Tundu Lissu anawatisha nini CCM?

Tundu Lissu anawatisha nini CCM?

Kwa hili la kutetea wezi namshangaa sana Tundu Lissu hata CCM watamshangaa tu
Hivi Lisu anewateteaje wezi? Na je hao mnaowaita wezi, mlikuwa hamjui kama ni wezi? Na je ninani aliyewakaribisha hawa wezi? Wakati mnapitisha mikataba kwa mbwembwe mlikuwa hamjui kama ni wezi? Tundu Lisu alijitahidi sana kupinga hiyo mikataba pamoja na wenzake, mkasema wapinzani hawataki maendeleo, leo Lisu anawapa tahadhari na kuwambia kuwa wizi mkubwa upo migodini na si kwenye mchanga, mnasema anatetea wezi. Hivi kweli nyinyi CCM wa humu mtandaoni ni wazima kweli?
 
Tulia uone CCM mpya ya wazalendo inavyoogopa na kuwachukia wasaliti
kila mwaka hii kauli mnaitoa tu ila mwisho wa siku pale lumumba mnanyooshwa tu ahahaha





Buku 7 hazitomuacha mtu salama
 
Ha ha ha ha Lissu noma sana hatari sana alimuuliza maswali shahidi wa lile zee la Bunda hadi akaomba maji ya kunywa mahakamani,yaani mimi naunga mkono mtu/chama/kitu au taifa lolote linalopinga MA CCM hata kama ni KENYA yaani siyapendi haya majitu wacha Lissu aendelee kuyanyima usingizi safi sana ngoja j3 tusubirie hiyo rubbish nyengine
 
Hiki kiwewe cha CCM dhidi ya Tundu Lisu kinatokana na nini hasa? Aliposema kwamba anagombea Urais wa TLS timu nzima ya CCM kuanzia Mwenyekiti wao wa taifa ikawehuka. Wengine tukajiuliza kwani TLS imeanza wakati Lissu anatangaza kugombea huo Urais wa TLS?

Wakati wa kupitisha Mswada wa Sheria ya Habari tulishuhudia bunge likiendeshwa hadi usiku sana huku wabunge wa CCM kama vile walikuwa wamejifunga kibwebwe dhidi ya Lissu. Hadi wengine tukapata hofu kwamba labda huenda Lissu anamiliki chombo cha habari ambacho sheria husika ikipitishwa basi serikali itafaidika kwa kukifuta chombo hicho.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 inasemwa kwamba Jakaya Kikwete alipata kusema ni heri watu wa Jimbo la Lissu wasimchague yeye kuwa Rais lakini pia wasimchague na Lissu kuwa Mbunge. Hapa tena tukasema inakuwaje mtu anayetaka kuwa Rais anaona ni bora mgombea wa chama chake ashinde ubunge lakini yeye pia asipewe kura na hao hao anaoomba wamchague mgombea wake ubunge!? Kisa Lissu!

Kwa nini Jeshi zima la CCM huamia kwenye mapambano na Lissu kwenye kila jambo analolisimamia? Wakati Lissu anawatetea watu wa Bhulyankulu dhidi ya wachimbaji wawekezaji, CCM nzima ilikuwa kinyume chake. Leo wanadai anaogopa kesi wakati hajawahi kukosa kuhudhuria hata zile kesi wanazomzushia kila uchao.

CCM kwa nini inapagawa kwenye mambo mengi sana anayoyafanya Lissu?
Wajinga watadhani Lissu anawatisha CCM, lakini werevu washang'amua Lissu anawatisha Ukawa kutokana na kung'ang'ania mgombea wao wa kudumu wa Urais.
 
Nachofahamu ni kuwa Lisu alilalamikia utaratibu uliotumiwa JPM kuzuia usafirishaji mchanga.

Na alifafanua kuwa kwenye mikataba ya makubaliano Mchanga ni mali ya wawekezaji,hivyo alitoa tahadhari
 
..msikilize kwenye video.

..hicho ndicho wanachokiogopa ccm.

 
Ccm ni watupu,wanaogopa watu weny akili nyingi.
 
Amtishi mtu yuko kazini lakini tukumbuke tunampa kesi nyingi na Zote ameshinda ndo maana nasema yuko kazi
 
Japo ripoti itapokelewa leo,ila macho yote na masikio yote ni kwa Lissu...
Swali kubwa kwenye vichwa vya watu makini ni:"Lissu atajibuje?atasemaje..."!
Can't wait for that!
 
Back
Top Bottom