PreGE2025 Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imepigwa kalenda hadi Aprili 24, 2025.

Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 3 ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

Ukiondoa kesi ya Uhaini, Lissu anashtakiwa pia kwa makosa mengine matatu:

1. Kuchapisha taarifa za uongo: Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 uliharibiwa kwa maelekezo ya Rais (YouTube)

2. Kuchapisha taarifa za uongo: Polisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi. (YouTube)

3. Kuchapisha taarifa za uongo: Majaji ni wa CCM hawawezi kutenda haki, ni wateule wa Rais wanataka uteuzi wa majaji wa rufani. (YouTube)




Soma Pia:

==============
Mashtaka matatu aliyosomewa Tundu Lissu kwenye Kesi ya nyingine baada ya kesi uhaini

Mbali ya kufunguliwa kesi ya uhaini, April 10, 2025 pia Tundu Lissu alifunguliwa kesi nyingine ya jinai yenye mashtaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo.

1. Shtaka lakwanza, ilielezwa kuwa April 3, 2025 katika Mkoa na Jiji la Dar es salaam Mshtakiwa alichapisha taarifa za Uongo kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa -2024 Wagombea wa CHADEMA walienguliwa kwa maelekezo ya Rais huku akijua ni uongo.

2. Katika shtaka la pili, ilielezwa kuwa April 3, 2025 mshtakiwa alichapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa Polisi wa Nchi hii wanatumika kuiba kura huku akijua kuwa ni uongo.

3 Katika shtaka la tatu, ilielezwa kuwa Aprili 3, 2025 mshtakiwa alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa Majaji wa Nchi hii ni CCM na hawawezi kutenda haki kwa kuwa wanapenda kuteuliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani.



Pia soma ~ Adhabu ya uhaini Tanzania siyo lazima kifo
 
Good Trouble!
~John Lewis (American Civil Rights Leader)
 
Lissu alisema anataka siasa ngumu, na kwamba Mbowe ni laini, haya, hakusikia mausia ya mzee wa siku, Mr. Mbowe, ameona mengi. Mbowe anawajua watanzania ndio maana aliachana na siasa za mapambano.
Watanzania sisi ni waoga ndio maana uoga wetu ni dili za watu,tuendelee kuvumiliana na kujipanga upya kimaisha
 
Jeshi la polisi inabidi lifumuliwe waajiriwe watu wasomi, mtu hata akipewa order awe na uwezo wa ku reason anachoambiwa, sio Kila ukiambiwa Fanya hivi unakimbia tu
No sheria zinazo govern hiko chombo ni outdated, no longer serve modern society
 
Jeshi la polisi inabidi lifumuliwe waajiriwe watu wasomi, mtu hata akipewa order awe na uwezo wa ku reason anachoambiwa, sio Kila ukiambiwa Fanya hivi unakimbia tu
Msingi wa kutofanya reasoning ya order katika hizi units ndio kuita Nidhamu na utii 🤣🤣🤣 Ukipewa Amri ya Shambulia adui mbele yako utaenda kuijadili vichakani huko
 
Safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…