Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

Hahaha mtu anasema fulani ni dikteta mara kuna ukiukwaji wa haki za binadamu wakati anayasema hayo akiwa huru hah ash ash a yani mtu awe dikteta halafu akuruhusu kumuhita dikteta? Hahahahaha

Mi nasubiri nione jinsi hayo mataifa yatakavyo msusuia Magufuli...
Sasa Lissu kuwa huru ndiyo kigezo kwamba nchi haiongozwi na Nduli???


Ili kujibu hizi hoja za Lissu inabidi CCM muite kikao kikuu cha chama mjipange.
 
Mkuu hakuna ubaya wowote ule nawe ukashare nasi Watanzania approach ambayo itafaa kupambana na huyu dikteta uchwara.

Sioni tatizo lolote lile kuwa na 2 approaches za kumpinga huyu au hata zaidi na zote zikatumika kwa wakati mmoja Mkuu.

Hii ina watu zaidi ya millioni 50...miongoni mwao wanasiasa ni kundi dogo sana...na kundi kubwa ni la wananchi ambao ndio watawaliwa......ambao kwa namna moja au nyingine ndio waathirika wa kwanza wa maamuzi ya wanasiasa kwa namna moja au nyingine.......

Kimsingi ni kuwa serikali ya CCM ilishashindwa kuwatumikia wananchi kwa kuwaahidi mambo yale yale ambayo wameshindwa kuyatimiza.....

Lakini hebu tujiulize ni kwanini CCM bado wapo madarakani.......ni kwanini bado inashinda kila chaguzi.....!!? Pamoja na tuhuma zote za rafu kwenye chaguzi mbali mbali za ndani na nje ya chama ni dhahiri kuwa kuna tatizo kwa wananchi.....

Tatizo kubwa ni kuwa wananchi hawajitambui na hawatambui stahiki zao kutoka kwenye serikali yao waliyoichagua wenyewe.........

Wananchi bado hawajui maana ya uchaguzi au thamani ya kipande cha karatasi anachotumbukiza kwenye sanduku la kura kumchagua kiongozi.....

Ni wananchi wachache sana wanaojua hata mistari miwili ya katiba achilia mbali maana ya katiba.....

Kumbu kumbu zinaonyesha kuwa sehemu nyingi palipotokea maandamano ya kimageuzi ni kutokana na wananchi kutambua haki zao na stahiki zao kwa serikali yao ambapo itapelekea wao kudai stahiki zao kutoka kwa serikali yao pindi watakapoona zinakiukwa.......bila hata ya kusikia ya mwanasiasa........

Wanasiasa wabadili approach yao ya kukabiliana na mfumo moja kwa moja badala yake wawekeze kwa wananchi waweze kutoka usingizini.......waawaamshe wajibu haki zao kwa serikali yao....wajue stahiki zao kwa viongozi wao.....wajue kuwa viongozi hawapaswi kuabudiwa bali kutumikishwa na wao.......

Wajue kuwa hii nchi ni ya kwao na wao ndio wenye kujenga au kubomoa nchi yao........

Hizi kelele za wanasiasa tumeshazizoea na hazina mafanikio tangu zianze.....

a0bf5e561c6dbfd15311bd881c98b32f.jpg
5bf3bd66a4632eb707cd69fd6bb600ba.jpg
ddd3f2e3b8ec1c910bbbb920926808c9.jpg
46f7d7386e24c28479d154d9880ea149.jpg
571d84e376f4346dfd75b44593712513.jpg
 
Magufuli ameshajulikana kuwa alikua anachukia mafisadi kwasababu alikosa nafasi ya kufanya ufisadi.

Sasa na yeye ameanza ufisadi rasmi kuanzia Chato International Airport pesa zinaidhinishwa na mpwa zinapigwa juu kwa juu.
Chato iko Tanzania kama ilivyo Dar es Salaam ambayo imekuwa ikiboreshwa, mara kwa mara, kwa fedha hizo hizo za WaTz.
 
Mkono mtupu haulambwi. Kama huwezi kumjali uliye karibu nae utaweza kumjali aliye mbali!

Hata Biblia inahimiza upendo nguzo kuu ni kujipenda kwanza - mpende mwenzio kama unavyojipenda wewe. Wenzetu husema charity begins at home.

Hata mimi nakuunga mkono kwa hilo, ila kweli kulikuwa na ulazima wa kujenga uwanja mkubwa wa ndege wa kiwango hicho kwa sasa? Hao watu wa huko kijijini kwake ni wangapi wanaweza kupanda ndege kwa wakati tulionao? Unaweza kutetea kwani ni wajibu wako lakini hata wewe binafsi unajua hiyo haijakaa poa.
 
ipo wapi pesa ya viwanda? Pesa ya kivuko, zile bilion 251 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa, zipo wapi 10% ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli, ukarabati wa bandari na ujenzi wa uwanja wa ndege chato? Mikataba ilipelekwa bungeni kujadiliwa? au mpaka aje Rais wa awamu ya 6 ndiyo afumue hizo skendo? CCM wamekula pesa za chenji ya Rada, chenji Bunge la katiba na mapesa mengineyo mengi lakini leo hii wanajidai kuwahadaa watanzania kwa kudhani watanzania ni wajinga kiasi hicho.
 
TAKUKURU kuhusu Lugumi kimyaaaa! Halafu tunazugwa na huyu dikteta uchwara eti anapambana na mafisadi! Labda huyu naye ana kinga kwenye katiba kwamba hawezi kushtakiwa kwa makosa yake
 
Democracy Dies In Darkness—Done In By Ignorance And Apathy
Politically ignorant citizens care a lot about what government does to hurt or help them, but apathy creeps in when we feel powerless.
Knowledge is deeper than the ocean and wider than the sky. There is always so much to learn. So always keep your mind open to learn new things and you will find yourself everyday becoming wiser than yesterday.
 
Wazungu wako makini sana wana msemo scratch my back I scratch yours. Huwezi singizia unamtetea mzungu halafu unaenda kumwomba rushwa ili umtetee bungeni kwenye madini nk Chadema wakitaka hao wazungu wawatetee wao si waliwapa cash? Wao wanawapa Cash shilingi ngapi? Tundu put a price tag here. Hawawezi kufanya uzalendo wakati nyie You put a Price tag
Mkuu hatudanganyiki japo sie ni wadanganyika

Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
 
kazi ya Upinzani ni kumkosoa Rais na timu yake lakini cha ajabu Serikali hii ya awamu ya 5 wakikosolewa hukaa vikao usiku nyumbani kwa Bashite na kupanga mipango ya kuwabambikia watu Kesi na kuwakomoa. Hawataki kujifunza wajirekebishe wanatumia pesa nyingi kwa kuandaa Kesi kesi kesi na uonevu wa kila Aina.
Kazi Ya upinzani sio kufanya kazi ya pepo la upinzani ni kupongeza pale serikali ikifanya vizuri pale wanadhani ndivyo sivyo kutoa ushauri mbadala kwa hekima na upole kazi ya upinzanl sio kufanya kazi za ibilisi za kuwa mshtaki au accusser of the brethren Tanzanians Kama ambavyo biblia inamwelezea shetani kuwa always kazi yake ku kupinga na kua accuse. Upinzani wana mapepo ya upinzani
 
Vuvuzela huyu tumemzoea. Hata kwenye makinikia alisema tutanyolewa bila wembe na wenye makinikia badala yake wakapanda ndege kuja kuomba tuongee!! Sasa anatafuta kick nyingine kama anataka tususiwe na mataifa si angewafuata hukohuko hao mabwana zake??
Umelipwa makinikia? Kikao cha pamoja kiko wapi na wanaume wa acacia? Tujaribu na kudodosa huku pia juhudi nzuri ee haya

Sent from my ALE-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Vyama vya siasa havijapigwa marufuku Tanzania.

Vyombo huru vya habari havijapigwa marufuku Tanzania.

Hakuna waandishi wa habari waliopo kifungoni kwa kuandika mambo yasiyopendezwa na serikali iliyopo madarakani.

Tanzania hatupo chini ya utawala wa kijeshi.

Tanzania hatuna wafungwa wa kisiasa.

Tanzania hatuna wakimbizi wa kisiasa waliokimbilia nchi zingine wakiogopa kufungwa au kuuliwa.

Sasa, kama hayo machache niliyoyaorodhesha yapo Tanzania hii basi tunastahili kususiwa.



Katiba iliyopo, licha ya mapungufu yake, inazuia hayo ya kusababisha tususiwe, kutokea.



Tanzania hatuna ukiukwaji wa haki za kibinadamu ulio wa kimfumo.

Kama mnadhani upo, basi pelekeni malalamiko yenu huko AU.

Pelekeni malalamiko yenu huko UN.

Pelekeni malalamiko yenu huko The Hague.

Fanyeni mikutano na waandishi wa habari wa vyombo vya kimataifa kama CNN, BBC, Reuters, Xhinua, AP, ABC, CBS, NBC, SKY, ITV, Al-Jazeera, na vinginevyo ili muitanabahishe dunia kuwa Tanzania imeharibika na kwamba inastahili kususiwa.

Halafu tuone mtafika wapi. Msiishie kulialia JF tu na kwenye vi video vya kwenye YouTube huko.

Hivyo vyote ulivyotaja hapo juu mpaka sasa vimefikia 70% ila ni uwoga ndio unawafanya watu wasipaze sauti. Sasa kwa watu kama kina Tundu Lissu kwa kuliona hilo ndio wameamua kutumia haki yao ya kikatiba kuonya kuhusu hilo. Hayo mashirika ya kimataifa mengi yamesha toa ripoti ya hali hiyo sasa ni suala la muda tu. Kwani kina Kagame, Museveni, Nkurunzinza nchi zao zinaongozwa na jeshi? Lakini hiyo inamaanisha viongozi wao sio madictator? Sasa hivi chombo gani cha habari kinathubutu kuripoti taaarifa itakayoudhi serekali hata kama ni kweli? Magazeti mangapi yamefungiwa kwa kuandika habari za ukweli lakini zisipondeza utawala?
 
Back
Top Bottom