tundu Lisu kwenye kesi ambazo hazina msingi, angekuwepo tangu tarehe 10 Aprili basi hadi leo kingekuwa KIMEELEWEKA.

Kudos Tundu Lisu!


Ulishindwa ubeberu na ufisadi nao utashindwa. Tutaenda na Mungu na kumaliza na Mungu.
 

Kwa kweli amefanya kweli! Tunataka wabunge wasiouma maneno bali wanayatema mazimamazima maana serikali yetu ni kiziwi. Kwa hiyo, mtu anyeumauma maneno haiwezi kusikia.
 
Wengi walioko serekalini wanatumikia matumbo yao na wale walioko juu yao, hawaitumikii nchi. Wako radhi waue ili washibe wao na familia zao. Wabunge hawa hawana uwezo wowote wa kuinyooshea kidole serekali kwa sababu wakiinyooshea hawamtumikii bosi wao raisi na mwenyekiti wa chama chao. Kwa hiyo ni heri maisha yaende kama yalivyo, wananchi waumie lakini wao na familia zao waendelee kumridhisha bosi wao.
 
Kauri thabiti ya umma ni 'Watanzania wote hatuna imani na serikari', haya wabunge malizieni tuanze upya.
 
Wanachokifanya wabunge wa CCM kurudisha imani kwa wananchi kwa kuwadanganya/kuwazuga kuwa wanakemea mambo hayo lakini waelewe kipofu akishajua anakula na mwingine anakuwa makini sana. Hizo ni mbinu tu wameibuka nazo ili waokoe CCM hata hao wanaohama kutoka CCM hakika kuna malengo yao yakitimia wanarudi lakini ifike mahali wakubali mwisho wa jambo ukifika hata ufanye nini huwezi zuia ni kifo cha kawaida kila kitu au mtu anakipata baada ya muda wa ktumikia jamii ukikamilika. nasema ASILAUMIWE YEYOTE CCM KUFA NI KIFO CHA KAWAIDA TU! PIA WANANCHI WAELEWE RIZIKI KUGAWANA SI KILA SIKU UTAPATA WEWE TU TUJIFUNZE! NI WAKATI CHAMA MAKINI KIONGOZE!
 
WanaJF hao wabunge wa magamba si kuwa wana uchungu kweli ila wana test zari maana wanajua Tv hata kule Misenyi zipo hivyo wanajikomba kwa wapiga kura ili waonekane wamesema neno ndani ya mjengo. Lakini nawaambia hiyo haitoshi kama wamesema na tumewasikia na wanaona kuwa serikali yao sio sikivu basi kuna njia sahihi mbili tu, wachague moja kujiuzuru ubunge au waiwajibishe serikali yao kwa maslahi ya umma.
 

I appriciate...
Kwa hoja kama zako zisizo egemea chama na kuwa na nia ya kujenga na Kuikosoa Serikali yoyote isiyokidhi matakwa ya wananchi..
Hata mwezi hautofika kuitoa serikali iliyoko madarakani..
Keep it up..
 
Ndiyo maana nasisitiza kwenye kauli zangu kuwa Tanzania ya kweli itajengwa na wenye uchungu na nchi hii.
 
Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?

changa la macho hilooo.
 
Daah! patamu hapo! jamaa saizi wanatoka moshi tu kwenye masikio!! ha ha ha!
 
haya magamba yameshaona kuwa ccm haina chao 2015 kwa hiyo yanatumia theory ya "chukua chako mapema"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…